CCM ina kazi kubwa sana ili kulikomboa Jimbo la Mbeya Mjini!

Usijali mkuu NEC yetu, Polisi wetu, Mkurugenzi wetu, Mkuu wa wilaya wetu, mkuu wa mkoa wetu, Majaji wetu na Mahakama zetu na Magereza pia yetu.

Hivyo hatuhitaji vikaratasi kuchukua jimbo.!
Hapo sasa,huyo sugu si tunamteka siku ya kurudisha form,uchaguzi mapema tu dr Tuloa anachukua jimbo
 
Wee mleta mada unadanganya umma

Hakuna jimbo lolote nchini ambalo CCM ikilitaka itashindwa

Si umeona leo ngoma ikichezwa? Waliotuma wawakilishi ni NECKI na Msijiajiri wa vyama
Huku Polyccm, Neckii, misjiajiri nani atashindwa!

Hakuna chaguzi ni upotevu wa pesa. Leo wanacheza ngoma kituo cha Polisi utashinda kwa njia gani!
 
Ninapenda sana watu wanaodadavua masuala ya kisiasa kama ulivyofanya.

Tatizo linalokumba kwa sasa hili jukwaa la siasa hapa Jamiiforums ni kuwa na wachangiaji wa sentesi moja yenye kutafuta LIKES za wajinga!

Kwa sasa watu wenye uelewa mpana wanasoma heading na thread tu halafu wanaenda kwenye thread nyingine kwa sababu ni kupoteza muda kusoma michango ya wachangiaji wa thread kutokana na michango ya kitoto au kijinga.

Usichoke kutoa elimu kwa faida yetu tunaopenda kusoma michango yenye kufikirisha zaidi.
Ni ujinga pia kusoma maelezo marefu ambayo hayaakisi uhalisia wa siasa na chaguzi za sasa. Achilia mbali mategemeo na mwenendo wa chaguzi zijazo. Are you serious kutuaminisha humu kuwa CCM ikilitaka Jimbo la Mbeya hata wiki ijayo itashindwa kulipata???.Wadanganyeni wajinga....
 
CCM bado inakabiliwa na kazi ngumu sana ya kulikomboa Jimbo la Mbeya Mjini ambalo linaongozwa na Mbunge kutoka CHADEMA, Joseph Osmund Mbilinyi maarufu Sugu pamoja na kupata ushindi wa Udiwani katika kata 3 kwenye uchaguzi mdogo uliomalizika jana katika Jimbo la Mbeya Mjini.

Ukichunguza utagundua kuwa matokeo ya kura za Madiwani yanaonyesha ni jinsi gani CCM bado ina safari ndefu sana katika kurudisha Jimbo la Mbeya Mjini. Matokeo ya Kata tatu ni angalizo linalojitoshereza kwa kiwango kikubwa kuchambua kwa undani mwonekano wa siasa katika Mkoa wa Mbeya hasa Jimbo la Mbeya Mjini.

Katika Kata 3, wagombea wa CCM walipata jumla ya kura 7,851 wakati wagombea wa CHADEMA walipata kura 6,115. Tofauti ya kura ni 1.736.

Kata ya Maanga, Newton Mwatujobe (CCM) alipata kura 1897 na kumshinda, Steven Mwashilindi (CHADEMA) ambaye alipata kura 1703.

Katika Kata ya Iwambi, Humphrey Ngalawa (CCM) alipata kura 2107 huku Elisha Mwandele (CHADEMA) akipata kura 1906.

Aidha katika Kata ya Nsalaga, Kasusura, David Ngogo (CCM) alipata kura 3847 wakati Reward Mshanga (CHADEMA) akipata kura 2506.

Matokeo haya yanaweza kuwafurahisha wanaCCM lakini ukichunguza kwa undani zaidi kwa kutumia sayansi ya siasa utagundua kuwa safari ya CCM kulikomboa Jimbo la Mbeya Mjini bado ni ndefu sana hasa ukichukulia kuwa ni mkoa ambao unaongoza kwa kuwa na vijana wengi wajasiliamali wasio na mitaji mikubwa.

Sijui ni nani atasimama kama mgombea wa CCM katika Uchaguzi Mkuu 2020, lakini kama CCM itaendekeza siasa za ‘’kubebana’’ katika mchakato wa kumpata mgombea wa kupambana na Mbunge Mbilinyi, sitashangaa kuona Jimbo likibaki mkononi mwa Mbunge wa sasa.

Nimemuona Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, Dr. Tulia Ackson Mwansasu akipita huku na kule Jijini Mbeya lakini ukichunguza zaidi utagundua anatafuta fursa ya kuchaguliwa na wanaCCM kuwa mgombea Ubunge. Ninaweza kuwa siko sahihi lakini historia inaonyesha kuwa ukiona mwanasiasa anafanya jambo fulani kwa jamii lazima atakuwa anatafuta maslahi zaidi ya kisiasa!

Baada ya kumsikia Dr. Tulia kwenye majukwaa ya kisiasa akijieleza, Sina uhakika kama huyu anaweza kupambana na kushinda ubunge katika Jimbo la Mbeya Mjini. Ninaweza pia kuwa siko sahihi kama ambavyo Waziri Mkuu wa Uingereza, Harold Wilson aliwahi kusema, ‘’a week is a long time in politics!’’

Kwa matokeo haya ya jana, CCM wanatakiwa wazichange vizuri karata zao za kisiasa kama kweli wanataka kulikomboa Jimbo la Mbeya Mjini.
Sayansi ya siasa ni muhimu uifahamu,sio kwa kuisikia tu bali kupitia darasani(kuelimishwa) au uzoefu(experience). Ilibidi uwasifu CCM kujikusanyia kura hizo kwa sababu kuu 4 zifuatazo;
1.Tofauti ya kura ni kubwa sana kwa kwa kiwango chake kwa sababu ushindi ni ushindi tu na huesabika kuanzia tofauti ya kura moja sembuse zaidi ya kura 1000(KWELI HUJUI POLITICAL GAMES, MFANO KUSHAWISHI WAPIGA KURA )
2.Izingatiwe jimbo hilo limekuwa chini ya upinzani zaidi ya miaka mitano,hivyo ingekuwa sahihi CCM isiambulie kura,lakini wamezoa kura nyingi na ushindi katika kata zote(UPO SIRIAZI KWELI WEWE??)
3.Kwanini useme CCM itakuwa na kazi ngumu uchaguzi ujao kutokana na tofauti ya kura kata tatu?Je, uchaguzi ujao tofauti si inaweza kuwa constant au ikazidi,hivyo CCM kujinyakulia jimbo kiulani?Ni mbinu gani za ushawishi mtatumia ili kushinda pasipo CCM kutumia mbinu zozote za ushawishi na kubweteka?(HIVI UMEWAZA KWA KUSHIRIKISHA SEHEMU ZAKO KUU ZA UBONGO SAWA SAWA PASIPO NA KISHAWISHI CHA KILEVI CHOCHOTE KICHWANI MWAKO?)
4.Hivi unajua wapiga kura hushawishiwa ndani ya muda mfupi kabla ya uchaguzi na kubadili mwelekeo wa wapiga kura kwa kuona kinachofanywa/kutatua kero za wananchi mfano sasa hivi Serikali Chini ya CCM?(HIVI HUONI MPIGA KURA HUSHAWISHIWA KWA HOJA ZENYE MASHIKO KWA KUTATULIWA MATATIZO YAO?HATA HAO VIJANA UNAOWASEMA NAO NI WAPIGA KURA WA KITANZANIA,WANA MAAMUZI YA KUCHUJA IPI PUMBA AU MCHELE,ISITOSHE VIJANA NAO WANAMAHITAJI KAMA RAIA WENGINE WA TAIFA HILI PAMOJA NA KUJUA UKWELI,ACHA KUOTA MCHANA WA SAA 7).
Tuachane na ngonjera za kukariri kuwa hawa wanashinda kwa sababu wana polisi,magereza,wakuu wa wilaya,wakurugenzi,mahakama,jeshi n.k.Yaani vyombo vyote hivi vinyamaze kimya ili uchaguzi uharibike na amani ikosekane halafu mwisho wa siku sisi hawa hawa ndio tutaanza kuilamu serikali na vyombo vyake vyote kuwa vilinyamaza bila kutekeleza wajibu wake ipasavyo.HAPANA NA WALA SIO SAHIHI KABISA SERIKALI KUNYAMAZIA UTOTO,ACHA MASIHAHARA MLETA UZI,KAJIPANGE TENA ILI USHAWISHI WATU WENYE AKILI ZAO.
Sijapata matokeo ya UKONGA NA MONDULI,HEBU TUHABARISHE MKUU WANGU KUTOKA JIJINI MBEYA UTAFAKARI NA KUFUTA KAULI ZAKO!!
 
...Na kosa kubwa sana ni kumfunga sugu bila kujua wanamuongezea Kiki kwa wananchi...
Licha ya kukubaliana na uchambuzi wako lakini hapo kwa Sugu sidhani kama ni sahihi. Kama alikutwa na makosa basi ni haki yake kupata kifungo bila kujali maslahi ya kisiasa.
 
Yaani pamoja na kushinda kata hizo tatu bado huoni ni kiashiria cha uwezekano Wa CDM kupoteza!? Kwa nn usitumie fact hzo hzo za udiwani Ku justify kwamba CDM wanaweza kupoteza?
Huwezi kutumia hiyo kama "fact" kwa sababu CCM wanapanda nguvu zaidi za kupora kwenye chaguzi ndogo, kwenye uchaguzi mkuu fursa ya uporaji huwa inashuka kwa sababu maeneo ya kunyang'anya yanakuwa mengi!
 
Huwezi kutumia hiyo kama "fact" kwa sababu CCM wanapanda nguvu zaidi za kupora kwenye chaguzi ndogo, kwenye uchaguzi mkuu fursa ya uporaji huwa inashuka kwa sababu maeneo ya kunyang'anya yanakuwa mengi!
haya ndgu ila umenchekesha ulivyosema maeneo ya kupora yanakuwa mengi
 
Hizo kura bado za wizi.ukiondoa za wizi hapo ni shida tu.ccm watapata kama kura 4000 tu.
 
Mkuu;
Ninakushukuru sana kwa kuzichambua vizuri siasa za Mbeya.

Nadhani mchakato wa kumpata mgombea wa CCM katika jimbo hilo ndio utakaochagiza ushindi au kushindwa.

Wala usipoteze muda wako kuandika post ndefu za kusema eti uchambuzi; sasa hv ccm haishindi kwa box la kura, bali mkuu wa nchi anatoa amri mgombea wa ccm atangazwe.
 
Ukitaka kujua CCM iliamua kwa dhati kabisa kukomboa majimbo na kata zilizoenda upinzani, angalia matokeo ya chaguzi za marudio.
Ni kweli ndio maana wametumia polisi, Tume ya uchaguzi kuhakikisha wanashinda
 
Ninapenda sana watu wanaodadavua masuala ya kisiasa kama ulivyofanya.

Tatizo linalokumba kwa sasa hili jukwaa la siasa hapa Jamiiforums ni kuwa na wachangiaji wa sentesi moja yenye kutafuta LIKES za wajinga!

Kwa sasa watu wenye uelewa mpana wanasoma heading na thread tu halafu wanaenda kwenye thread nyingine kwa sababu ni kupoteza muda kusoma michango ya wachangiaji wa thread kutokana na michango ya kitoto au kijinga.

Usichoke kutoa elimu kwa faida yetu tunaopenda kusoma michango yenye kufikirisha zaidi.
Kuna ujinga zaidi ya ule wa kuitisha uchaguzi alafu mnaiba kura?!
 
Back
Top Bottom