Ccm imeisha sababisha madhara makubwa

Mkorosai

Member
Nov 17, 2010
65
0
Lile tone dogo la maji walilo anzisha wapiga kampeni wa chama cha mapinduzi mwaka 1995, wakaliacha lenyewe na kuliongezea mwaka 2000, sasa limekuwa kubwa na litaleta ghalika baada ya kulichochea kwenye uchaguzi wa mwaka 2010!!

Jana nilisikiliza kwa makini hotuba ya rais Kikwete alipokuwa anazindua bunge, nikamsikia akilalamika kuwa uchaguzi wa mwaka huu umeacha majeraha makubwa ya udini na akaomba wananchi wamsaidie kutibia hali hiyo ngumu. Mimi nimemshangaa sana maana amegeuka mbuni anayeficha kichwa chake kwenye mbawa akitegemea kuwa haonekani.

tatizo la udini kwenye uchaguzi lilianzishwa na CCM mwaka 1995 walipomwandama mgombea wa NCCR Mageuzi Augostine Mrema aliyekuwa na nguvu kubwa. Walimwadama kwa kampeni za udini na kumkosanisha na Waislam eti aliwafunga waislam waliokuwa wamevunja bucha za nguruwe!Walimnyanyasa sana hata akazikosa kura za Waislam. Mwaka 2000, CCM ilirudia mchezo huo huo ikamkaanga Mgombea Ibrahim lipumba aliyekuwa na nguvu kwamba anaongoza chama cha kiislam hata kumkosanisha na wakristo na akakosa kura zao.

Mwaka huu pia, CCM wamekuja na staili yao hiyo hiyo kuwa Dr.Slaa alitumwa na Kanisa na kwamba waislamu hawahitaji kumchagua Padre kafiri. Kwa kampeni chafu za namna hiyo kama ilivyo kuwa mwaka 2000 wakati Waislam walipoamua kuinga mkono CUF, wakristo nao wenye uelewa wa kati waliamua kumuunga mkono Dr. Slaa kwenye uchaguzi wa mwaka huu!

CCM na Kikwete wao wamemwaga maji na sasa wanaangalia namna ya kuyazoa!! Walichezea shilingi ****** na sasa itawarudi maana kwa kiasi kikubwa sasa CUF inakubalika sehemu yenye waislam wengi na CHADEMA inakubalika nchi nzima hasa zile zenye wakristo wengi. Sijui nani atayazoa haya maji maana wakati wa kampeni Kikwete hakuliona hili kuwa ni tatizo. aliona ni mbinu ya kumsaidia kushinda uchaguzi lakini hakuona kuwa itamuumiza kichwa kuongoza nchi aliyoigawa kwa misingi ya kidini.

Sasa watanzania tumefika mahali tuko sensitive na mambo ya Dini na hili Kikwete alishindwa kulikemea na kuliweka wazi wakati wa kampeni! mbona la nyongeza ya mishahara ya wafanyakazi hakuliogopa ingawa lilitumiwa na wapinzani wake? Hili la dini kama siyo yeye aliye liasisi, kwa nini hakulikemea hata kutishia kuwa hataki kura za wanaotumia udini?

Kikwete ana maswali mengi ya kujibu kutokana na madhara makubwa yaliyosababishwa na namna CCM ilivyoendesha kampeni zake.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom