CCM imekosa mtu mwenye maadili?

Mpaka Kieleweke

JF-Expert Member
Feb 27, 2007
4,132
1,563
Nimepatwa na mshtuko mkubwa sana pale niliposoma leo kuwa eti Andrew Chenge amechaguliwa na kamati kuu ya CCM kuwa mjumbe wa kamati ya maadili.

Nimejiuliza swali hili ,hivi kuwa mjumbe wa kamati ya maadili maan yake si ni mtu wa kuhakikisha kuwa viongozi wenzake wanafuata maadili?

Ama kama wameamua kuufanya ufisadi sehemu ya chama chao basi Chenge anafaa kuwa mjumbe kwani kama hayo ndio maadili kwao nani awezaye kupinga chenge kuwa mjumbe humo?

Huyu Chenge nampinga kwa sababu kati ya watu waliouza taifa hili huyu ni wa kwanza akishirikiana na wakina Mkapa kuuza kila kilichomo ,na huyu ni fisadi mkubwa sana sasa kama anapewa kuwa mtu wa maadili hapo tumekwisha ....
 
Rwabugiri

JF-Expert Member
Jul 10, 2007
2,775
203

Mpaka kieleweke, Yaani hapo ujue ni jinsi gani CCM ilivo kwa sasa, Chenge ndiye ana unafuu kati yao ndo maana wameona angalau aweza kuwa kiongozi wao wa maadili!
 
Mpaka Kieleweke

JF-Expert Member
Feb 27, 2007
4,132
1,563
Huyu Chenge ndio mkurugenzi wa makampuni kama Tangold,meremeta n.k yaliyohusika na wizi wa mabilioni ya pesa pale BOT, sasa wanapomfanya kuwa mjumbe wa kamati ya maadili nashindwa kupata mantiki hapa.

Huyu Chenge ndio huyu huyu ambaye mke wake alikuwa anawahonga wajumbe wa NEC kutoka kanda ya ziwa hadi anafika Dodoma na kumfanya kuwa wa kwanza kwa kupata kura nyingi zaidi ya hata waziri mkuu wake ,ndio leo wanampa maadili ,ili akafanye nini jamani?

Hapa niombe kueleimishwa kuwa maana ama kazi za hii kamati ni kufanya kitu gani>?

Ama Chenge ndio msafi huko CCM kuliko wengine waliobakia kwenye kamati kuu?
 
MzalendoHalisi

JF-Expert Member
Jun 24, 2007
4,136
704
Yaani Chenge ndo mwadilifu zaidi kuliko wengine?

Hii kali! sasa taabu ya Tz Nyerere ameshafariki na hakuna wa kumkaripia mweingine- wote akina BWM sii waadilifu! JK msanii!

Bora tu liende!
 
Mpaka Kieleweke

JF-Expert Member
Feb 27, 2007
4,132
1,563
Wakati huo huo kamati hiyo imefanya uteuzi wa viongozi wake katika kamati ya maadili baada ya ile ya kwanza kumaliza muda wake.

Walioteuliwa katika kamati mpya ni Andrew Chenge , Pindi Chama na Yusuf Omar Yusuf ambao alisema kuwa wataanza kazi yao kuanzia sasa na watakuwa madarakani kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia sasa.

source.mwananchi
 
Mafuchila

JF-Expert Member
Apr 29, 2006
752
62
Inasikitisha sana...huwezi kuamini pamoja na udhaifu wa Mkapa,lakini bado tume yake ya maadili ilikuwa na watu waadilifu, ingawa Mkapa binafsi alikataa kuipa ushirikiano. Kumweka mtu kama Chenge kwenye viatu vya mzee Paul Sozigwa naamini ni matusi sio tu kwa CCM bali kwa Taifa zima.
 
Mpaka Kieleweke

JF-Expert Member
Feb 27, 2007
4,132
1,563
Hapa inaonyesha jinsi ambavyo CCM wamekosa mtu mwafdilifu wa kumkabidhi chama na hapo tutegemee nini kama chama kimekabidhiwa rasimi kwa mafisadi?

Nafikiri kuna haja ya kuiamsha jamii ijue kuwa nchi hii inaongozwa na chama chenye viongozi wa aina gani na hivyo wasitegemee lolote la maana kutoka kwa wazee hawa kwani ni aibu .
 
Mpaka Kieleweke

JF-Expert Member
Feb 27, 2007
4,132
1,563
si, ameokoka huyu nasikia sasa anasali kwa yule jamaa mtoa mapepo

Kuokoka ninavyosikia ni kuwa ni pamoja na kurudisha mali ama vitu visivyo halali ,sasa huyu naye yampasa kurudisha zile alizochota BOT pamoja na zile alizochota wakati Barrick inaingia mikataba na serikali kwanza.

Kama ni kweli anasali kwa mtoa mapepo huenda huyu ndiye mkuu wa mapepo na hivyo mapepo madogo yanamtii na kutoka bila hata ya kubisha la sivyo ajisalimishe na kuweka mambo hadharani kwanza.
 
Idimi

JF-Expert Member
Mar 18, 2007
14,510
9,614
Nimepatwa na mshtuko mkubwa sana pale niliposoma leo kuwa eti Andrew Chenge amechaguliwa na kamati kuu ya CCM kuwa mjumbe wa kamati ya maadili.

