CCM imekufa, anakosekana wa kutangaza imekufa

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,298
12,600
Awamu ya tano ilimalizia kuiua CCM iliyokuwa tayari imepigwa jembe la mgongoni na Edward Lowassa alipohamia Chadema.

CCM ya kweli haiwezi kuwa na viongozi aina ya Mh. Polepole na Mh. Bashiru kama watendaji wakuu na kuwafungia nje wenye CCM yao. CCM halisi haiwezi kuwadhalilisha watu kama Kinana, Yusufu Makamba, Nape na wengine kutokana na michango yao kwenye siasa za CCM.

Awamu ya Mh. Magufuli R.I.P haikuamini nguvu ya CCM bali jina lake tu. Walihitaji jina la CCM lakini sio nguvu ya CCM kwenye siasa zao.

Kuondoka kwa Rais Magufuli CCM pia inayo kazi ya kufanya ya kuirudisha CCM kwa wenyewe. Ndiyo maana hata mafanikio ya JPM yanakutana na changamoto kutoka ndani na nje ya CCM baada ya yeye kuondoka.

Bahati yao kubwa ni kumpata Rais Samia ambae sio mwanacha wa kundi hili na kundi lile la CCM Bars, vinginevyo tungeshuhudia makubwa kwwnye vikao vyao.

Imekufa anakosekana wa kusema imekufa.
 
Magufuli alishatangulia kuitangaza kuwa imekufa, maana kwenye kampeni zake 2015 alikuwa anasema"CHAGUA MAGUFULI,SIYO CCM"mpaka hayo maneno yakawa "Sugu" yakamlazimu MKAPA kuja kumrekevisha wazi wazi kwa kumwambia, kusema serikali yangu, serikali ya Magufuli si sawa, maana umepewa dhamana na CCM.

Kingunge alishasema kuwa CCM inatoa Moshi wa oil chafu, imechoka.
 
Nani amfunge "PAKA KENGELE SHINGONI"?

CCM ilikufa mara baada ya Magufuli kuanza "UDIKTERA UCHWARA NA KULEWA MADARAKA" kwake.

Alipoanza urais katika awamu yake ya kwanza, nakumbuka alivyoamka asubuhi siku ya kwanza na kwenda kufanya usafi nje ya ikulu magogoni kwa kuzoa taka taka kwenye dampo, ilikua mwanzo mzuri sana kwake. Raia waliitikia wito kwa nguvu zote na kumuunga mkono kwa kufanya nae usafi, walipata imani nae sana.

Baraza La Mawaziri aliloanza nalo lilikua tishio hata kwa tunaoichukia CCM, kina Nape Nnauye/January Makamba na kadhalika, kulikua na stability na chemistry fulani nzuri sana serikalini. Ila alipowageuka CCM wenzake kisa cha kulazimisha "KUMKINGIA KIFUA DAUDI ALBETI BASHITE (Paul Makonda)" katika mambo ya jinai aliokua akifanya kama;

1) Kuvamia ofisi za Clouds na mitutu ya bunduki.

2) Kutapeli wafanyabuashara na kuwapa kesi za madawa ya kulevya.

3) Kuwachafua wafanyabiashara kwenye vyombo vya habari.

4) Kujiita kwamba yeye ndio kila kitu na kuwatukana viongozi wa usalama mbele ya kadamnasi.

na mambo mengine mengi ambayo hakupaswa kutetewa, ndio moshi ukaanza kufuka lumumba vizuri sana. Makundi yakaanza kidogo kidogo.

Ila alipokuja kulewa "MADARAKA YA KULEVYA" na kuanza ubaguzi/matusi/kejeli/kupoteza na kuua watu/ufisadi/kubaka demokrasia/kurekodi maongezi ya faragha kwa wana CCM wenzake na raia kwa ujumla, akajiona mungu mtu, ndio ikawa pata-shika taifa zima, haikuishia hapo akaendelea zaidi kwa kuwaacha vijana wake aliowateua kwenye nafasi za DC (Kina Ole Saabaya, Ally Hapi n.k) kuanza kuwaruhusu kuonea/kutukana/kubambikiza kesi/kuteka raia na wafanyabiashara hovyo, na ndio "CCM IKAFA KIFO CHA MENDE".

