MAHANJU
JF-Expert Member
- Aug 26, 2014
- 5,244
- 7,970
Unaweza usinielewe lakini ukweli ndio huu! Unaweza usiyaone haya lakini utayaona hivi punde tu.
Chama hakina ziara mikoani, chama hakina muda wa kukagua uhai wake mikoani, chama ni kama hakina viongozi ngazi za chini.Imefikia mpaka mahali watu hawajui kama kuna makatibu na wenyeviti wa CCM mikoa wilaya na kata. Hii kazi ya kukitangaza Chama ni kama limekua jukumu za wabunge ambao wao wanalinda nafasi zao kwenye uchaguzi hapo 2020.sasa haijulikani kama CCM Kuna UWT, haijulikani kama CCM bado kuna jumuiya ya wazazi, Kidogo UVCCM bado inaonekana kwa mbali.
Watu wameridhika wakidhani kua chama kitabebwa na serikali hii ya awamu ya tano, laahasha! Tusubiri uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 ndipo tutaamini kua CCM imejizika rasmi.Serikali iko bize na Changamoto za kupigana na hali tete ya Uchumi na sio kutafuta wanachama wapya wa CCM, hiyo kazi ilifanywa zamani na komredi Kinana lakini sasa watu wameweka mikono kifuani tusubiri serikali itafute wanachama.
Kwaalalamiko juu ya hali halisi ya maisha ikiwa ni sambamba na mfumuko wa bei za vyakula nchini kwakweli mimi sitaki kusema zaidi. Ninauacha muda uzungumze zaidi, Maana hawa wanaohangaika waliamini kua CCM bado inayo nafasi ya kufanya mabadiliko lakini sasa mambo yamegeuka.
Mwananchi wa kijiji cha Machenje huko Tandahimba Mtwara utamwambia masuala ya Ndege huku akinywa maji kama kinywaji adimu utadhani ni soda atakuelewa? Utamweleza juu Masuala ya Reli ya standard gauge atakuelewa huku akipata uji wa mhogo asubuhi na jioni tu? Utamweleza juu ya Barbara ya Morroco iliyoko jijini Dar atakujibu nini? Labda kidogo Mtoto kutolipa ada ya shule hapo kidogo anaweza kukuelewa japo huyu mtoto anatakiwa awe na kalamu, aje chakula na aoge na kunywa maji safi.
Kwa hali niionayo huku kijijini jamani Mungu anazilinda jamii zetu tu hizi.