TAI DUME
JF-Expert Member
- Feb 20, 2014
- 8,846
- 23,090
Subal kheri Watanzania. Ni ndefu kidogo kama mvivu wa kusoma omba samari kwa jirani yako.
Kwa wale wapenzi wa muziki hususani mziki wa kufoka foka wanaelewa maana ya kunata na beat. Kwa wasioelewa ni kile kitendo Cha rapper kuimba sambamba na mdundo bila kuuacha nyuma au kutangulia mbele.
Sasa Basi kwa miaka mitano ya JPM, CCM kwa kiasi kikubwa imekuwa ikitekeleza sera au matamanio ya CDM waliyokuwa wanayapigia kelele kwa muda mrefu. Inawezekana kwa kujua au kutokujua. Ni wazi kwa kipindi hiki nchi iliendeshwa kwa matakwa ya CHADEMA. CCM haikutekeleza sera take isipokuwa ya CHADEMA.
No wonder hata mkuu wa kaya aliwapiga ban wapinzani kufanya siasa ikiwa ni ujumbe kwamba mnataka Nini Tena wakati yote mliyokuwa mnayalilia tunayatekeleza kwa vitendo. Inawezekana pia hii ikawa ni sababu ya baadhi ya wapinzani kuunga mkono juhudi za mwenyekiti iwe kwa hiyari au kuhiyarishwa.
Nitazungumzia machache.
Mosi, CHADEMA walikuwa wanataka rais mkali asiyecheka cheka hovyo. CCM ikawapa JPM.
Pili, CHADEMA walikerwa Sana na viongozi wakuu kusafiri safiri nje. Wakafikia hatua ya kusema CCM inaweza kubinafsisha nchi huko ulaya kwa kusaini mikataba hovyo hovyo. Kilio kikasikika JPM akapiga ban safari za nje.
Tatu. CHADEMA walisema hatuwezi kukuza utalii nchini Kama hatutafufua shirika la ndege. Tena kipindi kile shirika lilikuwa Lina ndege moja tu mbovu Tena ya kukodi. JPM akasema hewala, wengi wape ila wachache wasikilizwe. Wakasikilizwa na kupewa kabisa, Mungu awape Nini Leo shirika Lina midege ya kutosha.
Nne, CHADEMA walipigia Sana kelele ufisadi uliopo TANESCO. Kwamba shirika linajiendesha kwa hasara na halitoi huduma stahiki. JPM akaangalia mikataba ilivo pale akaona dawa ni kutafuta chanzo Cha umeme Cha uhakika. Akaja na stigglers gouge. CDM are very lack yaani kila kitu wanasikilizwa.
Tano, CHADEMA walichafukwa mno na utendaji mbovu wa watendaji wa serikalini, kwamba wengi wamewekwa kwa kujuana na hawana vigezo. Yaani wenye vyeti feki au wasionavyo kabisa ndio walioshikilia Ofisi za umma. Again JPM akaanza nalo Hilo. Waliowakera CHADEMA wote wakafyekelewa mbali.
Sita, CHADEMA walilalamika Sana miradi ya serikali haionekani na pesa zinatolewa. Yaani walikuwa wanataka kuona matokeo ya matumizi ya pesa za serikali. Wakafika mbali kulalamika kwamba miundo mbinu Kama barabara, reli na majini ndio backbone ya uchumi. JPM bwana maikivu sana hachoki. Akasema Sasa mtaona matokeo ya fedha zenu. Reli hii hapa, mabarabara njia kumi hayo hapo, madaraja sijui flyovers hizo hapo. Asee Mimi niaingeweza.
CHADEMA hao hao walilalamika Sana kuhusu Ada zinazotozwa mashuleni na kupelekea watoto wa masikini kunyanyasika. Ni kweli hii pia ilikuwa kero. Kilio kikasikika tatizo likapatiwa dawa.
Saba. Akh yapo mengi Sana yanafika hata 50 mengine mtajazia wenyewe msinichishe.
HOJA YANGU NI IPI SASA??
1. Ni kwamba vyama vyenye mawazo mbadala vikiwa makini Kama chadema, CCM itajikuta inacheza ngoma za upinzani kwa kutaka au kutokutaka.
2. Upinzani ili uweze kuongoza nchi sio lazima ungie madarakani. Wakiwa smart wanaongoza nchi kwa remote control huku wao wakiwa wanaongeza familia majumbani kwao.
3. Watanzania tusiwe na wasiwasi, hizi sera nzuri nzuri za cdm, CCM inazichukulia kwa uzito na kwa uhakika zitatekelezwa miaka mitano ijayo. Tena mengine yameshaanza kutekelezwa, juzi tuu zimetoka ajira elfu 13 baada ya CHADEMA kulalamika walimu hawajaajiriwa kwa miaka mitano. CHADEMA are luck utafikiri yule mwana mpendwa aliyekuwa anasikilizwa Sana.
Point ya kufungia Uzi wangu.
Sasa hivi CHADEMA wanakuja na hoja za kutaka maendeleo ya watu, hata rungwe amefikia hatua kugawa ubwabwa ikiwa ni msisistizo huduma Sasa ziende moja kwa moja kwa watu. Binafsi naamini in case CHADEMA wasipochukua nchi, JPM ni msikivu na atayatekeleza hayo kwa vitendo. Wapinzani turelax hoja zetu zinatekelezwa kwa remote control watake wasitake.
Mwisho mwishoni.
Kura nitapiga ya ubunge na diwani tuu, ya rais sipigi kwani nipige nisipige fidodido atashinda tuu.
Wasalaam