Wakudadavuwa
JF-Expert Member
- Feb 17, 2016
- 17,506
- 15,999
Katika imani ya Kikristo kuna andiko maarufu lina sema ''...watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa...'', hiki ndicho ninachokiona katika hii CHADEMA ya sasa. CCM wamefanikiwa kupandikiza watu wao ndani ya kamati kuu za maamuzi ndani ya CHADEMA na kufanikiwa kwa kiasi kikubwa kufanya watakalo. Kila wanaloongea, tenda, panga nk lazima lipate kibali kutoka Lumumba au kutoka kwa makada waliopandikizwa ndani ya CHADEMA.
Ajizi nyumba ya njaa, huku hayo yakiendelea wafuasi wengi wa CHADEMA waliojawa na ''hasira'' baada ya uchaguzi wameanza kukata tamaa na wale CHADEMA asili wakibaki mitandaoni hoi wasijue cha kufanya. Mida inayoyoma, tumeshuhudia jinsi Masha anavyotetewa kuliko Myinka, hakika huyu anayefanya mipango hii ndani ya CCM ni mwanamikakati mwenye mbinu kali sana katika medani za ujasusi wa kidola.
''Siasa ni sayansi'' Dr.W.P.Slaa ,01.09.2015.