CCM inahitaji kujenga au kuimarisha "Youth Nationalist Wing", hii ndio sababu?

Hisha Sorel

Senior Member
Dec 27, 2017
192
140
Falsafa wanzilishi ya Tanzania, Ujamaa, ilielewa uhusiano kati ya rangi ya ngozi, ukoloni, na ukandamizaji.

Hivyo ilikuwa na lengo la kuondoa dhana ya kudharilishwaji wa ngozi Nyeusi kwa kutokomeza sababu zinazochangia kupitia programu tofauti, mojawapo ikiwa elimu ya uzalendo .

Lengo kubwa lilikuwa ni kuzalisha Taifa la watu ambao waliamini thamani yao kama wanadamu na wenye ujasiri wa kutosha kutetea utu wao.

Ni wazi kuwa malengo haya hayakufanikiwa.

Katika hotuba yake kwa mawaziri wapya walioteuliwa, Rais Magufuli alidokeza juu ya shida hii ambayo alihusisha ujinga wa vijana wa Kitanzania wa historia na upendeleo kwa ushawishi wa nguvu za kigeni.

Ingawa ni kweli, ukosoaji wa rais haukuwa wa kutosha

++++

Hawana uelewa mpana wa masilahi yao, Hawana uelewa wa sehemu yao ndani ya Dunia.

Chuki binafsi ni dhahiri kwani bidhaa za kuchubua ya ngozi zinauzwa wazi na kununuliwa bile kelele zozote.

Vijana wa Tanzania HAWANA kabisa maarifa ya siasa za Rangi ya ngozi au Ubaguzi,

Siasa zao ni za kishabiki bila ufahamu mpana hivyo kuifanya iwe rahisi kwao kudanganywa kusaidia sera zenye faida kwa mabepari.

Ujuzi wao juu ya dhana nyepesi kama ukoloni umepotoshwa sana na wengine hata wanapongeza ukoloni na ubaguzi wa rangi (apartheid).

Hapa tunapozungumza wanawake wadogo wa Kitanzania wanasafirishwa nje ya nchi kwa unyanyasaji wa kijinsia kwa kisingizio kwamba ni watumishi wa ndani.
 
Umbumbumbu huo - kutojitambua na kujithamini kama mtanzania, muafrika na binadamu unachagizwa pia na wale tunaowaona kama viongozi wetu! Mfano ni mtu kama Lissu ambaye ni kiongozi wa kitaifa, yeye anaona mtu kuongea kingereza - ni basi umeukata na una uwezo mkubwa sana kimaisha na ni wewe tu unapaswa kuongoza wenzio! Hiyo ina tofauti gani na kujichubua ngozi ili uwe mweupe?
Nakubariana na wewe na rais Magufuli kwamba uzalendo upewe kipa umbele.

Nafikiri Bwana Lissu kuwepo Bubiligi (Belgium) - kutamfundisha kuwa Kiingereza siyo kila kitu! Maana mitaani Bubiligi ukisikika unaongea kiingereza, wanakushangaa kama ilivyo hapa Bongo.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom