CCM imefanya makosa makubwa kuyateka maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM imefanya makosa makubwa kuyateka maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Tuko, Jul 5, 2011.

 1. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #1
  Jul 5, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  CCM imetangaza kuadhimisha kile wanachokiita 'MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA BARA', Uhusiano wake na chama cha TANU.

  Binafsi naamini kama chama tawala, na kinachoongoza serikali, CCM haijawatendea haki watanzania kwa 'kuiteka siku hiyo na kuiadhimisha kichamachama'

  Nilimwambia Nape jambo hili asubuhi, lakini akatetea kuwa hata kama mtu haipendi TANU, au haipendi CCM, lazima historia ienziwe. Mi sipingani na Nape kwa hili, lakini namshangaa kwa sababu historia ni historia, haiwezi kubadilishwa. Pamoja na pengine nia nzuri ya CCM ya kukienzi TANU, lakini modality waliyotumia sio sahihi.

  Kwa ufupi ni kuwa watanzania watachukulia kuwa maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru yamechukuliwa na kuhodhiwa na CCM, yanaadhimishwa katika mashina na matawi ya CCM. Raisi ataongea na mabalozi wa nyumba kumi wa CCM, hivyo hata kama atakuja kufanya jambo jingine lolote kwa watanzania wote katika maadhimishi ya miaka 50, naamini kila mtu ataona kuwa ni mwendelezo wa CCM, kuadhimisha siku hii.

  Binafsi nilidhani kuwa serikali ingekuwa makini kuifanya siku hii iwe ya kitaifa zaidi, ijenge mazingira ambayo wananchi wangesahau tofauti zao za kisiasa, na kuangali baada ya kujitawala wenyewe kwa miaka hamsini, ni lipi tumefaulu, ni lipi tumefeli, na lipi tunatakiwa kujirekebisha kama taifa. Lakini kwa uamuzi wa CCM wa kuiteka siku hii, na kuadhimisha kichama, sishangai kama maadhimishi haya yatagubikwa na malumbano, maandamano, kebezana, na hata pengine kutukanana, na haya yote yatakuwa yamesababishwa na CCM.

  Kwa hali ilivyo, usishangae ukisikia CHADEMA nao wakaja ja slogan yao MIAKA 50 YA UHURU, ......................
   
 2. MANI

  MANI Platinum Member

  #2
  Jul 5, 2011
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,410
  Likes Received: 1,863
  Trophy Points: 280
  Lakini mbona sisi tunajua tofauti ya TANU na CCM !
   
 3. Limbani

  Limbani JF-Expert Member

  #3
  Jul 5, 2011
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 1,441
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
   
Loading...