Hapo hatukuhitaji tena mtu kutangaza CCM imekufa, tulijua moja kwa moja msiba tayari, muda tu ndio ukawa bado mambo kujiweka wazi zaidi.
 
CCM haijafa, haitakufa na itaendelea kuongoza nchi hii kwa sababu wapinzani wote ni wanaharakati na mbumbumbu. Mtakesha mitandaoni lakini upinzani wa nchi hii ni utopolo tu.
Hata hujui siasa wewe, wapinzani nchini sio chadema, cuf, ACT wala UDP bali ni wananchi wenyewe, kama upinzani ungekuwa ni chadema uchaguzi was 2020 ungekuwa free and fair maana vyama vyote vilizuiwa kufanya siasa kwa miaka 5 kabla ya upinzani.

Mijadala ya wabunge kwenye bunge LA chama kimoja inaonyesha kuwa CCM haipo bali kuna maslahi ya MTU binafsi, kabila, wilaya, mkoa na kanda ya mbunge. Hata wabunge wenyewe wengi wao ni matunda ya Tume "asante Magufuli" na sio wanaCCM wenyewe.
 
Hakuna aliyeiba kura mlipigwa kihalali kama mtakavyopigwa 2025. Huo ndio ukweli mchungu.
 
Awamu ya tano ilimalizia kuiua CCM iliyokuwa tayari imepigwa jembe la mgongoni na Edward Lowassa alipohamia Chadema.

CCM ya kweli haiwezi kuwa na viongozi aina ya Mh. Polepole na Mh. Bashiru kama watendaji wakuu na kuwafungia nje wenye CCM yao. CCM halisi haiwezi kuwadhalilisha watu kama Kinana, Yusufu Makamba, Nape na wengine kutokana na michango yao kwenye siasa za CCM.

Awamu ya Mh. Magufuli R.I.P haikuamini nguvu ya CCM bali jina lake tu. Walihitaji jina la CCM lakini sio nguvu ya CCM kwenye siasa zao.

Kuondoka kwa Rais Magufuli CCM pia inayo kazi ya kufanya ya kuirudisha CCM kwa wenyewe. Ndiyo maana hata mafanikio ya JPM yanakutana na changamoto kutoka ndani na nje ya CCM baada ya yeye kuondoka.

Bahati yao kubwa ni kumpata Rais Samia ambae sio mwanacha wa kundi hili na kundi lile la CCM Bars, vinginevyo tungeshuhudia makubwa kwwnye vikao vyao.

Imekufa anakosekana wa kusema imekufa.

Nadhan bado wewe mtoto sana

na inashangaza kama umegundua leo

CCM imekufa kitambo sana, tangu 1990s

na vyama vingine havijawahi kukua, vilizaliwa na kunyauka

ndio maana bado unaona maiti ya CCM ipo tu

Trust me, mpaka unaingia kwenye jeneza utaiacha CCM madarakani, mpaka vitukuu vyako

unajua kwa nini?? kwa sababu akili yako iko kwenye maiti...kama Lissu anavyomuwaza JPM akilala na akiamka, hatatoka kwenye kifungo hicho, na hatawaza nje ya hapo
 
Siku ya uchaguzi mkuu wa 2020 niliongea na ndugu yangu yuko kijiji kimoja ktk moja ya mikoa ya ktkt ya nchi yetu, nikamuuliza kama ameenda kupiga kura akaniambia ameenda, nikamuuliza vipi huko mwitikio wa watu akaniambia watu wameenda ila amekutana na watu wasiojua kusoma na kuandika sijui ilikuwaje lkn akaombwa awasaidie baadhi kupiga kura sasa alipokuwa anawauliza wanamtaka nani jibu lao lilikuwa "tunamtaka yule yule wa siku zote" kutoka kwenye hicho chama unachosema kimekufa.
 
