CCM "inaipaisha" CHADEMA

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,800
Sasa ni kero. Ni kero chamani kwakuwa CHADEMA inatangazwa na kujulikana. Hakuna kiongozi hata mmoja wa chama chetu cha Mapinduzi ambaye anaweza kuhutubia,kijijini au mjini,bila kuitaja na kuinanga CHADEMA. Midomoni-CHADEMA;kwenye vyombo vyetu vya habari-CHADEMA;katika ofisi zetu-CHADEMA na mitandaoni-CHADEMA. Inakera kwakweli. Na kwa sisi wazoefu wa siasa za nchi hii,tunauona huo ni kama mchezo mchafu unaochezwa na viongozi na makada wetu.Mchezo wa kuitangaza CHADEMA.

Mwalimu Nyerere alikuwa Mwenyekiti wa kwanza wa CCM. Hadi kifo chake hapo 1999,aliwahi kutoa hotuba kwa mamia.Hakuna hata hotuba moja aliyotaja chama pinzani chochote kiwacho nchini. Aliitangaza CCM;akaitetea CCM na kuwafanya wananchi hasa wa vijijini waijue CCM tu. Basi.Lakini sasa tofauti.

Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi alikuwa Mwenyekiti wa pili wa CCM.Alihutubu kama Nyerere.Kuitaja CCM tu.Vivyohivyo kwa Rais Mstaafu Benjamini William Mkapa-Mwenyekiti wa tatu wa CCM. Lakini, uongozi wa sasa unaona ufahari kutaja CHADEMA na viongozi wake katika mikutano yake yote.Tena kwa mabaya tu.

Badala ya kujielekeza katika kuichambua na kuielezea Ilani ya CCM ya 2010-2015 na jinsi inavyotekelezwa,hotuba hutekwa na CHADEMA tu. Huu ufahari una walakini. Haufai.Amini nawaambia,vipo vijiji na vitongoji havijawahi kuijua CHADEMA wala chama kingine cha upinzani tangu uhuru.Kwasasa wanavijua.Kupitia vinywa vya wana-CCM.Makosa kabisa. Tutapitaje bila kupingwa katika baadhi ya maeneo wakati wa uchaguzi kama tulivyozoea?

Kama viongozi na makada wetu wa CCM wameamua kuvitangaza kwa nguvu zote vyama vya upinzani nchini,basi tuweke kama sera ya chama na tuitekeleze.Na sisi tutatii matakwa ya chama. Kiujumla,CCM yenyewe ndiyo inayoipaisha CHADEMA kwa kuizungumziazungumzia.

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
 
ccm hawalali kwa sababu ya chadema. Yaani automatic walishakuwa affected na chadema nouma sana.
 
Tatizo ni kuwa CCM hawana sera zinazovutia wananchi tena kama chadema kilivyo. Miezi miwili mitatu walipiga kelele sana kuwa bomba la gesi likijengwa TOKA Ntwara, kwanza tutapata umeme wa uhakika na bei yake itashuka. Sasa wakati kazi ya bomba ikiendelea kwa kasi wanataka kupandisha bei ya umeme, tena kwa kashfa kuwa wasiotaka ipande watumie vibatari. Kwa nini wanadanganya wazi hivyo? Kupandisha bei ya umeme ndo maisha bora kwa kila Mtanzania? Au ni kwa sababu ya vuguvugu lile la Wanantwara limekwisha?? Kwa sasa hawana lingine la kusema badala ya kuimba CHADEMA!
 
watasema nini lazima waseme habari ambazo wananchi wanataka kuzisikia ziwe mbaya au nzuri wananchi wanachekecha na kuwaponda kwa nguvu zao zote KInana anachekesha yeye nape migiro wanalalamika safari nzima wanailalamikia serikali yao kama vile ccm sio sehemu ya serikali wakidhani wanasaidia serikali kumbe ni mtaji wa upinzani
 
Hili gamba lingefaa liungane na makamanda kukomboa nchi.lina akili sana hili gamba.
 
Sasa ni kero. Ni kero chamani kwakuwa CHADEMA inatangazwa na kujulikana. Hakuna kiongozi hata mmoja wa chama chetu cha Mapinduzi ambaye anaweza kuhutubia,kijijini au mjini,bila kuitaja na kuinanga CHADEMA. Midomoni-CHADEMA;kwenye vyombo vyetu vya habari-CHADEMA;katika ofisi zetu-CHADEMA na mitandaoni-CHADEMA. Inakera kwakweli. Na kwa sisi wazoefu wa siasa za nchi hii,tunauona huo ni kama mchezo mchafu unaochezwa na viongozi na makada wetu.Mchezo wa kuitangaza CHADEMA.

Mwalimu Nyerere alikuwa Mwenyekiti wa kwanza wa CCM. Hadi kifo chake hapo 1999,aliwahi kutoa hotuba kwa mamia.Hakuna hata hotuba moja aliyotaja chama pinzani chochote kiwacho nchini. Aliitangaza CCM;akaitetea CCM na kuwafanya wananchi hasa wa vijijini waijue CCM tu. Basi.Lakini sasa tofauti.

Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi alikuwa Mwenyekiti wa pili wa CCM.Alihutubu kama Nyerere.Kuitaja CCM tu.Vivyohivyo kwa Rais Mstaafu Benjamini William Mkapa-Mwenyekiti wa tatu wa CCM. Lakini, uongozi wa sasa unaona ufahari kutaja CHADEMA na viongozi wake katika mikutano yake yote.Tena kwa mabaya tu.

Badala ya kujielekeza katika kuichambua na kuielezea Ilani ya CCM ya 2010-2015 na jinsi inavyotekelezwa,hotuba
hutekwa na CHADEMA tu. Huu ufahari una walakini. Haufai.Amini nawaambia,vipo vijiji na vitongoji havijawahi kuijua CHADEMA wala chama kingine cha upinzani tangu uhuru.Kwasasa wanavijua.Kupitia vinywa vya wana-CCM.Makosa kabisa. Tutapitaje bila kupingwa katika baadhi ya maeneo wakati wa uchaguzi kama tulivyozoea?

Kama viongozi na makada wetu wa CCM wameamua kuvitangaza kwa nguvu zote vyama vya upinzani nchini,basi tuweke kama sera ya chama na tuitekeleze.Na sisi tutatii matakwa ya chama. Kiujumla,CCM yenyewe ndiyo inayoipaisha CHADEMA kwa kuizungumziazungumzia.

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
Wanataabu kidogo yakiufahamu,anaye wadanganya hasa ni Mwigulu.Huwezi kuua cdm kwa pupa utajikuta unaipaisha.Fikiria pale walipo anza kuweka ndani viongozi cdm.Pale waliipaisha sana.mpaka wanasituka imesha paa
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom