CCM inaanikwa Zanzibar -Wakuu wa Jeshi, polisi na vyombo vingine vya usalama kuweni nayo makini Itawazamisha

Shocker

JF-Expert Member
Sep 15, 2012
330
1,000
Kwa sasa sio siri hakuna mpango wowote wa CCM kwa upande wa Zanzibar usio julikana kuhusiana na mipango ya kuchezea daftari la wapiga kura.
Mitandanoni kumejaa ushahidi uliowazi na wa kuaminika kabisa kuwa waajiriwa wa vyombo husika hapo juu wanapangwa kutumiwa ili kuiletea ushindi CCM,mambo yote na mipango yote ipo uwanjani. Ndio nikasema CCM ipo uchi ,kiswahili sanifu kabisa.

Kuanza kwa kura kwa Zanzibar ni tarehe 27/10/2020 ,baada ya ufuatiliaji na uchunguzi uliojaa tahadhari kwanini imepangwa hivyo,imegundulika vyombo hivyo vimepangwa kupiga kura tarehe 27/10/2020 na hawataweka wino kidole gumba na halafu tena wafaajiriwa wa vyombo hivyo kupiga kura 28/10/2020 kwa maana hio watapiga kura mara mbili kuipaisha CCM kimagumashi.

Hayo yete kwa sasa yapo nje na hakuna Mzanzibari asiesikia na kulijua na bado linazungumzwa .

Suali ni Je Wakuu wa vyombo hivyo wanalielewa hilo kuwa wanataka kuingizwa kwenye mauzauza na hawa CCM waliopo Zanzibar na sio Zanzibar peke yao hawana ubavu wa kuamuru hivyo Vyombo, mambo haya yana baraka za kina Polepole na bashiru na yule kibaraka wao wao aliepo Zanzibar Mabodi,mipango yao imeshajulikana.

Maafande wana muda wa kufuatilia na kuwatia hatiani waliopanga njama hizo, kuvihusisha vyombo vyao na kutaka kufanya udanganyifu. sasa kama ushenzi huu unataka kufanywa yale majilabu ya Afande Siro yapo wapi ? taarifa zimezagaa mitandanoni hivi vyombo vinapakwa mivi na CCM na pia vitu hivyo ni ushahidi kikinuka kimataifa wataingia hatiani kiurahisi,kila mmoja atakuwa anajitetea hamtamuona Bashiru wala Polepole kuwatetea.

Na vizuri mjue balaa lililowakumba CCM Zanzibar kutokana na mgombea wao kutokubalika wacha kwa ujumla wa Zanzibar, ndani ya CCM Zanzibar ni mtihani mara nyingi kumeripotiwa sintofahamu ,hivyo ni vigumu nani yupo na nani,ndio ukaona wanapanga njama usiku asubuhi hata haijafika unakuta habari za kikao na njama zipo mtandaoni.

Msijaribu kuvitia na kuvihusisha vyombo vyenu katika Zanzibar katika kupanga matokea huko hakuna siri ndani ya CCM ,imekuwa sasa hadi picha za wanaopanga mbinu za kuiba na kubadilisha au kucheza na data za uchaguzi kutokea TISS zinawekwa mitandaoni,hio ni aibu na fedheha kubwa,usalama wa taifa hatakiwi hata kupiga au kupigwa picha.
 

vposterior

JF-Expert Member
Jul 19, 2018
762
1,000
Kibaya zaidi tume ya uchaguzi (ZEC) imetangaza wapiga kura ni 566,352 baada ya kutoa daftari imeonekana walioandikishwa ni 433, 337. Hii tayari ipo kwenye mitandao na vijana wanahoji hao laki moja na ushee wako wapi.
Inaonekana hawa ambao hawaonekani ndio wamekusudia kuwaambia majeshi wakazipige mbili mbili au tatu hadi zitimie lakini tayari njama ya imejuulikana.
ZEC jiandaeni tarehe 27 tunapiga kura sote halafu tutamalizia na 28 pamoja. UKHANITHI BAAAAAS.
 

Kibereko

Senior Member
Sep 26, 2018
181
500
Siku moja kabla ya tarehe ya kupiga kura watamwagwa wazee wa kazi kila kona ya Unguja. Kuwatisha Wananchi.
 

Shocker

JF-Expert Member
Sep 15, 2012
330
1,000
Huu uchaguzi sio wa Maalim ni wa Wazanzibari wote tena popote walipo maana Chama Cha Mazimwi (CCM) kimechomoka habari za chinichini wameanza kulana wenyewe kwa wenyewe.

Bila ya shaka yeyote WaZanzibari mara hii sio wa kisiwa cha Pemba bali makao makuu Unguja wataidhihirishia dunia kuwa wamechoka na hawapati pumzi.
 

dos.2020

JF-Expert Member
Feb 17, 2009
3,475
2,000
119649529_181144006939431_892889969102153479_n.png
 

kibwengomfupi

JF-Expert Member
Jul 21, 2016
685
1,000
Liwalo na liwe mwaka huu,alisikika kiongozi mmoja wa upinzani zanzibar

Sent from my SM-J200H using JamiiForums mobile app

Tuwekeni akiba ya chakula majumbani mwetu kabisa. Tunataka kuingia uwanjani kudai haki yetu ama kwa mananeo au kwa vitendo.
Haki haitolewi kama andazi kwenye kisahani cha chai. Lazima uipiganie. viongozi wa ACT kaeni kikao cha dharuara mtoe mwongozo wa next step itakuwa vipi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom