Kama siyo mbinu ya JPM Kupiga Marufuku mikutano ya kisiasa tangu Alipoingia Madarakani, sasa hivi tungekuwa tunaongea mengine kabisa, Nina Imani hata kitendo cha kuvunja katiba ya Nchi makusudi ni baada ya Kuona CCM ilivyozidiwa ktk Kampeni za Uraisi, 2015. Binafsi Mimi siyo mfuasi wa Chama chochote cha siasa, ila Mmi ni Mtanzania ninayependa sana Nchi yangu.
Lakini kutokana na Chama hiki kushinwa kabisa kuwa na mbinu za kuwaletea Maendeleo Watanzania, niseme tu ukweli, ninatamani hiki chama kipumzishwe na tukikabidhi kazi chama kingine chochote cha siasa labda tunaweza kuona tofauti. Kwa sababu kwa CCM iliyopo ambayo imeshachoka kabisa, hata tungewapa tena miaka 50, bado tutadidimia tu, hawana jipya tena.
Kwanza tu mjue, Viongozi wengi wanaotuongoza Kutoka CCM ni wazee na wengi ni wagonjwa. Ushahidi ni wakati wa Yule babu wa Loliondo alipoamua Kugawa dawa yake maarufu Kama Kikombe cha Babu. Tulishuhudia jinsi Viongozi wetu walivyomiminika kugombea kikombe. bahati mbaya kile kikombe kilikuwa ni Tiba feki, kwa hiyo Mkae mkijua wale watu bado wanaumwa tena kwa sasa maradhi ndiyo yamekomaa, Mtu yeyote anayeumwa Mara nyingi huwa na msongo wa mawazo na Mara nyingi huwa hutumia fikra na akili zake zote kufikiri juu ya hatma ya Maradhi yake, Kwa hiyo tusitegemee lolote jipya juu ya hawa watu, ila inatakiwa tuwasaidie kuwaambia Wapumzike Wameshatutumikia vya kutosha, sasa ni Muda wetu kuwatunza.
Sababu kubwa ya JPM Kuangusha uchumi wa Nchi ni kutumia nguvu na Raslimali nyingi sana kuhakikisha anavunja nguvu ya Upinzani, badala ya Kuongoza Nchi yeye akaamua kudeal na Wapinzani. Kumbe alitakiwa tu kupiga mahesabu ya kawaida na apate majibu ya ni kwanini ni vigumu sana kuua upinzani. Matokeo yake ilipokuja ripoti ya CAG ikaonekana Tsh, 1.5 Trilion hakuna na Matumizi yake hayajulikani. Raisi mwenyewe Hiyo ripoti ilimuumiza sana, kwa sababu ninavyomjua Mimi huyu JPM ni mtu mwaminifu sana. Nina Imani alipojaribu kuwauliza watu wake walimwambia kuwa Hii 1.5 trillion ndiyo gharama ya Kukilinda Chama.
Gharama ya kuilinda CCM kwa sasa ni kubwa kuliko bajeti ya wizara yoyote ktk Nchi hii, kwa sababu kila mtu anajua, CCM Haina jipya na Muda wake umepita, CCM ya Sasa Bila Polisi haiwezi kupata hata 15% ya kura halali ktk uwanja wa Haki wa Kidemokrasia, Kamanda Siro huu ndiyo Muda wake halali kabisa kutajirika pamoja na Maafisa wake wa ngazi za juu, Ingekuwa Mimi ndiyo Kamanda Siro sasa hivi ningekuwa tajiri Mkubwa katika matajiri wa nchi hii. Potelea mbali.
Ikiwa vyama vya siasa vimezuwiwa kufanya mikutano kwa miaka 5 kinyume kabisa cha Sheria ya Nchi yetu, na wakati huo huo CCM pekee ndiyo wanaruhusiwa kufanya mikutano na ikiwa Tv, Redio na magazeti karibu yote yanaiimbia CCM pambio na bado watu hawaelewi na hawataki kabisa kusikia CCM, ni Matokeo ya kwamba, Sikio limeshakufa, hata utie ubani kiasi gani lazima harufu itatoka tu.
Rai yangu, kwa Wahusika wote wa CCM, Nguvu Mnayoitumia kukilinda hiki Chama Cha Wazee ambacho kimeshakufa,Ni bora mkatumia fedha hizo kwa kuwekeza ktk miradi ya maendeleo kwa Mustakabali wa Uzee wenu.