CCM imekosa DIRA?

Je CCM ni chama cha Kibepari, Kikomunisti, Kisoshalist, kiliberali, kiislam? CCM ni chama kinyonga na kila mahali kipo (katika hizo siasa tano juu)!! Ni kweli kuwa hata upinzani huoni sera hasa, lakini ni hatari kwa chama kinachoongoza serikali kukosa dira.

Upinzani haujawahi kuwa explicit kwenye mambo kama ubinafsishaji wa mali za umma, Uendeshaji wa uchumi, mambo ya nje, n.k. Vyama vya upinzani kwenye sera nyingi vinafanana na CCM; ila vina ahidi kutekeleza vizuri zaidi kuliko CCM. Ndo huwezi kuchora mstari wa wapiga kura. Wapiga kura siku zote wako confused na pole pole wataanza kupigia kura dini, makabila, n.k.

sera hata kama zipo, hazitekelezeki au wanaozisema hawatekelezi kile wanachosema. Kwa hiyo huo ni ukweli mtupu kuwa CCM hakina dira wala mwelekeo, kinaongozwa na matukio!! Hata vyama vya upinzani vinaongozwa na matukio vile vile!
Ungea yote lakini Islam is more than siasa and chama? please be infomed...
CCM ni chini ya sisimizi kwa uislamu!!!
CUF ni chini ya sisimizi kwa uislam!!!
Chadema ni chini ya sisimizi kwa uislamu!!!
Just to make it clear ndugu huwezi "linganisha mbingu na ardhi"
 
Tumain,
Ndo maana nikauliza kama CCM ni chama cha kiislam. Najua uislam ni zaidi ya CCM kama tembo na sisimizi ndo maana CCM inadandia gari la uislam ili kujihalalisha! Nadhani hapa tuko pamoja!
 
Tumain,
Ndo maana nikauliza kama CCM ni chama cha kiislam. Najua uislam ni zaidi ya CCM kama tembo na sisimizi ndo maana CCM inadandia gari la uislam ili kujihalalisha! Nadhani hapa tuko pamoja!
Kivipi fafanua?
 
Kwa kuingiza sera ambazo wanajua zinamshiko kwa uislam ndani ya election manifesto yao. Kadhi courts na kujiunga OIC ni purely mambo ya kidini ambayo CCM wanajua yana mshiko kwa waislam. Maana yake CCM wamebeba bango kama wateteaji wa maslahi ya waislam na uislam!!
 
Chama cha siasa maana yake ni ku-solve problems na mahitaji ya wananchi wake wakiwemo waislamu I see no problem with that kwakuwa ni mahitaji ya wananchi wa Tanzania
 
Suala la CCM haina dira liko wazi, Jambo kubwa ninalo liona je tutafanyaje kuiondoa CCM 2010 na mbinu zao hizi za kuiba kura na kubadilisha matokea, sasa cha muhimu ni kupata namna ya kuzui wizi wa kura na ubadilishaji matokeo ili tupate uchaguzi safi 2010
 
KipimaPembe,
Chama chochote kile kitakachochukua madaraka siku yeyote Tanzania madai mahitaji hayo yatakuwepo kutoka kwa wananchi waislamu Tanzania no matter how long it takes..you need just to solve the problem siyo kukimbia tatizo.
 
Chama cha siasa maana yake ni ku-solve problems na mahitaji ya wananchi wake wakiwemo waislamu I see no problem with that kwakuwa ni mahitaji ya wananchi wa Tanzania

Lakini kuwa na ajenda inayohusu waislam peke yao kama waislam, na hiyo ikawa ni sehemu ya manifesto ya chama ndo maana tunasema ni chama cha kiislam! Chama cha kijamaa hutetea ujamaa, cha kibepari hali kadhalika. Kinachotetea uislam kama dini basi ni cha kiislam!
 
KipimaPembe,
Chama chochote kile kitakachochukua madaraka siku yeyote Tanzania madai mahitaji hayo yatakuwepo kutoka kwa wananchi waislamu Tanzania no matter how long it takes..you need just to solve the problem siyo kukimbia tatizo.

Kwa hiyo kwa kuwa haya matatizo yatakuwepo na chama chochote kitakumbana nayo, iko haja basi ya sheria ya vyama vya siasa kubadilishwa ili dini ziruhusiwe kuanzisha vyama vya siasa? Au vyama vya siasa viruhusiwe kuwe na mrengo wa kidini?

