Simba Mkali
JF-Expert Member
- Jan 31, 2012
- 620
- 239
KWANZA ilianza na Wafanyabiashara wakubwa wale matycoon ambao walipelekeshwa puta kwelikweli.... kisha ikaja na wale waliowatumbua pamoja na familia zao, ikajikomboa kwa wamachinga ( hawa wanamfagilia Magu kwa kuwaruhusu kukaa barabarani).
Ikawapoteza wakazi wa Mkoa wa Kagera...hotuba ya Magu imewapoteza wapiga kura wengi wa mkoa huo. Baadaye ikaja kuwapoteza wasanii wa muziki na Bongofleva...kamatakamata ya madude.
Sasa imehamia kwa wanachana na mashabiki wa Yanga. Sijui lini itaamua kuwapoteza wale wa Simba? Bado CCM inaweza kubomoka zaidi kadiri siku zinavyokwenda mbele... 2020 hata wewe unaweza kuwa rais. Kwani itawapoteza zaidi Watanzania wanaolia na maisha magumu... kila kona ni kilio tu... unga 2000, sukari... mvua hainyeshi... duuu!