CCM ina wanachama zaidi ya milioni 15 lakini bado inachukua wapinzani na kuwapa ubunge, shida ni nini?

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,891
141,824
Hili swali nimemuuliza kada mkongwe mzee Mgaya lakini majibu aliyonipa yamenitatiza kidogo, amedai huenda CCM kuna Binadamu wengi lakini " watu " ni wachache. Kwa kunifafanulia amesema binadamu huzaliwa lakini mtu hutengenezwa.

Mdau wa siasa wewe unalionaje hili la wapinzani kuhamia CCM na moja kwa moja kupewa fursa ya kugombea nafasi za uongozi?

Maendeleo hayana vyama!
 
Hivi ni vita lazima tuteke majeshi ya adui na kuyaunganisha kwetu kuhusu utu na ubinadamu hilo ni tatizo la nchi sio CCM pekee nchi hii imejaa mijitu ya hovyo sana na hii ndiyo sababu ya kuwa na viongozi wa ajabu sana
 
SABABU KUBWA hata kama watu haiwaisemi ni:

~ Chuki, Visasi, Rushwa na Kukomoana.

- Yaani wanatoa Rushwa ya pesa na vyeo kwa kila anaewakosoa ili akae kimya au awashambulie wapinzani wao.

Kumbuka bila kuwa pesa, vyeo na nafasi yoyote hakuna atakayehamia ( ndio maana Marekani hakuna anayejikomba kwa Rais kwa sababu kila mtu anakula kwa jasho lake ).

[ Tangu tuingie mfumo wa vyama vingi CCM imepoteza kabisa mwelekeo ( inachokifanya ni kumtegemea Rais | Dola | ) au sometimes uwezo binafsi wa mtawala ].

Kila kinachofanywa sasa nchi hii na watawala, FOCUS yake ni KUDHIBITI WAKOSOAJI na KUWAKOMOA.

Ndio hata bungeni sasa wakosoaji ndio wanaojadiliwa.

Hata watawala wastaafu hawawezi kumkosoa aliyepo kwasababu, lengo la tawala zao inaonekana ni kubadilishana tu ZAMU ZA KULA.

Kwahiyo kama wakati wako wa kula wenzio hawakukupigia kelele na wewe unatakiwa ukae kimya.

Sasa hivi Tanzania imekuwa kama Burundi ( Hakuna cha kujivunia miaka zaidi 60 ya uhuru ).

A complete definition of a FAILED STATE.
 
Hili swali nimemuuliza kada mkongwe mzee Mgaya lakini majibu aliyonipa yamenitatiza kidogo, amedai huenda CCM kuna Binadamu wengi lakini " watu " ni wachache. Kwa kunifafanulia amesema binadamu huzaliwa lakini mtu hutengenezwa.

Mdau wa siasa wewe unalionaje hili la wapinzani kuhamia CCM na moja kwa moja kupewa fursa ya kugombea nafasi za uongozi?

Maendeleo hayana vyama!
Wewe jamaa ni CCM lakini nakupenda sana kwa jinsi ulivyo na reasons za maana. Uko tofauti sana tena sana na mpumbavu mmoja anayejiita Bia Yetu.
 
Watu wengine niwanachama hewa mfano Mimi ninkadi ya ccm toka 2010 pia naingiaga mpaka kwenye vikao vya ccm, lakini siwezi kuipigia ccm kura yangu hata sikumoja Mimi ccm hewa , kwaiyo kati ya wanachama mil 15 itakuwa wanachama hai niml 2 tu.
 
usidanganywe na namba (digit), kwenye msafara wa mamba na kenge wamo. Kundi linawanafki wengi ndio maana wenye akili wanatazama walio nje wawasaidie kazi zao :cool:
 
Fidel Castro aliwahi kuikosoa Sera ya Marekani na kuiita kuwa ni ya kipumbavu, kumpa uraia kila M - Cuba anayekanyaga ardhi ya Marekani...
 
Hili swali nimemuuliza kada mkongwe mzee Mgaya lakini majibu aliyonipa yamenitatiza kidogo, amedai huenda CCM kuna Binadamu wengi lakini " watu " ni wachache. Kwa kunifafanulia amesema binadamu huzaliwa lakini mtu hutengenezwa.

Mdau wa siasa wewe unalionaje hili la wapinzani kuhamia CCM na moja kwa moja kupewa fursa ya kugombea nafasi za uongozi?

Maendeleo hayana vyama!
Hili jambo linafikirisha sana. Labda wengi wa wanachama wao waliumbwa kwa ajili ya kuhudhuria mikutano, kushangilia, kufanya vurugu, kununua sare, na kuwapamba viongozi huku wao wenyewe wakiwa hawana sifa za uongozi!!
 
Hili jambo linafikirisha sana. Labda wengi wa wanachama wai waliumbwa kwa ajili ya kuhudhuria mikutano,kushangilia, kufanya vurugu, kununua sare, na kuwapamba viongozi huku wao wenyewe wakiwa hawana sifa za uongozi!!
Unataka kuniambia Tarime kwa mfano hakuna wanaccm wenye sifa za kugombea ubunge tangu aondoke Nyambari Nyangwine?
 
Back
Top Bottom