CCM ina Moral Authority ya Kuongoza TanZania!

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,811
Kwanza maana ya moral Authority ; is authority premised on principles, or fundamental truths, which are independent of written, or positive, laws!

Hivyo basi CCM ina moral authority ya kuendelea kuongoza TanZania na Mlm.Nyerere alikuwa sahihi kabisa na aliona mbali sana aliposema kwamba TanZania bila CCM imara nchi itayumba!
Ingawaje ni rahisi sana kukipinga, kukidharau au hata kukiombea kifo Chama cha Mapinduzi lkn kati ya hao wote wanaokiombea kifo CCM hawasemi wanataka kuweka nini badala yake, labda watatuambia chadema ndiyo ije badala ya CCM sasa tuiweke chadema kwenye radar kama vile tunavyoiweka CCM, tuichambue chadema nje ndani kama vile tunavyoifanyia CCM halafu mniambie inaizidi au hata kukaribia tu CCM kwa kiasi gani!

Ni kwa sababu ya mfumo wa kuongoza nchi wa CCM ndiyo ulioifanya nchi hii iwe bado intact kwa miaka zaidi ya Hamsini tangu Uhuru, siyo kazi rahisi kujaribu kumridhisha kila mtu lkn ile tu kwamba Dini mbili yaani Waislamu na Wakristo tunaishi pmj, tunashirikiana na tunachanganyikana hii haijaanguka ktk mtini kama tunda bali ni kazi iliyofanywa na waasisi wetu!

Chukulia kwa mfano Raisi Magufuli au hata Kikwete mwenyewe hawa ni watu ambao ni kizazi cha kwanza kwao hata kwenda Shule lkn wameweza kujiendeleza kwa kutumia mifumo mizuri ya haki na isiyo na upendeleo na ubaguzi wa kidini au eneo walilotoka mpaka kufikia ngazi ya kuwa Raisi wa nchi, Raisi Magufuli alianzia kuwa Mwalimu wa Sekondari leo hii ni Raisi wa nchi, nitajieni nchi tano hapa Afrika ambazo hili linawezekana!
Mfano mzuri ila dhana ya kujivua gamba, ni vyma vingapi Afrika hii vina uwezo wa kufanya CCM ilivyofanya? Yaani kuwaengua Matajiri waliokuwa na nguvu ya fedha ndani ya Chama chake kwa kumuondoa Kingpin wa ufisadi Lowasa?

CCM viongozi wake wanamuwakilisha karibia kila mtu hapa nchini kuanzia Wanawake, Dini zote, maeneo yote ya nchi, mpaka walemavu wamewakilishwa, vijana na wazee sasa niambie chama gani cha siasa kinaweza kuwakisha sura ya TZ nzima?
Tuchukulie chadema hauwezi hata kuona uwakilishi wa watu wa Dini ya Kiislamu, zaidi ya 3/4 ya Uongozi wa chadema ni watu ktk KLM na Arusha mjini ( na siyo Mkoa wa Arusha), hakuna muwakilishi wa Walemavu, wanawake ni wale ambao ni mahawala, wake au ndugu wa Viongozi wa chadema, tuje chama cha CUF hakina Uwakilishi wa watu wa Kikristo kwanza unaweza hata kukiita ni Chama cha Waislamu kama ingeruhusiwa kufanya hivyo, hivyo basi naweza kusema kabisa kwamba CCM ina moral authority ya kutawala TanZania na itaendelea kuwa hivyo kwa maana moral authority ni absolute truth na CCM kuongoza TanZania ni absolute truth!
 
Back
Top Bottom