Kwa sababu haya ni matatizo ya kidini ambayo yanahitaji solution ya kidini. Kupelekwa serikalini huoni kuwa ni kuyapeleka mahali ambapo siyo pake?
 
Lakini kuwa na ajenda inayohusu waislam peke yao kama waislam, na hiyo ikawa ni sehemu ya manifesto ya chama ndo maana tunasema ni chama cha kiislam! Chama cha kijamaa hutetea ujamaa, cha kibepari hali kadhalika. Kinachotetea uislam kama dini basi ni cha kiislam!
Sidhani kama wanatetea uislamu (nilishasema CCM ni chini ya sisimizi kwa Uislamu) wana solve matatizo ya wananchi waislamu ndiyo kazi yake, ndio maana inaomba ridhaa ya kuongoza nchi kusolve problems na kuwapa mahitaji wananchi wao
 
Tazama mambo yalivyo hivi sasa ndani ya chama chao hivi leo Nyerere angekuwa hai watu kama Wakina RA na wengine wasingeweza kukaa wala kuvaa nguo za kijani na kusema kuwa wao ni CCM, Leo wezi na mafisadi ndio CCM rafiki zao
 
Kwa hiyo kwa kuwa haya matatizo yatakuwepo na chama chochote kitakumbana nayo, iko haja basi ya sheria ya vyama vya siasa kubadilishwa ili dini ziruhusiwe kuanzisha vyama vya siasa? Au vyama vya siasa viruhusiwe kuwe na mrengo wa kidini?

Kwa sababu haya ni matatizo ya kidini ambayo yanahitaji solution ya kidini. Kupelekwa serikalini huoni kuwa ni kuyapeleka mahali ambapo siyo pake?
NO sidahni tunahitaji kubadilisha sheria ila chama cha siasa kilichopata ridhaa ya kuongoza (presume imechaguliwa na waislamu na wakrisot na wengine) itasolve problem ya kila jamii kutegemeana na mahitaji yake???
kwahiyo kwakuwa waislamu wanahitaji mahakama serikali inaangalia namna bora ya kuanzisha mahakama?? siyo kuwauliza wakristo nyie mnaonaje tuwape au tusiwape? wapi na wapi?
 
Shida yangu ni kuwa hii mahakama ikianzishwa na serikali kuna uwezekano serikali isiiendeshe kama wenye dini wanavyotaka. Kwanza haitaweza kabisa kwani serikali si competent kwenye masuala ya imani, tena inahusisha watu ambao imani hiyo haiwahusu.
 
Lakini vile vile ni suala la principle. Kwa serikali yenye sheria inayozuia vyama kuwa na mwelekeo wa kidini hapa tutakuwa tumesha compromise principle na sheria zetu. Kwa nini kwanza tusinge debate kuziondoa hizo sheria ili kama ni kutetewa na vyama vya siasa dini zote zipate hiyo advantage?
 
Ndani ya CCM wanajua wanachokifanya, Je sisi wananchi tunajua tunachokifanya?
 
Vyama vya upinzani havikuwahi kuwa na dira, havina dira na hakuna dalili kama vitakuwa na dira katika miaka michache ijayo.

Hata CCM haina dira.

Kama wangekuwa nayo basi TZ ingekuwa mbali mno. Kwa hiyo hakuna tofauti kati ya CCM na wapinzani.
 
CCM is riding on poverty and illiteracy of the Tanzanian masses. Wanakwenda kama farasi asiy na kichwa. Ndo maana kila kitu kwao ni sera. Matokeo yake hakuna kinachotekelezwa na hakuna anayeulizwa.
 
Vyama vya upinzani havikuwahi kuwa na dira, havina dira na hakuna dalili kama vitakuwa na dira katika miaka michache ijayo.
Kibs, mtu maarufu kuyasema maneno yanayofanana na haya katika miaka ya hivi karibuni alikuwa Kolimba... na sote tunajua aliyatamka dhidi ya nani
 
CCM inajua inachokifanya ,imeingiza udini na kukifanya chama cha CUF kionekane cha kidini na sasa kinaingiza ukabila ndani ya Chadema na vyama vingine saizi yao kuvisambaratisha.
 
Back
Top Bottom