CCM imehalalisha ukabila? Magufuli anahutubia kilugha

Jamani mimi sioni kosa hapa. Mfano mimi nimezaliwa iringa ni mhehe. Sasa nikienda kujinadi nyumbani kwangu nilikozaliwa nishindwe kutumia lugha yangu niliyozaliwa nayo kisa nitaambiwa makabila. Nafikiri kuzungumza lugha siyo issue, issue ni kutumia ukubwa wa kabila lako kuomba wakuchague wewe kwa favor ya kabila. Lakin pia amepita songea, iringa amekuwa akijaribu kutumia lugha za mahalia lengo kubwa ni kuonyesha yupo karibu na watu wake. So nafikiri tutofautishe hili. Nafikiri mtoa maada utakumbuka style aliyotumia Lowassa alisema wazi video zilisambaa si asemavyo magufuli. So be careful mzee

Hivi magufuli ni msukuma?
 
Alivyokuwa Mtwara aliwasalimia kimakonde. Kwa hiyo alifanya makosa!! Na hata Tobo lisu akiwa kahama aliwasalimia kwa lugha ya kisukuma. Nae ni mkabila!!
Suala siyo kusalimia ni sms na wito wa wasukuma wamchague mgombea kwa sababu anatokea huko, hayo yamesemwa majukwaani Geita, Meatu, Kahama na kwingineko Kanda ya Ziwa. Swali je ingekuwa ni EL nadhani kelele za ukabila zingekuwa zimepamba moto! Kweli EL anastahili huruma, hatendewi Haki na wapinzani wake vinginevyo tuseme wapinzani hao ni washari.
 
Jamani magufuli anaongea lugha nyingi mpaka anashangaza lol huyu ndie atakayetuunganisha vizuri..Magufuli ikulu ni yako....wewe ndio chaguo la Mungu..hukutegemea utafika ulipofika,hukuwa na makun nginja nginja hadi,ni kazi tu mpaka ikulu
Lol! Jiulize anajua kiingereza ama kiswahili?
congretions=congratulations
Laha=raha
UN,AU atahutubia kwa kisukuma wamwelewe
nb mkewe mwalimu wa kiingereza msingi
 
Magufuli alikuwa mwalimu was kemia na physics inamana alifundisha kwa kiswahili pale Sengerema sec.magufuli jembeee
 
Mbona ccm karibu wote ni waislam? Wwkiristo wasiichague?

Hoja hiyo haina uzito, ccm tafteni hoja nyingine. Mimi ni mwana ccm na sio mchaga lakini nampa kura lowassa.

...........lowassa anapewa kura na wachaga kwa sababu amewapa pesa na malofa na wapumbavu wanaojipendekeza !
Kwakuwa wewe si mchaga basi umo kwenye hilo kundi la pili ! kaka km
 
Last edited by a moderator:

Lowassa na Ikulu.JPG
 
Umemsingizia, sijamsikia akihamasisha ukabila. Tena kama ukabila basi anakosea kuwaambia wananchi wasiendekeze ukabila. Magufuli msukuma na kama angesema wasukuma wote wampigie kura hiyo nayo ingekuwa kali naamini hakuna mgombea atamsogelea lakini anajua jukumu lake namsifia hajahamasisha ukabila zaidi ya kusalimia kwa kisukuma lakini pia na salam za makabila kibao anatoa. Mimi ni msukuma ningependa pia wasukuma waongoze nchi lakini isiwe kigezo tosha cha kumpima mgombea
 
We Great thinker unaongea vitu kama hivyo!? insult to the JF!! Sijioni kama nipo ktk level ya kubishana na wewe! Yaani TZ kuna sehemu kuna lugha kuu kupita Kiswahili?, je hao wanaoishi huko huwa wanasikiliza au kusoma media ipi mkuu? Are we talking abt TZ or???
Acha ulofa wewe! Upo wapi? Au unabeba boksi ughaibuni?
 
Umemsingizia, sijamsikia akihamasisha ukabila. Tena kama ukabila basi anakosea kuwaambia wananchi wasiendekeze ukabila. Magufuli msukuma na kama angesema wasukuma wote wampigie kura hiyo nayo ingekuwa kali naamini hakuna mgombea atamsogelea lakini anajua jukumu lake namsifia hajahamasisha ukabila zaidi ya kusalimia kwa kisukuma lakini pia na salam za makabila kibao anatoa. Mimi ni msukuma ningependa pia wasukuma waongoze nchi lakini isiwe kigezo tosha cha kumpima mgombea

mkabila sana na mbaguzi ingawa anafanya kinafiki akiwa kanda ya ziwa amefanya ukabila wa aibu yeye na Bulembo ni aibu kwa karne hiii-leo babati anajifanya tanzania hakuna ukabila mbona hakusema hayo kanda ya ziwa?
 
Yupo manyara now Haleruya za kumwaga Aisee ...... tuombe mungu tu lkn kwa kweli jamaa anajisahau yakuwa anahutubia dini tofauti na wengine hawana dini.
 
Umemsingizia, sijamsikia akihamasisha ukabila. Tena kama ukabila basi anakosea kuwaambia wananchi wasiendekeze ukabila. Magufuli msukuma na kama angesema wasukuma wote wampigie kura hiyo nayo ingekuwa kali naamini hakuna mgombea atamsogelea lakini anajua jukumu lake namsifia hajahamasisha ukabila zaidi ya kusalimia kwa kisukuma lakini pia na salam za makabila kibao anatoa. Mimi ni msukuma ningependa pia wasukuma waongoze nchi lakini isiwe kigezo tosha cha kumpima mgombea

kwani magufuli MSUKUMA AU MZINZA? au MZINZA = MSUKUMA?
 
Magufuli Akichaguliwa Ataleta Machafuko!, Afanyiwe Ukatili! Kwenye Sanduku La Kura!
 
baadhi ya wasukuma hawafahamu kiswahili. anapaswa afikishe ujumbe, mnashindwa kuangalia chama cha mbowe mnaangalia magururi
 
kwani magufuli MSUKUMA AU MZINZA? au MZINZA = MSUKUMA?

Ukienda Ulaya....weusi wote tunaitwa African; and we are real proud. Wazinza, wasukuma na wanyamwezi...n.k. wote tunawaita wanyamwezi au wasukuma ni ndugu na wanaelewana kilugha
 
Kwa wale washabiki na wasiolewa umuhimu wa mada hii watakuja na kuanza kutukana au kuchangia nje ya mada, ila kama mtanzania kijana nimeanza kuona viashiria vya nchi yetu kuingia katika ubaguzi wa kikabila na kikanda, na hali hii imeanzishwa na JPM.

Mwalimu Nyerere alikemea kwa nguvu zote dhambi hii ya ubaguzi wa kikabila na kikanda na akaonya kuwa mtu wa tabia hii hatufai hata kidogo kuwa kiongozi wa nchi yetu. CCM kama chama kikuu waliienzi kauli na busara hii ya Mwalimu Nyerere kiasi cha kuweza hata kutuhumu chama chochote kilichoonekana kuwa na dalili za ukabila na ukanda.

Ni mara nyingi tumesikia viongozi wa ccm na makada wakikituhumu chama cha chadema kuwa ni cha wachaga. Pia Cuf iliwahi kutuhumu na ccm kuwa chama cha waislamu kutokana tu na hisia tu.

Leo tunaona wazi kwa macho yetu jinsi JPM alivyoasisi ukabila na ukanda, kiasi kwamba amekuwa akihutubia kwa lugha ya kisukuma anapokuwa kanda ya ziwa, wapo watakaomtetea ila ukweli ni huu, hakuna mahali popote ndani ya taifa hili ambapo kuna kabila moja tu, hata umasaini.

Leo kwa bahati mbaya sana mbunge wa Geita msukuma ameongea maneno mengi kwa kisukuma akiwa anahutubia mkutano wa hadhara ambao mzee Mkapa na JPM ni miongoni mwa watu waliokuwa wanamsikiliza.

Kwa namna tunavyoendelea ukabila na ukanda utajitokeza kwa nguvu sana nchini, na hii isipokemewa tutajikuta pabaya.

Tusipoziba ufa tutajenga ukuta, ccm zuieni jambo hili mapema.
 
Back
Top Bottom