CCM ina Hali Mbaya Sana Kata ya Njoro Wilayani Kiteto

Lancanshire

JF-Expert Member
Sep 20, 2014
14,019
2,000
Wakuu kwa taarifa alizonipa jamaa yangu ambae kwa sasa yupo Njoro huko Kiteto akinunua mazao ananiambia ccm wamelazimika kukimbia baada ya wananchi wa Kata ya Njoro kuwafukuza na mapanga pamoja na silaha nyingine za jadi walipojaribu kufanya kampeni. Jamaa ananiambia vyombo vya ulinzi na usalama wilayani Kiteto vinahaha kunusuru hiyo hali Ni tête Sana. Nitawaletea taarifa kamili baada ya muda mfupi.
 

Lancanshire

JF-Expert Member
Sep 20, 2014
14,019
2,000
Kwa taarifa zaidi Ni kwamba ccm wameshindwa kufanya kampeni katika eneo la kata ya Njoro na kulazimika kuondoka kutokana na wananchi kukataa kabisa kuongea na watu wa Chama hicho tawala hapa nchini. Wananchi wengi wamekuwa wakitoa kauli za kwamba ccm Ni wezi ,mafisadi na hawafai kuwaongoza. Nafasi zote za uongozi zinatarajiwa kuchukuliwa na vyama vya upinzani.
 

Lancanshire

JF-Expert Member
Sep 20, 2014
14,019
2,000
Mimi nipo hapa njoro lakini hali ni shwari kabisa!
Mkuu kama uko hapo Njoro utakuwa umejionea hali halisi ya wananchi wanavyowakimbiza watu wa ccm. Hiki chama kimechokwa na watanzania kila upande wa nchi hii wananchi wanalia na ccm.
 

needeseela

JF-Expert Member
Feb 13, 2014
1,897
2,000
Nilipita pale Jana majira ya saa 11 jioni nikielekea Arusha kupitia Kiteto na Simanjiro. Watu wa Njoro
, Matui, baadhi wa Dosidosi, Kiteto majini, Langatomon, na baadhi ya watu wanaozunguka hifadhi ya Mutangos na Emboliei hawajawahi kuipenda CCM kwa yao wanayofahamu wenyewe. CCM Kiteto daima ni 65% na upinzani ni 35% rejea matokeo ya uchaguzi zote kuu na uchaguzi mdogo wa 2008.

Ninavyo andika Uzi huu nipo hapa Simanjiro na CCM hapa wamepita kwa zaidi ya 90%. Hii pia imeonesha Imani kubwa waliyonayo watu Wa Simanjiro dhidi ya Mbunge wao kipenzi Chao Christopher Olonyonkie Ole Sendeka ambaye ambaye siku zote amesimama kupinga ufisadi Wa ESCROW. Hili pia liwe fundisho kwa wabunge wengine wa CCM kuwa ukisimama kutetea maslahi ya wananchi nao watasimama na wewe pale unapotaka msaada wao wakisiasa. Hongera Sana Sendeka.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom