Uchaguzi 2020 CCM imetekeleza ilani yake kwa 31% tu, mambo mengi ni nje ya ilani. Je, Rais Magufuli alitumwa na nani?

Jelavic

Senior Member
Dec 28, 2016
176
500
Leo katika uzidunzi wa ilani ya ACT-Wazalendo nimemsikia Zitto akitaja mambo zaidi ya kumi ambayo CCM waliahidi kwenye ilani yao na hawakutekeleza hata kidogo, na sio tu kutekeleza bali hata kuanza japo kwa hatua za awali hawakufanya.

Nimekua najiuliza huku kusifusifu kulikovuka mipaka kunatokana na nini?

Je, Magufuli alikuwa anatoa wapi anayoyatekeleza, katumwa na nani kwa maslahi ya nani ikiwa chama kinacho wakilisha wananchi kimeisha toa mahitaji ya wananchi kwenye ilani?

Nimekuwa najiuliza: je, hao CCM wanauhakika gani tena kama Magufuli atasimamia ilani anayotaka kuanza kuinadi sasa hivi ikiwa ndani ya miaka mitano alifanya mambo mengi bila kufata ilani ya chama chake.

Hivi CCM ya Mafuguli mnahitaji ilani au ndio hakuna namna inabidi tu mchapishe ilan sababu ni chama cha siasa ila mnajua haitafuatwa?
 

sblandes

JF-Expert Member
Apr 25, 2010
5,949
2,000
Maguli hafuati ilani, ilani anayo kichwani.
Elimu Bure Haikuwemo
Kufufua ATC na kununua ndege haikuwepo.
Kuhamia Dodoma haikuwepo
Kujenga Ikulu Dodoma yenye eka 8000 badala ya eka 45 haikuwepo
Bwawa la Nyerere halikuwepo
Standard gauge reli ya kati haikuwepo
Kubomoa nyumba za Kimara bila fidia halikuwemo.
Kufufua Reli ya Dar Tanga Moshi Arusha haikuwepo .
Kujenga Daraja la Busisi haikuwepo.
Kujenga ukuta wa Merelani kuzuia utoroshaji wa Tanzanite haikuwepo.
Kufufua shirika la uvuvi TAFICO Haikuwemo.
Kudhibiti Wafanyakazi hewa na vyeti fake alikuwemo

Na mengine mengi.Safari hii natabiri haya yasio kwenye manifesto ya uchaguzi wa mwaka huu
Atajenga Daraja la kuunganisha Bagamoyo na Zanzibar.
Atanunua Manowari kibao za kikosi cha wanamaji
Atajenga Reli kutokea Mtwara kwenda Mbamba bay
Atajenga kiwanda cha kufua chuma huko Liganga.
Atajenga Airport kubwa Tanga
Atajenga LNG processing plant (ya gesi asilia )mkoa wa Lindi au Mtwara
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom