Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,735
- 40,858
Na. M. M. Mwanakijiji
Kuna mambo mengi ambayo tunaweza na tayari tumeishaibebesha lawama CCM kama chama tawala. Tunaibebesha CCM kwa sababu ndicho chama ambacho sera zake za kiutawala ndizo zimekuwa zikijaribiwa miaka nenda rudi tangu uhuru. Kimsingi, hakuna jambo lolote linalofanyika, lililowahi kufanyika au litakalofanyika katika miaka hii hadi 2020 ambalo halitahusiana na sera za CCM.
Mafanikio na matatizo mbalimbali ambayo tumeyaona kwa miaka hii 55 tangu uhuru yanafungana moja kwa moja na uongozi na mwelekeo wa chama tawala. Tunaweza kuilaumu CCM kwa matatizo ya elimu, afya, maji, usafiri, n.k na yote haya naamini ni kwa haki kabisa wanastahili lawama.
Hata hivyo, naamini katika miaka hii arobaini ya CCM ilivyo sasa kuna jambo moja kubwa Zaidi ambalo CCM inastahili lawama na sioni ni namna gani itaweza kuondokana nalo kwani ni kana kwamba CCM na serikali yake na wao wenyewe wamekuwa watumiaji wa madawa ya kulevya ya jambo hili.
CCM imetengeneza utegemezi uliopitiliza (extreme dependence) ya misaada ya kila namna. Kwa CCM misaada hii imekuwa kama cocaine! Kwamba, kila kukicha serikali an vyombo vyake (wakitekeleza sera mbalimbali za CCM) wanajikuta wakitafuta misaada ya kila namna ili kuifanya serikali na maisha ya nchi yaende. Ni sawasawa na vijana ambao wakiamka wanahitaji kupata dozi kidogo ya heroine, meth au crack cocaine ili maisha yao yaende.
Katika somo la Pharmacology 101 (utangulizi juu ya elimu ya madawa) mojawapo ya mambo ya awali kabisa mtu anajifunza ni kuelewa ni kwanini dawa zinaandikwa kwa dozi na si vinginevyo. Mtu ambaye anatumia madawa halali anaishi kwa kufutuata matumizi sahihi ya dawa hizo lakini akifanya vibaya au akijifanyia kivyake kivyake ama dawa haitofanya kazi, anaweza kujudhuru au anaweza kutengeneza (kwa madawa ambayo ni addictive) dependency.
Misaada ya kigeni ni mojawapo ya madawa addictive sana kwa nchi kuliko kitu kingine chochote. Kama vile madawa haramu yanavyoweza kumfanya mtu atende kama mwendawazimu akikatishwa kwa ghafla au kunyimwa ndivyo ilivyo kwa misaada ya kigeni. Taifa ambalo linategemea misaada ya kigeni linakuwa katika huruma ya wale wanaotoa misaada hiyo na wanapokosa ni kama hawawezi tena kufikiri na badala yake wanajawa na kila dalili ya watu waliokosa madawa (withdrawal symptoms); watu wanakuwa wana wasiwasi, mioyo inaenda mbio, na wako tayari kufanya lolote ili wapate "shot" kwenye mishipa yao ya damu.
Hata hivyo, hilo la misaada ni utegemezi mmoja lakini siyo ambao ninailaumu CCM sana kwayo.
Nailaumu sana CCM kwa kutengeneza utegemezi wa kifikra (intellectual dependence). Kwamba, tunategemea watu wengine kutufikiria namna ya kutatua matatizo yetu kiasi kwamba sisi wenyewe hatuamini kuwa tuna uwezo wa kuyatatua kama tukifikiria vizuri na kuamini katika ubora wa fikra zetu!
Hata Rais Magufuli - kwa masikitio yangu - bado hajaonesha kwua taifa linaweza kweli kuacha kunyonya titi hili la misaada miaka 55 baada ya kuzaliwa kwa taifa letu. Bado hajaweza kuonesha anaweza kuongoza taifa na kusimamia lijiendeshe bila kutegemea misaada. Kwamba, kama kuna taifa linalotaka kutusaidia lifanye hivyo kwa kupitia uwekezaji na masuala ya biashara, mambo ya misaada yakomeshwe. Kama alivyowakatalia watu wa Kagera kuwa wakisubiriai misaada "waafwa" ninaamini wakati umefika kuiambia serikali yake na Watanzania kuwa zama za misaada zimekwishwa na anayesubiria misaada ili kupanga bajeti yake "aaafwa"!
Ni lazima wasomi wetu, watu wetu na viongozi wetu kufikiria nje ya the addictive potency of foreign aid!
Nje ya hapo, sijui nani tutamuambia tukutane naye Central ili kutafuta namna ya kutibu ugonjwa mkubwa wa fikra haramu za kutegemea misaada!!!