CCM ina hazina kubwa ya viongozi, Rais Samia njia nyeupe hadi 2030

Countrywide

JF-Expert Member
Mar 2, 2015
18,159
27,194
Bila shaka wote tunaweza kukubali kuwa CCM ni chama kikongwe duniani na kilichokaa muda mrefu madarakani.

Haya yote hayafanyiki kwa bahati mbaya, Bali ni kutokana na hadhina kubwa ya viongozi ambayo imekuwa nayo.

Wengi wanasema watanzania hawajielewi ndio maana hadi sasa CCM inaendelea kutawala, huu si ukweli. Ukweli ni kuwa watanzania ni waelewa sana na wanajua wanachokitaka.

Ieleweke kuwa CCM kuendelea kutawala sio kwamba watafanya vizuri kila siku, la hasha bali watafaanya makosa na watayarekebisha haraka sana.

Natolea mfano hapa:

Ni nani alijua CCM watakuja na Raisi Kikwete?
Rais Kikwete kafanya mengi mazuri na hili nina amini hakuna atayepinga humu labda awe katumwa. Nchi ilifanya vizuri kila angle, hakika CCM waliweza kutuletea kiongozi Bora kabisa. Nasisitiza mapungufu hayakosekani.

Ni nani alijua CCM watakuja na Magufuli?
Hapa pia nadhani hakuna atayepinga labda awe katumwa, Magufuli kafanya makubwa sana nchini na imefanya vizuri kila angle. Nasisitiza mapungufu hayakosekani. Mungu amlaze mahala pema peponi.

Ni nani alijua CCM watakuja na Mama Samia?
Nadhani hapa kila mtu anashuhudia ambacho mama Samia anafanya, ukweli ni kuwa mama anaipeleka Tanzania kuwa nchi ya asali na maziwa.

Mama Samia anarekebisha makosa ya JK, anarekebisha ya Magufuli na kuendelea mbele zaidi, muda utasema. Kama utampinga huyu mama hakika wewe nichawi.

Nasisitiza Mama Samia nae ni binadamu kuna mapungufu yanaweza kujitokeza katika utawala wake ila sio sababu ya kuanza kumbeza hivyo ninashauri watu wote wamuunge mkono na hivyo sio sababu ya kuwa na uchaguzi wa ushindani 2025.

CCM ina viongozi wazuri na hili linathibitika kila anapoingia rais mpya.

Hakika kwa hili CCM inahitaji pongezi kubwa sana, kwa maana vyama vingi vya siasa duniani vimeshindwa kuwa na consistency ambayo CCM wanayo.

Screenshot_20210329-111904_1.jpg
 
Bila shaka wote tunaweza kukubali kuwa CCM ni chama kikongwe duniani na kilichokaa muda mrefu madarakani, na kuweza kuzalisha umaskini mkubwa kwa wananchi wake.
 
Baada ya Magufuli, kama tutaendelea hivi, inaonekana kichaa yeyote anaweza kuongoza Tanzania.

Hatuhitaji hazina.

Watu watamuogopa tu kwa sababu rais.

Na kama CCM imetupa Magufuli, inaweza kutupa maradhi yoyote, muda wowote.
 
MAGUFULI hakuwa Kiongozi Sahihi kabisa kupata Kutokea Baba wa Taifa hakuwalea Watanzania kuja KUUANA, KUONEANA, KUFUNGANA
 
Bila shaka wote tunaweza kukubali kuwa CCM ni chama kikongwe duniani na kilichokaa muda mrefu madarakani, na kuweza kuzalisha umaskini mkubwa kwa wananchi wake.
Umasikini wako unahusiana vipi na CCM? Unataka wakuwekee pesa mfukoni?
 
Kama ni Hazina ya madeni nitakubali, tunaambiwa sasa deni la taifa ni Trillion 71 na ushee. Kazi ipo.
 
Mama akituvusha salama Kwa nini 2025 tusiende na Bashiru ?
ni mzalendo na mnyenyekevu 🇹🇿🔰📗✅
 
Back
Top Bottom