CCM ina wanachama Milioni 15, wakijiandikisha wao tu inatosha, tusilazimishane kujiandikisha

Mukulu wa Bakulu

JF-Expert Member
Aug 12, 2014
4,052
12,904
Polepole hua mara nyingi anasema ccm ina wanachama milioni 15 ambao wako hai.

Takwimu za NEC za mwaka 2015 waliojiandikisha walikua milioni 21 hivi na wakapiga kura watu milioni 15.

Wakijiandikisha wanaccm pekee wanafika 100% ya waliopiga kura 2015, ya nini kulazimisha wengine wajiandikishe na kutishia kufuta vijiji wakati ccm wenyewe wakijiandikisha wanatosha?

Ccm jiandikisheni, mpigiane kura wenyewe mpate ushindi wa 100%, ushindi wa kishindo. Msilazimishe wengine kujiandikisha.
 
2014 mlijianfikisha ila mlipigwa chini na wananchi..sioni sababu ya kwanini mpoteze muda safari hii.
 
Mhe. Mwenye Kitambi alisema Wilaya yake haitamtangaza mshindi iwapo atatoka chama kile. Hivyo wananchi wakaona hakuna umuhimu wa kujifuta kwani ukimchagua au usipomchagua lazima atashinda tu. Wanajiuliza je kuna haja ya kujifuta kweli?
 
Umewezaje kujua idadi ya wana CCM kabla hawajiandikisha?

Au unatumia data gani kubaini idadi ya wanaCCM?
 
Kwa sasa wakuu wa shule za sekondari wamepewa agizo la kuhakikisha wanafunzi wao wote hasa wale wa bweni, wanakwenda kujiandikisha. Hali ni tete! Kila mtu analinda tumbo lake lisije likatumbuliwa.
 
Hivi polepole yuko wapi?.simuoni akihamasisha watu wake ccm kujiandikisha na yeye ni katibu wa itikadi na uenezi
 
Back
Top Bottom