CCM inafirisi nchi kwa kununua watu ili waipende. Wanatoa wapi pesa?

tikatika

JF-Expert Member
May 6, 2011
2,330
4,119
Baada ya sekeseke la madawa na hata kabla ya hapo kuna malalamiko ya watu wengi kuifanyia kazi CCM na kutolipwa!! Nashawishika kuamini kila aliye CCM yupo pale kwa masrahi !! Hakuna hata mmoja asiye lipwa kwa kuipenda CCM. Je CCM inatoa wap hela za kuwalipa watu wote wanaokisifu chama hicho??

Kuna watu watakuja na maneno kwamba ina vyanzo vya mapato vingi nchi nzima. Ikiwemo na ruzuku , wakiwa na maana wanawalipa kupitia hivyo. Iweje ipite miaka miwili wasiweze kuwalipa kupitia vyanzo hivyo? Nashawishika kuamini baadhi ya tuhuma za huko nyuma kama meremeta kwamba zilitumika na chama na wakasingizia zimetumika na jeshi hazipaswi kuhojiwa zinaweza kuwa kweli.

Nayakumbuka majibu ya zakia meghji akijibu bungeni na ikaja thibitika ni ya uongo!! Hivyo nahisi kuna mapigo wanayaandaa ili yaje kusawazisha madeni yao. Maana sion biashara mpya itakayo lipa madeni yao kwa mara moja zaid ya kutegemea pigo kutoka sehem fulani.

Kwa maneno ya wale wasanii hakuna mtu anayekipenda CCM bila kununuliwa. Watu tulisema akina Ray kigosi kuhama ukawa na kujiunga na CCM kanunuliwa mlipinga leo yamekua waz walinunuliwa. Hii ina maana hakuna mtu maarufu anayekisaidia CCM ila CCM inawasaidia wao.

Sasa naamin woote mlio CCM mnapendeza kupitia CCM. Ndugu wana ukawa tusishawishike kununuliwa na hawa CCM bali tukubali kutoa mali zetu ili tuikomboe tanzania mikononi mwa hawa wanaogawana mali za nchi yetu.

Rejea mwaka jama ililipotiwa wafanyakazi wao wa uhuru publishers hawakulipwa miez saba! Kama wanewalipa zimetoka wap kama watawalipa zitatoka wapi ??? Hawa watu kuna pigo wanataka kutupiga wachote pesa zetu kusawazisha chama mambo yao.

Ndugu watanzania kuanzia sasa tuwe makini hawa ccm nahisi wanampango wa kutuibia ili walipe madeni ya watu. Lejea shigongo wema na leo mjane wa Komba. Wengine watakua wanadai kimya kimya.

Masikitiko!!

Kumbe nyie wote mnaokisifu CCM mnalipwa!!
Lizaboni na wenzako kumbe mnalipwa!!
Hamuwezi kukataa kwamba hamlipwi ili hali wale wakata viuno wanakiri hadharani wamelipwa. Nyie ni wafia CCM zaid ya wale wasanii!! Lazima mnalipwa. Nyie ndio mnaoifirisi Tanzania. Zile buku saba itakua zimeongezeka ila mnawadai hamjalipwa!!
 
Back
Top Bottom