CCM ina ‘Succession Plan?’ Vijana wameiangusha. Je, wazee watakuja na mapya?

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,271
47,269
Chama cha Mapinduzi CCM kimeamua kuendelea kuwatumia wastaafu baada ya vijana kiliowaamini kina Ally Hapi, Sabaya, Makonda, Polepole, Bashiru kuwaangusha kiutendaji, na wengine baadhi kukosa radhi na kuanza kuwabeza Wazee kwa matusi kina Musiba, Musukuma, “Nafurahi Wastaafu Kutukanwa”.- Lusinde.

Labda CCM kimeona kiwarudishe wastaafu kwa ajili ya uzoefu wao, lkn tujiulize hao wazee watakuja na mapya yapi ambayo hawakuyafanya wakati wa ujana wao.

Hali hii ipo hata serikalini tunaona watu walewale kina Nehemia Mchechu, Nape wanarudishwa nafasi zilezile walizoshindwa kuzihudumu utadhani hakuna wengine wenye uwezo.

Hii recycling ya watu wale wale Mwinyi & sons, Kikwete & Sons, Nauye & Sons, Kinana & co inaifanya Tanzania iwe kama nchi ya kifalme. Hali hii ya Nepotism hatukuiona kwenye utawala wa Nyerere.

Nepotism is the practice of favoritism based on kinship.
 
Wanasema Quinine ya enzi zile hazina utamu wa hizo za enzi mpya 🤔.Hivyo ni dawa kweli, kweli🤔
 
“Ukiona chama cha siasa viongozi wake walioomba kustaafu, wakastaafu halafu wakaombwa tena kurudi kuongoza ujue hicho chama kilishajifia. Chama kikishindwa kuandaa kizazi kipya wakati bado kipo kizazi kinachoendelea jua hicho chama kimeshakufa tayari”. - John Pambalu.
 
Back
Top Bottom