CCM Ina-Capitalize msiba wa Kanumba for Political gain?

Of course, JK na CCM wana haki ya ku-sympathize na familiana mourn msiba wa Kanumba kama rafiki yao wa karibu. Lakini hili la kuufanyamsiba wa Kitaifa ni joke of the century!!!

 
Pasco, nimeliona hili suala na nimelisema jana. CCM wanatumia msiba wa kanumba kupata umaarufu, lakini kumbe marehemu alikuwa mwanachama wa Chadema.
 
Ukiwa politician, unakuwa kama mcheza kamali/draft.
ready to strike is any opportunity appears....
This is why you can not separate politics with social life...

Naona hili suala Mh.Sugu limemshinda kuseparate, maana nimemuona kapiga Sare ya Chama(Combat) msibani
 
Mkuu pasco umeenda mbali sana,
ni desturi ya watz kuhudhuria misiba na haina uhusiano wa kisiasa kabisa, sidhani kama ni sahihi kila jambo kuliingizia na siasa, hatutafika! kuna masuala ya kijamii na mengine ya kitaalamu!
Acheni hizo
Kama kweli ni hivyo mbona Mzee Kipara alipofariki hakuna aliyejitokeza? Au kwa kuwa Kanumba ni kijana ndio maana wanajipendekeza kwani wanajua vijana hawakipendi chama chao kwa hiyo wanajisogeza karibu ili wapate cha kusema. Hatudanganyiki nyie!!!!!!!!
 
Pasco,

..mwanzo mlikuwa mnamuona JK ni muungwana kuhudhuria hii misiba, lakini sasa ndiyo mnagundua kwamba ni siasa za CCM tu.

..lakini siyo misiba tu inayotumika kisiasa, wameanza kuwatumia WALEMAVU na WATOTO kama mitaji ya kisiasa.

NB:

..msiba wa Regia nao waliuvamia, wakati akiwa hai walikuwa wakimshambulia yeye na CDM kuwa wanataka nchi isitawalike.
 
Siku hawa viongozi wakiacha kabisa kwenda kwenye misiba wapo watakaolalama pia.

Some things just come with the territory. You are damned if you do and damned if you don't.
 
Mbona Mzee wa "bomu linalosubiri kulipuka" sijamwona tena
huu ndo msiba wa mabomu (vijana) haswaa! Au kaogopa yasimlipukie kama AR-Meru
 
Vyovyote vile watu watakavyosema lakini kilichofanywa na CCM pamoja na serikali yake ni kutafuta masilahi ya kisiasa kupitia msiba huu!, period.
 
wanabodi,

naangalia msiba wa kanumba live kupitia clouds tv, nimenote viongozi wa ccm wakipewa maximum recognition.

Tangu mwanzo mc akitangaza miongoni mwa wageni mashuhuri akawataja mawaziri na wabunge akamalizia kwa mukama na nape, mhe. Mbilinyi ambae yupo hapo has never been mentioned na siamini kuwa mc hajamuona sugu mahali pale!.

Baadae katika kukusanya maoni ya watu mbali mbali, clouds radio na tv waka zero in mkama na nape tuu, yaani hawakuonekana wengine wowote wa kutoa maoni yao!.

Nilikuwa najiuliza jinsi msiba huu ulivyofanywa wa kitaifa na serikali kutoa ushirikiano mkubwa hivi ikiwemo logistic support kuwezesha kanumba kuzikwa maziko ya kitaifa nikijua ni kuuenzi mchango wa kanumba tuu kumbe nia ni kuwashika wapenzi wa kanumba!.

Politics is very interesting game, japo wengine wanaita is a very dirty game, for me, politics is a game of exploration of opportunities!. For every event hata kama ni msiba, wao kwao they see an opportunity!.

Pasco.

ndugu yangu pasco kuna watu wanaweza kukuponda kwamba unaingiza mambo hayana ukweli na kwamba wewe labda hujali misiba lakini ukweli unabaki pale pale kwamba viongozi wa sisiem wametumia msiba huu kisiasa na clouds tv inatumika kisia. Mtagundua kwamba clouds tv ndiyo ilofanya coverage kubwa ya msiba huu kw akuuonyesha live mathani tbc however tbc hawakuinfluence sana which means sisiem waliogopa kwenda moja kwa moja kuripoti tukio hili kwa tbc wakaamua tbc ionekana kama imeshirikiana na clouds (shame on them) wapembuzi tumegundua janza yaoooo hatudanganyikiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii!
 
