Return Of Undertaker
JF-Expert Member
- Jun 12, 2012
- 4,572
- 26,868
Kamati kuu ya chama tawala nchini Afrika Kusini, cha African National Congress, ANC imeamua kumuondoa rais Jacob Zuma kama kiongozi wa taifa hilo. Amepewa masaa 48 ya kujiuzulu. Taarifa hii ni kulingana na chanzo kutoka uongozi wa juu wa ANC, kilipozungumza na shirika la habari la Reuters, mapema hii leo. Hatua hii inafuatia kikao kilichodumu kwa masaa 13, kilichohusisha viongozi wakuu wa chama hicho.