CCM inaendeshwa na Serikali, Wakati Serikali inaendeshwa kwa remote na CHADEMA, Je hii ni KWELI? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM inaendeshwa na Serikali, Wakati Serikali inaendeshwa kwa remote na CHADEMA, Je hii ni KWELI?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by fikirikwanza, Jun 18, 2012.

 1. f

  fikirikwanza JF-Expert Member

  #1
  Jun 18, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 5,935
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Nimesikia mara kadhaa kwenye vyombo vya habari madai kuwa CCM imekuwa ikiendeshwa na serikali, wadau hawa wa mambo ya siasa nchini wamekwenda mbali zaidi na kudai CCM ingekuwa makini isingekubali kuendeshwa na serikali maana serikali inawajibika kwake.

  Katika kuonesha udhaifu huo, wadau wa siasa nchini, wamesema CCM, inapaswa hata kusimama majukwaani na kuikosoa serikali kitu ambacho kingeipa umarufu kwa umma, mfano ilitolewa mingi kuhusu Mwakyembe, Filikunjombe, Sitta na wengine kuwa wamepata umarufu kwa kuikosoa serikali na sio kwa kuitetea. Hivi sasa huwezi jua serikali iko wapi na CCM iko wapi, tunachoona ni CCM kufuata maelekezo ya serikali badala ya serikali kuagizwa na CCM. Mawaziri wa serikali ndo wanahutubia kwenye mikutano ya CCM, tena ndo wasemaji wakuu kama kwamba chama hakina viongozi wake, hakina watu wakukisemea hadi serikali iseme. Nape na siasa zake za kitoto haziwezi kuokoa CCM, wababe wa siasa kama malecela maarufu kama tingatinga wamenyoosha mikono, ni kama hafahamu kuwa ukiona uji wa mgonjwa unarudishwa toka hospitali ujue mgonjwa kaaga, nape njia ndefu lakini hafungi kuni, riziki ni kwa mafungu, bandu bandu gogo humalizika, kilichoila CCM kimekula taratibu sana na hakuna tena gogo wal kigogo wakuepusha chama kufa, ulikuwa wapi wakati fedha za UMMA zinaibiwa, ulikuwa wapi wakati wa EPA, RADA, Ndege ya Rais?

  Kwa upande mwingine wanazi wa mambo wameendelea kufikiria na kuona kuwa CCM karibu kabisa na kuwa tawi la CDM, kwani kama CDM ndo imekuwa ikiongoza serikali kwa remote, na kama serikali hiyo hiyo inaongoza CCM, ni dhahiri kwa hesabu za kawaida kwenye maamuzi ya CCM kuna mkono mkubwa wa CDM. Nini kinafanyika CCM inategemea zaidi CDM wanasema nini jukwaaani na bungeni; mfano utaona jinsi wabunge wa CCM walivyoaamka na kuamua kuikandia serikali yao eti bajeti ni cha mtoto, haya ni mawazo ya siku nyingi sana kwa CDM, sasa yanaingia ndani ya CCM kupitia njia mbalimbali ikiwemo bunge na serikali.

  Kwa hali ilivyo sasa kulegalega kwa CDM itakuwa sawa kabisa na kulegalega kwa nchi, Je ni ukweli CDM mnaongoza serikali kwa remote, ambayo pia inaongoza CCM na bado muda kidogo mtashika usukani wenyewe.
   
 2. m

  mamajack JF-Expert Member

  #2
  Jun 18, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 1,162
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  ni ukweli usionampinzani.hata nape analijua hilo.hebu muulize.
   
 3. M

  Mgelukila JF-Expert Member

  #3
  Jun 18, 2012
  Joined: May 27, 2012
  Messages: 224
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tusubiri wakatae ili tuje na mifano maana wabishi sana nitarudi.
   
 4. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #4
  Jun 18, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  serikali imeshindwa kujiendesha ndio maana wapinzani wameamua kuwasaidia
   
 5. mgashi

  mgashi JF-Expert Member

  #5
  Jun 18, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 304
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Atakae bisha ni kawaida yake kubisha kila kitu laki huo ndo ukweli wenyewe.
   
 6. makoye2009

  makoye2009 JF-Expert Member

  #6
  Jun 18, 2012
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,646
  Likes Received: 500
  Trophy Points: 280
  Huo ndiyo ukwell wa mambo.

  Kiwete analijua hilo,Mizengwe Pinda analijua hilo,Mukama analijua hilo na hata Nepi Naye analijua hilo.
  Kama wanabisha wamwulize BENARD MEMBE aliyeweka mambo hadharani baada ya Team ya CHADEMA kutinga jimboni kwake na yeye kwenda kuwalaki kwa kuwakaribisha nyumbani kwake na kula nao chakula!!!

  Viongozi wengine wa CCM kama kina WASSIRA, NEPI, MAGUFULI na wengineo watapiga makele yao ya kuilaani CHADEMA na matusi ya kila aina lakini ukweli unabaki palepale kama ulivyowekwa wazi na bwana MEMBE.

  M4C OYEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE! PEPOZZZZZZZZZZZZZZZZZZ, POWEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEER!!!
  SAAFI SANA CHADEMA. ENDELEENI KUWAFUNDISHA KAZI HAO MAFISADI WA CCM.
   
 7. F

  Froida JF-Expert Member

  #7
  Jun 18, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Ukweli kabisa nilicheka walipowahamisha wahanga wa mafuriko Tabata shuleni baada ya kuona godbless lema anaenda kufungua matawi huko,halafu eneo karibu la msitu wa kazimzumbwe wamerudishiwa wananchi baada ya kusikia Marando anaenda kufungua kesi kwa niaba yao ha ha hadi raha
   
 8. k

  kilawe Member

  #8
  Jun 18, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni kwel kabisa; kila mtu analiona hili, kama kuna mtu atapinga haya bac atakuwa hana macho wala maskio ili aweze kuona na kuskia!
   
 9. f

  fikirikwanza JF-Expert Member

  #9
  Jun 19, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 5,935
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Je CHADEMA Kuendesha nchi kwa remote ni afya ktk siasa za Tanzania??
   
Loading...