CCM Ina-Capitalize msiba wa Kanumba for Political gain?

Wanabodi,

Naangalia msiba wa Kanumba live kupitia Clouds TV, nimenote viongozi wa CCM wakipewa maximum recognition.

Tangu mwanzo MC akitangaza miongoni mwa wageni mashuhuri akawataja mawaziri na wabunge akamalizia kwa Mukama na Nape, Mhe. Mbilinyi ambae yupo hapo has never been mentioned na siamini kuwa MC hajamuona Sugu mahali pale!.

Baadae katika kukusanya maoni ya watu mbali mbali, Clouds radio na TV waka zero in Mkama na Nape tuu, yaani hawakuonekana wengine wowote wa kutoa maoni yao!.

Nilikuwa najiuliza jinsi msiba huu ulivyofanywa wa kitaifa na serikali kutoa ushirikiano mkubwa hivi ikiwemo logistic support kuwezesha Kanumba kuzikwa maziko ya kitaifa nikijua ni kuuenzi mchango wa Kanumba tuu kumbe nia ni kuwashika wapenzi wa Kanumba!.

Politics is very interesting game, japo wengine wanaita is a very dirty game, for me, politics is a game of exploration of opportunities!. For every event hata kama ni msiba, wao kwao they see an opportunity!.

Pasco.
Leo ni imetimia miaka 10, toka kifo cha nyota huyu wa Bongo Movies, Steven Kanumba, na mpaka Leo, sio tuu pengo lake halijazibika, bali hajapatikana star mwingine yoyote wa kuvaa viatu vyake vikamfiti.

RIP Steven Kanumba, tutakukumbuka milele!.
Paskali
 
Back
Top Bottom