Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,479
- 30,144
Kama alivyonukuliwa Katibu Mkuu wa CCM, Dkt Bashiru Ally hivi karibuni "akijimwambafai" kuwa Chama chake cha CCM, kitaendelea kubaki madarakani milele na milele, kwa kutumia vyombo vyote vya dola vilivyopo nchini ambavyo kama alivyonukuliwa yeye mwenyewe kuwa wao ndiyo wanavimiliiki!
Akimaanisha kuwa vyombo vyote vya dola nchini, kama vile Jeshi la Polisi nchini, maRC na maDC, wakurugenzi wa wilaya, Tume ya uchaguzi ya Taifa, pamoja na vyombo vya habari vya Umma na binafsi vyote vitahakikisha katika uchaguzi ujao, ni lazima CCM inapata ushindi wa kishindo!
Ingawa chama cha CCM ni chama cha siasa, hata hivyo kinajipambanua kuwa chama hiko ni chama dola, ambacho hakitegemei tena ushawishi wa kisiasa majukwaani, bali chenyewe kinategemea mabavu ya vyombo vya dola, kuendelea kulazimisha kubaki madarakani.
Kwa mazingira hayo, vyama vya upinzani hapa nchini, vimekuwa kama watoto yatima, ambavyo vyenyewe vinategemea tu nguvu ya ushawishi kwenye majukwaa ya kisiasa, ili viaminike kwa wananchi wa nchi hii na kupigiwa kura, kwenye sanduku la kura na kuzilinda kura hizo ili zisihujumiwe na CCM kwa "kusaidiwa" na vyombo hivyo vya dola nilivyovitaja
Hata hivyo wananchi wote tumeshuhudia kuwa katika awamu hii ya utawala wa awamu ya tano, hata hayo majukwaa ya kisiasa ni CCM pekee ambao wameachiwa wakijidai, inapotokea vyama vya siasa makini, kama Chadema, nacho kikitaka kufanya siasa ya majukwaani, Jeshi la Polisi linajitokeza kwa kuzuia mikutano hiyo!
Kwa mazingira hayo ni kuwa vyama vya upinzani vinakuwa katika mazingira magumu sana, wakati Taifa likiingia katika uchaguzi mkuu baadaye mwaka huu, ukilinganisha na CCM, ambacho chenyewe kimejiita bila aibu kiwa ni chama dola, ambacho kama Katibu Mkuu wa chama hicho cha CCM, Dkt Bashiru Ally, alivyoeleza kuwa kinabebwa katika kila hali na vyombo vyote vya dola nchini!
Kwa hiyo kama mwito wa chama kikuu cha upinzani nchini, cha Chadema, ambao umetolewa kwa vyombo vya habari, ukiwaambia watanzania kuwa wao vyama vya upinzani nchini, wamebakiwa na "option" moja pekee nayo ni kuwa-mobilize wananchi katika kutumia nguvu ya Umma, ili kuhakikisha kuwa uchaguzi mkuu ujao, unakuwa huru na haki na wakaendelea kusisitiza kuwa wasitishwe na vyombo vya dola, vikiongozwa na Jeshi la Polisi nchini, kwa kutaka kuuvuruga uchaguzi huo
Tutambue tu kuwa katika historia, hakujawahi kutokea mahali popote duniani nguvu ya dola, yaani mapolisi, ikaishinda nguvu ya Umma iliyojizatiti
Mungu ibariki Tanzania, ili watawala wake wawe na busara na kuona umuhimu wa uchaguzi mkuu ujao, sanduku la kura ndilo liamue viongozi wetu wajao na wasiuvuruge uchaguzi huo na kusababisha kuleta machafuko nchini na umwagikaji wa damu