CCM imemuaibisha Lijualikali baada ya kujivua heshima aliyopewa na CHADEMA

Tabutupu

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
13,107
18,322
Anaandika Rodrick Chamafwa

Nimeona Lijulikali akidhalilishwa CCM. Kura 5 za ubunge na kura 2 za udiwani ni udhalilishaji mkubwa kwa mtu aliyekuwa Mbunge. Lakini huyu anayedhalilishwa hivi ni mtu aliyeheshimishwa sana na CHADEMA. Nakumbuka mwaka 2013 alipokuwa anafanya kazi pale St.Francis Ifakara hakuwa na kitu.

Alikua anaishi kwenye chumba kimoja hichohicho ni chumba, ni jiko, ni stoo, ni sebule. Chumba chenye kitanda cha futi tatu godoro la futi tatu na sabufa isiyo na speaker. Ukweli alikua kijana ambaye alikuwa hana hata uwezo wa kumiliki chumba chake mwenyewe.

Chadema ikampa heshima ya kugombea udiwani kwenye uchaguzi mdogo kata ya Ifakara ambayo kwasasa imegawanya na kuwa kata tano 5 za halmashauri ya mji wa Ifakara baada ya kufariki diwani wa kata hiyo na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero Ramadhani Kiombile.

Si kwamba Lijualikali alikuwa mgombea mzuri sana kuliko wengine. Kulikua na watia nia wengine wazuri kuliko yeye, wenye elimu kuliko yeye, wenye hoja kuliko yeye. Lakini chama kilimpiyisha kugombea.

Pale St.Francis alikua Librarian, kazi yake ikiwa kupanga vitabu na kuvifuta vumbi. Akilipwa laki moja na nusu kwa mwezi. You can imagine aina ya maisha aliyokua nayo kwa kipato hicho. Hakuwa na kitu. Aliwahi kupigwa makofi pale Asante Bar baada ya kunywa na kushindwa kulipa.

Alipopitishwa kugombea hakuwa hata na pesa za kampeni. Viongozi kutoka mkoani walipoenda kumfanyia kampeni alishindwa hata kuwalipia guest house. Ikabidi awaombe baadhi yao wakakae nae kwenye getho lake. Akaenda mmoja, wengine wakajilipia guest kwa siku zote za kampeni.

Katikati ya kampeni akasema kuwa anataka kujitoaa kwa sababu hali ya kampeni ilikua ngumu sana. Freeman Mbowe alipoelezwa hali halisi ya akamtumia milioni tano. Ni pesa ambayo hajawahi kuishika maisha yake yote. Akachachawa, hakujua aifanyie nini, akina Kumbulu wakamsaidia kuipangia bajeti.

Kampeni zikaenda vizuri na viongozi kutoka makao makuu ya chama wakaenda kumuombea kura. Lakini ikafika mahali akaonesha kukata tamaa. Akasema anataka kujitoa. Tukaambiwa amehongwa milioni 15 na mgombea wa CCM Benjamen Masepo ili ajitoe. Tukakaa kikao na kumwambia akifanya huo ujinga wa kujitoa tunammaliza. Tukaanza kumlinda ili asijitoe. Kwenye kikao cha tathmini tukakubaliana kuhakikisha anakuja kukaa tunapokaa hadi mwisho wa kampeni.

Akagombea na kushinda kwa kupata kura 4323 huku Benjamen Masepo wa CCM akipata kura 3723 na Tunu Msakile wa CUF akipata kura 110.

Huu ndio ukikua mwanzo wa Lijualikali kuibuka kisiasa. Akawa diwani na kuanza kujijenga vizuri Ifakara. Wananchi wakamuona ni mwenzao na alipogombea Ubunge wakampa ushindi. Baada ya ubunge ndio akapata uwezo wa kujenga, kununua gari na mambo mengine.

Lakini Chama kilichompa heshima hiyo alikitukana na kukikashifu. Akahamia CCM na na kusema ina demokrasia. Sasa ameona matunda ya demokrasia ya CCM. Lijualikali ameweka rekodi ya kuwa mbunge wa kwanza duniani kupata kura 5 akitetea kiti chake, na kupata kura 2 kwenye udiwani. CCM imemuaibisha baada ya kujivua heshima aliyopewa na Chadema.
FB_IMG_1596413000210.jpeg
 
Mwanadamu siku zote ni mwepesi kusahau
Alafu huwezi ukajiunga ccm Leo na lro hii hii
Unajifanya unakijua Chama vizuri, wakati Kuna watu mule wamo Miaka kibao... Na wao wanataka
Vyeo
Hapo kilichobaki aombee apewe nafasi/cheo cha Kuteuliwa na Rais

Ova
 
Siwaungi mkono chadema lakini huyu Lijuakali alipitiliza sana hadi akasababisha chama kilichompeleka bungeni kuhojiwa na takukuru kwa uzushi wake tu. Ile ilimsababishia laana kubwa, laana sasa inamwanadama na hata akija kupewa udc udas au kinginecho anaweza kuishia pabaya tena. Akawaombe radhi aliowakashfu kwanza mambo yake yatanyoka.
 
Sioni kama amedharirishwa .hivi kwan ni watu wangapi mashuhurii washawahi kuhama vyama vyao tangu tuanze mfumo wa vyama vyingi? Kupanga ni kuchagua na hyo ndo mana halisi ya demokarasia mm nadhani ww ndo ulikua una lengo la kumdharirisha kwa kuweka mambo ya ndani ambayo hayana tija kwa sisi kuyajua
 
Back
Top Bottom