Uchaguzi 2020 CCM imeonesha demokrasia kuhesabu kura kwa uwazi, tume ya uchaguzi ifanye hivyo

Ulimbo

JF-Expert Member
Aug 14, 2009
3,767
4,035
TUME YA UCHAGUZI IFANYE HIVYO KWENYE CHAGUZI ZA URAIS, WABUGE NA MADIWANI. Ili kuepuka usumbufu na malalamiko ya kuibwa kwa kura.

Ingekuwa vizuri kuwepo na sheria kuwa kura zote zihesabiwe kwa uwazi kwenye vituo vya kupigia kura na matokeo ya kila kituo yatangazwe pale pale kwenye kituo husika.

Kama kweli serikali ya CCM pamoja na CCM yenyewe wakikubali hili, basi watu watazidi kuiamini serikali pamoja na CCM yenyewe. Vinginevyo itakuwa CCM wametupiga change la macho tu
 
kuhesabu kura mia sio sawa kuhesabu kura milioni. Wacha wahesabu kikawaida wamalize haraka watoe jibu tu.
 
Si mkuu alisema wanafanya mambo kwa uwazi bila kificho, na akatoa wito kwa vyama vingine vifanye hivyo?
uwazi si kwenye kupiga kura.... ndiyo maana kwenye uchaguzi mkuu mtu hutengewa chamber yake peke yake ya faragha!
 
kuhesabu kura mia sio sawa kuhesabu kura milioni. Wacha wahesabu kikawaida wamalize haraka watoe jibu tu.

Ni kweli si kazi rahisi, lakini kama kwa dakika chache waliweza kuhesabu na kutoa matokeo ya kura zaidi ya 1000, sitegemei kuwa itakuwa vigumu kuhesabu kura za kila kituo kwani wapiga kura hawatazidi 1000 kwa kila kituo. Wahesabu kura kwa uwazi kwa kila kituo na kuyatangaza papo kwa papo, then hayo ya jumla wakayajumlishe huko.
 
Mwaka huu mwendo ni mmoja tu, Kura zinapigwa kituoni, wananchi wanazilinda kituoni, zinahesabiwa mbele ya wananchi kituoni na matakeo yanatolewa hapo hapo kituoni. Kuanzia ya udiwani, ubunge na uraisi. Watu wanaondoka kituoni wakijua kabisa nani ameshinda kwenye ngazi ipi kwenye eneo lao.

Na matokeo yakiibwa wananchi waingie mtaani kudai matokeo yao halisi. Full stop
 
Ni kweli si kazi rahisi, lakini kama kwa dakika chache waliweza kuhesabu na kutoa matokeo ya kura zaidi ya 1000, sitegemei kuwa itakuwa vigumu kuhesabu kura za kila kituo kwani wapiga kura hawatazidi 1000 kwa kila kituo. Wahesabu kura kwa uwazi kwa kila kituo na kuyatangaza papo kwa papo, then hayo ya jumla wakayajumlishe huko.
Zile za kikaoni kwao hazikuzidi 200 kama sikosei....si tunazungumzia hizi za juzi apa kumchagua rais wa Zanzibar?

Hapo kituoni si kunakuwa na mawakala kutoka kila chama wakihesabu kura? wakimaliza wanatia saini halafu zinapelekwa makao makuu ama utaratibu kwenu ukoje? Mana huku kisiwani uliopita ulikuwa umewekwa wazi, ila baada ya kuona kuwa ngoma imewaelemea na mambo kuwa wazi wakaamua kujecharize matokeo.
 
Wajumbe wa CCM huku Bara walishapangwa kabla hata hawajatoka mikoani kuwa awamu hii Zanzibar ni Hussen Mwinyi tu.

Pale kilikuwa kiini macho tu.
 
Kwani huwa zinahesabiwa wapi. Mdogo wangu umeshawai piga kura kweli au awamu hii ndyo itakuwa mara yako ya kwanza?
 
Back
Top Bottom