Kashaijabutege
JF-Expert Member
- Oct 20, 2010
- 2,696
- 740
Ati umefika wakati wa mwanamke kushika muhimili mmoja wa dola. Ratiba hiyo anayo nani? Ikiwa ipo, tuambiwe basi ni lini CCM imepanga mwanamke awe Jaji Mkuu. Si vibaya pia, CCM ikatanabaisha ni lini imepanga mwanamke apitishwe kugombea urais au umakamu wa rais.
Hizi hakika ni dalili za chombo kinachozama. Haingii akilini kumfanya mwanamke ni mtu wa kupangiwa saa ya kula, kujisomea, kucheza na kulala. Kwa hiyo leo CCM imeona mwanamke anafaa kuwa Spika; kwani wanawake hao hao hawakuwa na uwezo huo hata mwaka 1995? Huu ni uongo na udhalilishaji wa kijinsia.
Chiligati na Makamba watupe ratiba ya mwana mama kuwa Rais wa Tanzania, na Jaji Mkuu ili tujue kweli CCM inawependa wanawake.
Mapendekezo: Mwanamke ateuliwe na CCM kuwania nafasi ya Rais mwaka 2015 na awe Jaji Mkuu baada ya Jaji Ramadhani.