CCM imeua/kuuza kiwanda na karatasi cha Mufindi na mitamho ikauzwa Kenya kinazalisha malighafi tunanunua karatasi Kenya

Wabunge wa Tanzania hawako serious mtu anasimama anasema Saloon ni kiwanda..yaani ni bora unambie Mama Lishe ndio kiwanda maana wanaprocess mchele uwe wali ila sio saloon.kumbe viwanda tulivyoahidiwa na saloon zipo
Mbunge kama yule unashindwa kuelewa kama ni kichaa au mwendawazimu.
 
View attachment 741971 View attachment 741970 View attachment 741969

Kiwanda cha karatasi kilichopo wilaya ya Mufindi mkoa wa Iringa kiitwacho Mufindi paper mills LTD (MPM) zamani Southern Paper Mills (SPM) kilichokuwa kinamilikiwa na serikali ya jamhuri ya Tanzania 100%, chini ya shirika la Maendeleo la Taifa (NDC), Kwasasa kinamilikiwa na kampuni ya RAI GROUP LIMITED ya nchini Kenya.

Kiwanda hiki cha mgololo kilianzishwa rasmi na kuzinduliwa na Rais wa kwanza wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, hayati Mwl. JULIUS. K. NYERERE mwaka 1985 kikiwa na thamani ya Bilioni TANO za Kitanzania kwa wakati huo, jukumu lake kuu ilikuwa kuzalisha karatasi kwa kutumia malighafi za ndani toka katika msitu wa Saohili Mafinga, lengo ilikuwa ni kufanya biashara na kuongeza wigo wa ajira kwa watanzania.

Na kukazia hilo, Mwakimu Nyerere aliamua kujenge shule ya ufundi Ifunda Tech maalumu kwaajili ya kuzalisha wataalamu mbalimbali wa kuendesha kiwanda hicho, sawa kabisa na Arusha Tech iliyokuwa shule kwaajili ya kuwanda cha Arusha tools.

Tarehe 24/01/1997 kwa waraka wa serikali (Government Notes) namba 33, Serikali ili-specify Kiwanda na kukiweka chini ya tume ya kurekebisha mashirika ya umma (PSRC) iliyopewa jukumu la kusimamia shughuri za Kiwanda zikiwemo huduma kwa wafanyakazi wanaotunza kiwanda kwa kufanya uzalishaji mdogo mdogo (mill warming) na pia kutafuta mwekezaji (kukinadi hatimaye kukiuza kiwanda).

Tarehe 13/02/2004 kiwanda kilikabidhiwa rasmi kwa Rai Group ya Kenya kwa maelezo ya kuwa wao ndio wanunuzi wa Kiwanda hicho adimu barani Afrika, hakuna taarifa rasmi za bei ya ununuzi wa kiwanda hicho lakini inatajwa kuwa kiliuzwa kwa Shilingi bilioni MOJA za Kitanzania.

Leo hii kiwanda hakizalishi karatasi tena, mitambo imeng'olewa na kuhamishiwa kenya, ambapo pale Mgololo zinazalishwa malighafi tu za karatasi, kisha husafirishwa Kenya, nakutengenezwa karatasi kisha hurudishwa nchini kutuuzia Karatasi hizo,

Serikali ya CCM itueleze watanzania, kwanini kiwanda hiki chenye malighafi zote hapo Mufindi lakini hakizalishi karatasi hapo na badala yake soko la ndani la karatasi linategemea Muhindi aagize toka India na Kenya?. Achana na Karatasi, lakini msitu wa Saohil Mufindi ndio msitu wa uzalishaji wa nguzo za Umeme barani Afrika, lakini Tanesco miaka yote wamekuwa wananunua nguzo toka Afrika kusini (japo mwaka jana kulikukuwa na agizo la kirais waache mchezo huo) ambazo nguzo hizo zinatoka hapahapa Mufindi kwenda Afrika Kusini kusindikwa kisha zinauzwa Tz na kurejeshwa hapa kwa bei ya mara tatu au nne.

Nani mchawi wa taifa hili kamw sio sera mbovu za serikali ya chama cha mapinduzi? Taifa linapoteza mabilioni ya pesa kwa ujinga unaoitwa kujiuzuru ubunge ama udiwani kwa kumuunga mkono Rais, kibaya zaidi ujinga huu unasherekewa na wakuu wa maamuzi ya nchi, pesa zile za uchaguzi tungeamua kuwekeza 5b tu pale Mgololo tungezalisha ajira ngapi na kuongeza godi ya taifa?

Upo wapi ujasusi wa Kiuchumi ikiwa Kenya anatupiga hata kwa mambo madogo kama haya?

Na Yericko Nyerere
sio mufindi paper mills tu, tanwat, na viwanda vya chai vya makampuni ya mufindi venye kutoa ajira kubwa mikoa ya njombe na irina navyo vimeuzwa kwa kampuni za wakenya serikali inaangalia tu. Huu uchumi wa viwanda ambavyo sisi ni spectators ni uchumi gani?
 
sio mufindi paper mills tu, tanwat, na viwanda vya chai vya makampuni ya mufindi venye kutoa ajira kubwa mikoa ya njombe na irina navyo vimeuzwa kwa kampuni za wakenya serikali inaangalia tu. Huu uchumi wa viwanda ambavyo sisi ni spectators ni uchumi gani?
Na
sio mufindi paper mills tu, tanwat, na viwanda vya chai vya makampuni ya mufindi venye kutoa ajira kubwa mikoa ya njombe na irina navyo vimeuzwa kwa kampuni za wakenya serikali inaangalia tu. Huu uchumi wa viwanda ambavyo sisi ni spectators ni uchumi gani?
Naona unachanganya mambo, Tanwat na viwanda vya chai "Stone valley" havijawahi kuwa vya serikali. Hivi vilimilikiwa na kampuni za Kingereza kwa hiyo kama ni kuuza hisa wamefanya hivyo kibiashara. Na kuonyesha shukurani Princess Anna alitujengea kwa msaada barabara ya Makambako to Songea
 
Katika utoaji wa taarifa, makosa kidogo yanaweza punguza kuaminiwa kwa kusudio. Dhana kuwa CCM iliuza viwanda ni dhana potofu, sababu viwanda vingi viliuzwa na Serikali kwa shinikizo la IMF wakati huo. Hata kujiuzuru Mwalimu iliaminika ni kukwepa utekelezaji wa mashrti usiangukie mkononi mwake. Tujifunze historia, wakubwa hawakutaka maendeleo ya viwanda kwa nchi masikini kwani ilikuwa ni tishio LA bidhaa zao. Na kuna ukweli ktk kutekeleza masharti haya, kwa kujua au kutojua kuna makosa yalifanyika.
Kwa hiyo Nyerere asingetoka bila kuwekewa masharti yaliomkera?
 
Nadhani watu hawaijui CCM vizuri, CCM ni zaidi ya uijuavyo, ni zaidi ya unavyoifikiri, ina NGUVU kuliko unavyoifikiri

kuiondoa CCM ni safari kama ya WAISRAEL, inahitaji kujivika moyo wa UJASIRI na USHUJAA,

itafika mahali kilio cha watanzania juu ya CCM kitafika kwa MUNGU ( ni lazima) hapo ndipo CCM itaondoka na itasahaulika kabisa wengi watajaribu kuirudisha lakini hawatafanikiwa.

kwa sasa hivi sisi tuendelee kulia tu
 
10 Reactions
Reply
Back
Top Bottom