Nimejiuliza swali hili ,hivi kuwa mjumbe wa kamati ya maadili maan yake si ni mtu wa kuhakikisha kuwa viongozi wenzake wanafuata maadili?

Ama kama wameamua kuufanya ufisadi sehemu ya chama chao basi Chenge anafaa kuwa mjumbe kwani kama hayo ndio maadili kwao nani awezaye kupinga chenge kuwa mjumbe humo?

Huyu Chenge nampinga kwa sababu kati ya watu waliouza taifa hili huyu ni wa kwanza akishirikiana na wakina Mkapa kuuza kila kilichomo ,na huyu ni fisadi mkubwa sana sasa kama anapewa kuwa mtu wa maadili hapo tumekwisha ....

Hivi huyu ni Chenge ambaye alishiriki kudizaini ile mikataba yenye utata tunayoipigia kelele ama mwingine?
Ufafanuzi tafadhali!
 
Mpaka Kieleweke

JF-Expert Member
Feb 27, 2007
4,132
1,563
Ndio huyo ambaye kwa sasa ni waziri wa miundo mbinu na ndio huyo aliyeuza taifa hili ili kujipatia pesa za kujenga nyumba kila mtaa pale kinondoni...
 
Gembe

JF-Expert Member
Sep 25, 2007
2,502
153
hivi mke wa chenge anafanya biashara gani,Niliwahi kukutana naye pale Dodoma wakati wa uchaguzi wa mkutano mkuu wa cham ila sikujua status yake.

pili nasikia hata jimbo aliloshinda chenge ni ukweni kwao na kina Chenge.So huyu mama nadhani ndie spinning wa huyu mwana ume..
 
MaMkwe

JF-Expert Member
Sep 5, 2007
284
21
Hapa inaonyesha jinsi ambavyo CCM wamekosa mtu mwafdilifu wa kumkabidhi chama na hapo tutegemee nini kama chama kimekabidhiwa rasimi kwa mafisadi?

Nafikiri kuna haja ya kuiamsha jamii ijue kuwa nchi hii inaongozwa na chama chenye viongozi wa aina gani na hivyo wasitegemee lolote la maana kutoka kwa wazee hawa kwani ni aibu .

Hapana waadilifu tupo tele, ila wengine wana kimbelembele, wanataka wawepo kila mahala. Sasa tumeamua kukisafisha chama chetu. Si umesikia wanene wameambiwa waamue moja siasa au biashara. Wengine siku zao zinahesabika.
 
Mafuchila

JF-Expert Member
Apr 29, 2006
752
62
Ndio huyo huyo Chenge aliyesimamia ile sheria ya TAKRIMA na kupitishwa na Bunge kabla mahakama hawajaifuta baada ya kumalizika kwa matumizi yake.
 
Idimi

JF-Expert Member
Mar 18, 2007
14,510
9,614
Hapana waadilifu tupo tele, ila wengine wana kimbelembele, wanataka wawepo kila mahala. Sasa tumeamua kukisafisha chama chetu. Si umesikia wanene wameambiwa waamue moja siasa au biashara. Wengine siku zao zinahesabika.

Ni vyema kama mmeamua kukisafisha chama, ambacho hata mimi naamini kwamba sio kila mtu kachafuka ndani yake. Ila sasa huo mkwara wa Kikwete (mwenyekiti wa chama)ni mzaha tu kwa sababu huwa wabunge wanasajili biashara zao kwa majina ya ndugu zao na wao wanaziendesha kwa rimoti tu, ukiachilia wachache ambao wamesajili biashara zao kwa majina yao halisi. Mnaposema wabunge wachague kimoja kati ya ubunge ama biashara nadhani mnamaanisha kwamba hawa wafuatao wasigombee ubunge mwaka 2010.
1. Nazir Karamagi (TICTS)
2. Basil P Mramba (Southern Link Contactors Ltd)
3. Mohamed Dewji (Mohamed Enterprises Ltd)
4. Ahmed Shabiby (Shabiby Express)
5. Nimrod E Mkono
6. Juma A Kapuya
7. Abood
8. Richard Nyaulawa n.k.

Je watakubali?
Tuendelee na mjadala.
 
Mpaka Kieleweke

JF-Expert Member
Feb 27, 2007
4,132
1,563
Hapana waadilifu tupo tele, ila wengine wana kimbelembele, wanataka wawepo kila mahala. Sasa tumeamua kukisafisha chama chetu. Si umesikia wanene wameambiwa waamue moja siasa au biashara. Wengine siku zao zinahesabika.

Hiki kusema kuwa chama kimeanza kusafishwa ilke hali wanaoingizwa kwenye kuandaa maadilib ya kukisafisha wenyewe ni wachafu kuliko uchafu wenyewe ni kujidanganya tena mchana kweupe .

Naamini kiuwa hilo lilikuwa ni jambo ama waswahili husema stori za baraza hakuna kitakachotokea hata siku moja juu ya hao kwani ndio wenye chama.

Alishasema kyuwa walarushwa ana majina yao lakini mwaka mzima umeisha hakuna hatua iliyochukuliwa kwa nini hili tumwamini JK?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Top Bottom