CCM ina kansa ya rushwa na ufisadi

tajirijasiri

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
2,863
3,851
Majipu yooote unayoyaona na kuyasikia yakitumbuliwa na mengine kushindikana kutumbuliwa kama LUGUMI, ESCROW, MELI CHAKAVU, KIWIRA N.K, Ni mazao yaliyolimwa, kupandwa, kupaliliwa na kukomazwa na CCM miaka yooote ya utawala wake.

Kutumbua "Majipu" haitoshi, kwani "Majipu" ni matokeo ya athari zilizo ndani ya mwili. Ndani ya mwili (figurative language) ndiko iliko kansa inayoibua hayo "Majipu" nje ya mwili.

CCM ina kansa ya Rushwa na Ufisadi.
 
Kweli kabisa, ili mtu upone inabidi ukubali kuwa unaumwa na ukubali kupata matibabu lakini wakija hapa utawaona jinsi kamasi na mapovu yanavyowatoka utafikiri nyati
 
Kama umeshawahi kufanya counseling utagundua kuwa iwapo mshauriwa haoni tatizo na kukiri kuwa ni tatizo basi kupona Kwame ni aghalabu. Ndivyo ilivyo kwa Hawa Jamaa zetu. Hawajawahi kuona hivyo ni kazi Bure kushughlika na tatizo lao. Maka wakiri kwamba kweli hilo ni tatizo watuombe msamaha hapo utaanza kuona uponyaji wa kweli. Sasa hivi kazi kubwa itafanyika kwa nguvu sana lakini sioni mwendelezo wake wasipoona tatizo na kuamua kulishughulikia kimfumo. JPM Sasa anapiga kelele peke yake lakini kama Chama wangeliona na wakaona kuwa ndiyo tatizo kwa hiyo wakalishughulikia kama tatizo lao
 
Kweli kabisa, ili mtu upone inabidi ukubali kuwa unaumwa na ukubali kupata matibabu lakini wakija hapa utawaona jinsi kamasi na mapovu yanavyowatoka utafikiri nyati
Nadhani wameshindwa kuipinga hoja. Nimewasubiri toka asubuhi lakini naishia kuwaona waki view na kukaa kimya Tu. Dawa itakuwa imewaingia.
 
Haya ni maigizo anayotufanyia Magufuli, majipu ya maana yanayopiga hela chafu anayazunguka na kuyaacha. Akamate wa ESCROW, IPTL, NSSF walionunua heka moja zaidi ya sh billion, Lugumi, UDA kama anaweza.

Lugumi wameishaanza danadana kuipotezea, CCM na ufisadi ni uji na mgonjwa hawaachani, bahati nzuri kwao watanzania ukiwapa fulana za umoja ni ushindi umewapata.
 
Kuna wakati mwingine inakuwa ngumu kumuelewa huyu mtumbua Majipu. Yeye alikuwa ni sehemu ya baraza la mawaziri lililopita na yeye alikuwa mbunge sasa alikuwa wapi kuyapinga haya?

Imekuwaje leo hii anajifanya kuyasahau madudu aliyoshiriki kama mwanachama na mbunge wa CCM?

Au sasa amehama chama?
 
Kuna mwingine inakuwa ngumu kumuelewa huyu mtumbua Majipu. Yeye alikuwa ni sehemu ya baraza la mawaziri lililopita na yeye alikuwa mbunge sasa alikuwa wapi kuyapinga haya?

Imekuwaje leo hii anajifanya kuyasahau madudu aliyoshiriki kama mwanachama na mbunge wa CCM?

Au sasa amehama chama?
Mwanaccm mzuri lazima awe mwongo na mnafiki ndiyo maana wanaweza kukaa na mafisadi na wakateteana
 
Back
Top Bottom