CCM Inapenda Kuongoza Umeya Maeneo Yote Dar es Salaam

Hismastersvoice

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
18,595
22,200
Kama kawaida CCM imekuwa ikichukua madaraka ya umeya maeneo yote ya Dar, wakishachukua wanatulia kwani wanaona wamemaliza kazi! Mbagala ni eneo llilo nchini ya meya toka CCM na ni eneo lililokithiri kwa uchafu wa mitaro ya maji ya mvua.

Mbagala ina barabara moja tu ya lami nayo ni barabara ya Kilwa, barabara hii hivi sasa imefunikwa na mchanga kiasi haijulikani kama ni ya lami, swala la mitaro ni kubwa kwani imejaa taka zilizozolewa na mvua na ndizo zilizokuwa zikisababisha barabara kufunikwa na maji, ukweli Mbagala kunanuka kiasi hata nzi wamekimbia!

Kwa hali ya kawaida mtu kung'ang'ania kazi ili aifanye kwa ufanisi lakini kwa CCM ni kinyume!
 
Back
Top Bottom