Mkuu Pasco,
Haya mambo ni magumu kidogo kueleweka! Binafsi, sizani hata kidogo kama CCM walikusudia kuugeuza msiba huu for political reason!! Frankly speaking, kifo cha Kanumba kwangu nilikichukulia ni kifo cha staa wa kibongo kama ilivyokuwa kwa marehemu Complex, Mtoto wa Dandu, Remmy Ongara, n.k….kumbe maskini nilikuwa najidanganya! Ikumbukwe kwamba, mara baada ya taarifa za kifo cha Kinumba kuzagaa, watu wakajazana maskani kwake! Humu JF posts zikawa zinamiminika kama mvua…zote zinahusu Kanumba! Hapo ndipo nikaja kushituka kwamba kumbe kifo cha Kanumba si kama kifo cha mastaa wengine tuliowazoea! Wananchi, bila kushawishiwa wala kuhamasishwa…..wakajikuta tu wanaupa msiba huu kipaumbele cha mambo yao! Siku nne a Pasaka niliamua kujifungia ndani bila kwenda kokote….ajabu leo nilipofika ofisini, nikakuta stori za Kanumba!

Kifo cha Kanumba kikawa kumbe ni public issue…..katika hali kama hii kiongozi hana choice; ni lazima atajumuika na wapiga kura tu!!!!

Tukirudi kwenye suala la Clouds kutoa air time kwa viongozi wa CCM, hilo ni suala la Clouds wenyewe! Ni wao wenye kuamua ni nani wamuhoji na nani wasimuhoji…! Siamini hata kidogo kwamba leo hii mwananchi ambae alikuwa haipendi CCM ataanza kuipenda kwavile tu timu ya CCM ilikuwapo pale!! Siamini kwamba viongozi wa CCM waliokuwapo msibani huu ndio msiba wao wa kwanza…!

All in all, maoni hasi ya wana-JF (simaanishi kwamba yako ni hasi) kuhusu msiba wa Kanumba na jinsi unavyopaishwa na serikali ya JK naona ni kama ile simulizi ya heri mimi sijasema!! Tunasahau kwamba, jinsi tunavyooengeza threads za Kanumba ambazo zinapata michango ya kutosha; kumbe nasi tunapaisha!
 
clouds, ccm, hovyo tu,

Na wamefanikiwa kuwafanya wakaazi wa dar kuwa mazuzu kweli hasa!

Tukio hili limedhihirisha jinsi wabongo wanavyoendeshwa kwa hisia na mihemko, mbaya zaidi hali hii inagusa mpaka taasisi nyeti ya nchi "RAIS"

"Tumepotea"
 
Kama kweli ni hivyo mbona Mzee Kipara alipofariki hakuna aliyejitokeza? Au kwa kuwa Kanumba ni kijana ndio maana wanajipendekeza kwani wanajua vijana hawakipendi chama chao kwa hiyo wanajisogeza karibu ili wapate cha kusema. Hatudanganyiki nyie!!!!!!!!

Nilikuwepo kwenye mazishi ya Mzee Kipara...Samuel Sitta nakumbuka ndie aliongoza msafara!
 
Hii ni kweli taifa letu ni la hovyo na linatawaliwa na watu wa hovyo. Hata hivyo tusishangae msukumo na hadhi aliyopewa Kanumba. Ni kwa vile ni msanii kama wao na mazinzi mwenzao so to speak. Nilishangaa kuona msiba wake unapewa uzito kuliko hata wa marehemu makamu wa rais Omari Juma. This is saaaad. Tunaelekea wapi iwapo watu wanakwepa majukumu muhumi ni kujichimbia kwenye mambo ya hovyo? Hakika tumekwisha na tuililie Tanzania inayogeuzwa kuwa Tanzia.
 