Awamu ya tano ilimalizia kuiua CCM iliyokuwa tayari imepigwa jembe la mgongoni na Edward Lowassa alipohamia Chadema.

CCM ya kweli haiwezi kuwa na viongozi aina ya Mh. Polepole na Mh. Bashiru kama watendaji wakuu na kuwafungia nje wenye CCM yao. CCM halisi haiwezi kuwadhalilisha watu kama Kinana, Yusufu Makamba, Nape na wengine kutokana na michango yao kwenye siasa za CCM.

Awamu ya Mh. Magufuli R.I.P haikuamini nguvu ya CCM bali jina lake tu. Walihitaji jina la CCM lakini sio nguvu ya CCM kwenye siasa zao.

Kuondoka kwa Rais Magufuli CCM pia inayo kazi ya kufanya ya kuirudisha CCM kwa wenyewe. Ndiyo maana hata mafanikio ya JPM yanakutana na changamoto kutoka ndani na nje ya CCM baada ya yeye kuondoka.

Bahati yao kubwa ni kumpata Rais Samia ambae sio mwanacha wa kundi hili na kundi lile la CCM Bars, vinginevyo tungeshuhudia makubwa kwwnye vikao vyao.

Imekufa anakosekana wa kusema imekufa.

Kukata tamaa Ni dhambi mbaya sana. Lakini kujifariji kila siku bila Ukweli na jitihada Ni ubwege na uzandiki sana. Mkuu kama hiyo CCM yenu ingekuwa imekufa unadhani Kwanini unaandika uzi mrefu hivyo.
 
Hata hujui siasa wewe, wapinzani nchini sio chadema, cuf, ACT wala UDP bali ni wananchi wenyewe, kama upinzani ungekuwa ni chadema uchaguzi was 2020 ungekuwa free and fair maana vyama vyote vilizuiwa kufanya siasa kwa miaka 5 kabla ya upinzani.

Mijadala ya wabunge kwenye bunge LA chama kimoja inaonyesha kuwa CCM haipo bali kuna maslahi ya MTU binafsi, kabila, wilaya, mkoa na kanda ya mbunge. Hata wabunge wenyewe wengi wao ni matunda ya Tume "asante Magufuli" na sio wanaCCM wenyewe.

Kwa lugha za kijinga Hivi ndo unatetea mada. Hivi unadhani hapa Ni Jukwaa la kutangaza misiba. Uza sera zako Acha kujifariji kizembe
 
Awamu ya tano ilimalizia kuiua CCM iliyokuwa tayari imepigwa jembe la mgongoni na Edward Lowassa alipohamia Chadema.

CCM ya kweli haiwezi kuwa na viongozi aina ya Mh. Polepole na Mh. Bashiru kama watendaji wakuu na kuwafungia nje wenye CCM yao. CCM halisi haiwezi kuwadhalilisha watu kama Kinana, Yusufu Makamba, Nape na wengine kutokana na michango yao kwenye siasa za CCM.

Awamu ya Mh. Magufuli R.I.P haikuamini nguvu ya CCM bali jina lake tu. Walihitaji jina la CCM lakini sio nguvu ya CCM kwenye siasa zao.

Kuondoka kwa Rais Magufuli CCM pia inayo kazi ya kufanya ya kuirudisha CCM kwa wenyewe. Ndiyo maana hata mafanikio ya JPM yanakutana na changamoto kutoka ndani na nje ya CCM baada ya yeye kuondoka.

Bahati yao kubwa ni kumpata Rais Samia ambae sio mwanacha wa kundi hili na kundi lile la CCM Bars, vinginevyo tungeshuhudia makubwa kwwnye vikao vyao.

Imekufa anakosekana wa kusema imekufa.
Mkuu ule usemi usemao "CCM INA WENYEWE" unajua maana yake? Mama hujui subiri 2025 Mungu akitiweka
 
Siku tukija kuyaona matokeo halisi ya uchaguzi wa 2020 ndio tutajua hiki chama alikiua Magufuli.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom