CCM Inavyodhulumu Demokrasia Tanzania. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM Inavyodhulumu Demokrasia Tanzania.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mpaka Kieleweke, Jul 22, 2009.

 1. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #1
  Jul 22, 2009
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Hebu soma e -mail hii iliyokwenda kwa mweka hazina wa CCM Taifa.

  From: Gaudencia Ngetti <gaudencia.ngetti@yahoo.com>
  To: <amosmakalla@yahoo.com>

  Habari za muda huu ndugu yangu.

  Ninachotaka kuzungumza na wewe ni kwamba, ule mfululizo wa makala yangu ya MHIMILI WA SHETANI kweli imeleta mtikisiko mkubwa ndani ya Chadema na uhusiano wao na Mengi ambao ninauona kama ni wa kishetani na isiyoitakia mema nchi yetu na mustakabali wa Taifa letu.

  Imefikia hatua Mengi na washirika wenzie wameenda mbali kiasi cha kuiomba Mahakama nisiendelee kuandika makala hayo kwani inalenga kukidhoofisha Chadema kabla ya Uchaguzi Mkuu wa hapo mwakani.

  Kutokana na ushauri wa wasomaji wengi hasa wanazuoni wa UDSM sehemu ya mlimani wamenishauri nifanya mwendelezo wa makala hayo kuwa KITABU ili ujumbe niliokusudia uweze kuwafikia watu wengi nchini.

  Ni dhahiri kupitia kitabu hiki Chadema itaweza kudhoofika mno kwani kitawafunua utupu wao na watu kujua rangi yao halisi. Na ninadhani huu utakuwa ni mchango wangu kwa chama tawala na kwa nchi yangu.

  Ninachoomba kwako ni kasma ya kuniwezesha kuchapa kitabu hicho na kukisambaza. Kwamba nipate wadhamini wa kuniwezesha kukichapa kitabu hicho na kukisambaza ili kisambae nchima watu wakifahamu Chadema kwa rangi yake halisi.

  Gharama zote za uchapaji na usambazaji ni jumla ya shilingi 21,000,000 (Milioni ishirini na moja tu). Unaweza kunisaidia aidha kama chama, kama Makala au kwa kuniunganisha na watu unaodhani wanaweza kunikasimisha ili shabaha yangu ya kuona Chadema inadhoofu kabla uchaguzi mkuu mwakani INATIMIA.

  Ni matumaini yangu kuwa utalichukulia suala hili VERY SERIOUS.

  Ni mimi Bollen Ngetti
   
 2. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #2
  Jul 22, 2009
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Huyu Bolleni Ngetti ni miongni mwa wamiliki wa gazeti la SAUTI HURU , na pia kila kukicha anaandika kuhusu CHADEMA na huwa anapewa matangazo ya serikali wakati gazeti lake likiwa haliendi hata mikoa 4 nchini.

  Huyu ni mtu ambaye anajiita kuwa ni mwandishi makini akishirikiana na mhariri wa kagazeti hako anayejulikana kama IDD MUKWAMA .

  Watu hawa wanaweza kuwa hatari sana kwa Taifa kama wakiachwa waendelee kuandika uchochezi wao huku wakipewa fedha na CCM makao makuu.

  CCM inaweza kufanya lolote mradi iendelee kubakia madarakani hata kama ni kwa kuwatoa roho watanzania ili mradi kufanya hivyo kunawapa fursa ya kuendelea kutawala .
   
 3. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #3
  Jul 22, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Kwa hiyo jamaa shughuli yake ni kuisambaratisha tu CHADEMA?, sijawahi soma makala zake, lakini anachekesha, anatia huruma, anatia aibu. Japo sina chama, ila huyu jamaa kuna jambo analitafuta kwa CCM.
   
 4. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #4
  Jul 22, 2009
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Ameandika mfululizo wa makala 16 aliyoipa jina la CHADEMA ni mhimili wa Shetani na makala zote amekuwa akimhusisha Mengi na harakati za CHADEMA kwa hisia tuu bila hata ya kuweka hata chembe ya ushahidi kidogo.

  Anachokitafuta CCM ni kupata fedha 21 milioni za kuchapisha kitabu chenye makala zake na kama ukisoma utaona kuwa lengo lake ni kuidhoofisha CHADEMA kabla ya 2010.
   
 5. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #5
  Jul 22, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,098
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  njaaaa ya mawazo inayochochewaa na upeooo mdogoooo
   
 6. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #6
  Jul 22, 2009
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Kutokana na uroho wa pesa waandishi kama hawa wanashindwa hata kusimamia taaluma zao.
   
 7. L

  Lukundo Member

  #7
  Jul 22, 2009
  Joined: Feb 19, 2009
  Messages: 61
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  JAMAA ANASIKITISHA. KWA E MAIL YAKE HIYO MBONA KAJIANIKA. NAFIKIRI ATAKACHOKIPATA KUTOKA HAPA KITAMFANYA AOGOPE HATA KUPITA MITAA YA DAR KAMA KWELI E MAIL ZAO HIZO NI GENUINE. CCM KWA STYLE HIYO KAZI WANAYO. HAYO NDO MAGAZETI YALIYOLALAMIKIWA WIKI ILIYOPITA NA BUNGE, HALAFU ANNA MAKINDA AKAYEYUSHA ILI MKUCHIKA ASIJIBU SWALI LA VIJIGAZETI HIVYO KUPEWA TENDA ZA KUSAMBAZA HABARI ZA SERIKALI WAKATI REACH ZAO NI NDOGO SANA.

  TANZANIA KAZI IPO KWELI, NA SAFARI BADO NDEFU. HEKO mpakakieleweke kwa kuleta hii.
   
 8. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #8
  Jul 22, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Tuwaandikie barua tukiwaambia ukweli kwamba ndege ya Chadema ilishapaa na hakuna wa kuishusha, labda kama kawaida yao wajanja wanawaibia sisi maf... kwa njia hiyo.
  Kisha wanategemea kupata na tucheo kama Salva!
   
Loading...