Binafsi najiuliza; Who is KANUMBA???? hata Bunge lifanye hivyo.

Naona mwisho tutataka na Bendera ipepeee nusu mlingoti, kisha tarehe aliyofariki iwe ni siku ya mapumziko kama zilivyo "Karume Day", na "Nyerere Day"

SHAME ON YOUR BRAIN!!!!!!!!!!!!!!



MIZAMBWA
NABII MTARAJIWA!!!

Yaani mkuu Mizambwa we acha tu, hii nchi ni ya majuha sio kidogo......!
 
Leo Pasco umetoa point sana...

Kwanza tujiulize hii haki ya kufanya huu msiba ni wa Clouds radio na Tv imepatikanaje, wameivamia tu kama kawaida yao??
Pili tujiulize kwa nini wamuweke kichaa kuwa MC, kwa jinsi Kibonde anavyopenda kuropoka simtofautishi na kichaa. Ila kikubwa kinachopelekea yote haya kutokea ni ile desturi ya watanzania kupenda kujipendekeza na ku-side na wenye power. Hawataki kabisa kukubaliana na ukweli kuwa Kanumba aliplan siku moja kugombea ubunge kupitia CDM, wanatamani hata kumpa kadi ya chama chao akiwa mfu ili kulitafutia ubani li chama lao la KUVUNDA

Mkuu,
Hauwatendei haki kuwalaumu Clouds kuupa coverage msiba huu!! Pamoja na mambo mengine, kituo cha redio na tv kingependa kurusha kile ambacho kitasikilizwa/kuangaliwa/kufuatiliwa na watazamaji/wasikilizaji wengi zaidi!! Clouds, walishasoma hisia za wananchi kwamba wengi wangependa kufuatilia suala la Kanumba…nao wakawapa wananchi kile walichokitaka!! Kama upo Bongo, si ajabu hata wewe (kama ilivyo kwa Pasco) ulifuatilia kupitia huko!!!! Lengo la kuonwa/kusilizwa na wengi hapo lilitimia!! Na wala usishangae, endapo pangefanyika utafiti, si ajabu ingegundulika Clouds (TV+Radio) ndivyo vyombo vya habari vilivyofuatiliwa zaidi tangu kifo cha Kanumba!
Kwa upande mwingine, ni kuwaonea kuwashutumu kwamba Clouds wamefanya hayo kwa maslahi ya CCM! Tangu kutokea kwa kifo cha Kanumba, Clouds walianza kufanya coverage ya kifo kile mapema sana…..tuwe wakweli, nobody expected kwamba ule msiba ungebamba kiasi kile! Hivyo, Clouds walianza kufanya coverage kabla haijajulikana kwamba msiba ungevuta sana hisia za watu! Waliongea saa ngapi hapo na CCM?!
Jana usiku nilikuwa nasikiliza Magic FM…kwenye kipindi cha Kwetu Flavor, 99% ya nyimbo zilizokuwa zinapigwa na maombolezo ya Kanumba!! Mi mwenyewe nilishangaa! Je, hawa nao walitumwa na CCM?
BBC Kiswahili Service! Hawa, tangu siku ya kwanza ya kutokea kifo cha Kanumba…wamekuwa wakiripoti taarifa hizo, kwenye habari zao za asubuhi na jioni!! Je, hawa nao wamenunuliwa na CCM?!
Nazani tunapaswa kukubali kwamba kifo cha Kanumba kimewateka wengi! Umati aliokusanya haundani hata chembe na aliyofanya!! Haya mambo yanatokea, kuna wengine wanakuja na karama zao hapa duniani! Si wewe, wala mimi tunaweza kuyabadilisha hayo!! Na hata kama viongozi wasingeenda, bado raia wangeshona tu!! Hapo, wasiohishiwa maneno; au wenye kukosoa kila jambo pia wangepata la kusema! Ungesikia, “Kanumba ameiletea sifa sana nchi hii kwa kuitangaza kila sehemu, lakini leo hii anakufa hakuna kiongozi hata mmoja aliyejitokeza!”
Jamani, tupunguze siasa…..!!!
 
Back
Top Bottom