CCM inanyonga Watanzania kwa kutumia rasilimali zao | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM inanyonga Watanzania kwa kutumia rasilimali zao

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MPadmire, Mar 17, 2011.

 1. M

  MPadmire JF-Expert Member

  #1
  Mar 17, 2011
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 2,628
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Kwa mfano kodi na mrahaba serikali ya CCM inayokusanya kutoka kwa uwekezaji haswa wa mali asili zetu, inawafadishaje watanzania?

  Nasisitizia vitu ambavyo vinaweza kutumika hapa Tanzania kwa manufaa ya watanzania.

  Angalia Natural gas ya Songosongo. Kwa nini Watanzania wasipate Nishati mbadala ya bei rahisi.

  Sasa kama gesi inapatikana bure kutoka kwa Mungu, sisi/wawekezaji wameweka tu gharama za uchimbaji, inakuaje bei ya gesi isiwe bei rahisi??

  Nini kinasababisha gesi iwe bei ghali?

  Pia kwa nini makaa ya mawe pia yakatengenezwa katika mfumo wa kutumika ili kuokoa misitu yetu.

  Jamani ni recycle ni obvious kabisa. Angalieni wajameni Misitu ndo inahifadhi maji, na maji ndo tunayataka kwa hydro electric generation.

  Sasa kama tunamaliza misitu ya asili kwa mkaa, umeme huo utakuwa historia Tanzania.

  Haya Kilimo Kwanza. Mbolea ya Minjingu inachimbwa pale Minjingu barabara ya Babati.

  Hiyo phosphate si bure tumepewa na Mungu, kwa nini mbolea iuzwe ghali hivyo??

  na mengi mengi Wana JF na watanzania kwa ujumla mnaweza kuongezea.

  TATIZO Ni Upopompo wa Viongozi katika CCM.

  Ubinafsi na u.pum.bafu, kwa nini utelekeze watanzania na mabilioni kwa ajili ya 10%??

  hao wasaliti wanyongwe, ni akina nani jamani
   
 2. M

  MPadmire JF-Expert Member

  #2
  Mar 17, 2011
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 2,628
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Na sehemu nyingine ni pamba, kwa nini tununue nguo nje?
   
 3. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #3
  Mar 17, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  SHAMBULIO KWA MWANA-JF MMOJA NI SHAMBULIO KWA WANACHAMA WETU WOTE 35,000 KOTE WALIKO DUNIANI NA NDANI YA VYOMBO MBALIMBALI VYA SERIKALI HUMO

  Kama mpango mzima wa kuwawekeni Uenyekiti wa Kamati za Bunge (Lowassa, Kabwe na January Makamba) ilikua ni kutumbukiza tena kwenye biashara ya ma-hayawani DOWANS mara Richmonduli ambazo ni mali zake Rostam Aziz, basi bora msahau mapemaaa maana nanyi mtakwenda na maji kwenye mkumbo huo huo!!

  Wajanja Tanzania wapo wengi sana zaidi yenu nyie hapo. Pili muelewe kwamba sera yetu hapa JF ni kwamba mwenzetu mmoja (kama alivyo hivi sasa mwenzetu Mzee Mwanakijiji) akishambuliwa visivyo kama ambavyo Zitto Kabwe ameruhusu kamati yake kufanya dhidi ya mmoja wetu basi mjue ya kwamba tayari mtakua mmetangaza vita na Jamii Forum kwa ujumla wake bila kujali itikadi zetu tofauti humu ndani.

  Wasiwasi wangu tu ni kwamba Kamati ya Zitto Zuberi Kabwe na watu wanaowatuma kuishambulia JF hivi kweli MTANANGE HUU MTAUWEZAAA???
   
 4. p

  plawala JF-Expert Member

  #4
  Mar 17, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 627
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jambo la muhimu ni elimu ya kiraia,hili ndilo tatizo letu watanzania,upungufu wa elimu hiyo,na utamaduni wa kuaminiana na kuvumiliana,sasa tumeshajua tunaibiwa kwa sababu ya kuwaamini tuliowapa dahamana ya kusimamia rasilim ali zetu
  na ni tatizo ambalo lipo mpaka kwa watu waliofika chuo kikuu,kuna watu wanasoma vyuoni leo hii hawajui dowans ni nini
  tukishajua mali asili zetu ni nini na zinaweza kutusaidiaje hatua ya pili ni kukataa ujanja ujanja wa kuzipora kupitia uwekezaji uchwara na mikataba ya kinyonyaji(ambayo imeshaanza kwa kasi miaka mishache iliyopita)
  tushirikiane kuzidi kusambaza elimu ya kiraia tunakaribia kushinda sasa
   
 5. M

  MPadmire JF-Expert Member

  #5
  Mar 18, 2011
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 2,628
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Naipongeza sana chadema kwa kutoa elimu ya uraia na kuwaelimisha watanzania jinsi wanavyongwa.

  Ndo maana ccm wana haha maana wameshtukiwa...

  Nani atawapa wezi kura...?

  Watabaki kuchakachua kura tu...

  Na katiba mpya yaja, hakuna kuchakachua...
   
Loading...