CCM Imechokwa, CHADEMA Haijajipanga!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,440
113,449
Wanabodi,

Kutokana na majukumu yangu kama Mshauri wa Siasa wa Ubalozi fulani, moja ya kazi zangu ni kufanya kitu kinaitwa "stakeholders mapping", hii hufanyika kwa kitu kinachoitwa "interactions" hivyo from time to time, huwa nawajibika kuwapo Dodoma kwa interactions na waheshimiwa wabunge.

Sasa nikiwa hapa Dodoma kwenye hili Bunge jipya, nimebahatika kukutana baadhi ya wabunge wapya wa CCM na wa kambi ya upinzani, kujaribu kufahamiana nao, sio siri, baadhi yao. kwa kuwaangalia tuu na kuzungumza nao, hawana kabisa any substance ya ni nini kilichowafanya washinde, na kwa wabunge wa viti maalum ndio kabisa usiseme!, kwa baadhi ya wabunge hawa wa viti maalum, sikuona ni kipi kilichowafanya wateuliwe na vyama vyao kuwa wabunge wa viti maalum!, wengi wao japo wameteuliwa kutimiza hitaji la usawa wa kijinsia, sababu za uteuzi wa baadhi yao ni ile jinsia yao kwa matumizi ya kutoa zile huduma muhimu za kibinaadamu kama vidumu vya waheshimiwa sana na sio kwa ajili ya kuchangia mijadala na hoja nzito za bungeni, na hili litathibitishwa na michango yao bungeni katika mijadala mbalimbali, kuna baadhi mtawashuhudia kazi yao itakuwa ni kuonyesha umaridadi wa mavazi, kuonyeshea shapes na kuuza tuu sura kule mjengoni! na mwisho wa siku hivi 'vidumu' vitakuja kuwaponza wamiliki wa 'vidumu' hivi kwa kupata mapigo ya karma ya wake wa ndoa wa waheshimiwa hao.

Nilipoongea na baadhi ya wale makamanda waliokata magogo kule Kanda ya Ziwa, kiukweli nimewaona baadhi yao ni watu wa kawaida sana tuu with nothing special kilichowafanya wachaguliwe na kuibwaga CCM na vigogo wake wenye nguvu, influence na pesa, iliyoota mizizi kwenye kanda hivyo , hivyo nimefikia jibu moja tuu la uhakika, kuwa CCM katika baadhi ya maeneo, imechokwa mpaka basi!, upinzani hata ungesimamisha jiwe, jiwe lingechaguliwa!, nadhani hii ni moja ya sababu kuu iliyopelekea wengi wa waliojiandikisha kupiga kura, hawakujitokeza kupiga kura, waliona kujitokeza kupiga kura ni wastage of their valuable time, ni kujisumbua tuu!.

Nasisitiza CCM imechokwa, na ule ushindi wa kishindo wa Kikwete toka asilimia Zaidi ya 80% mwaka 2005 hadi asilimia 60% 2010, ni uthibitisho tosha, Watanzania sasa wameichoka CCM ila pia hawakuwachagua wapinzani kwa wingi zaidi, kwa sababu wapinzani bado hawajaonyesha kukomaa vya kutosha kuweza kukabidhiwa nchi kwa kushindwa kuonyesha utayari kukamata dola na kutawala.

Najua kwa dhati, japo CCM na JK wanafurahia ushindi huu kiduchu kwa furaha, ni furaha ya machoni tuu, lakini moyoni ni maumivu na vilio kwa huzuni ya kukataliwa toka ushindi wa kishindo wa asilimia 80% ya 2005 hadi ushindi kiduchu wa asilimia 60 za 2010, na hiyo asilimia 20% ya kukataliwa, kukataliwa ni kukataliwa tuu kunauma!.

Hivyo chama makini chochote lazima kikae chini na kujiuliza, hivyo CCM lazima watakaa chini na kujiuliza kulikoni, ni katika kujiuliza huko, huenda wakajipanga upya na kuja kwa mbinu mpya, kwa nguvu zaidi na kasi zaidi, ila kwa vile CCM imechokwa, hata ijipange upya vipi, kama Chadema itajipanga, then kwa CCM, safari ya kwaheri ndio imeanza, there is nothing to stop it from failing down unless ibadilike kwa revamping.

Dawa pekee ya kuitibu CCM chovu iliyochokwa, ni kuirevamp CCM completely, task nambari moja ni Makamba and his old guards pale Lumumba, should go, kupisha new blood. Tena CCM msisubiri mpaka uchaguzi mkuu wa chama chenu, miaka miwili ijayo (2012), itakuwa too little too late. If you are to do anything, just do it now and fast!. Leteni fresh blood kina January type, Kippi, Nape type and the like ambao wanaziweza siasa za kisasa za .dot com type.

Hakuna ubishi, Chadema imenyanyuka, toka wabunge 5 mpaka 22 wa kuchaguliwa tena majimbo ya haja yenye impact ikiwemo kuyashika majiji makubwa katika mikoa the big five!, huku sio kukua bali ni kupaa, tatizo kubwa la Chadema, bado hawajipanga mkao wa kichama tawala, ili kikabidhiwe nchi, kitawale, Chadema bado kimekaa kichama harakati, hivyo kuna wengi wanakiona kama bado hakijakomaa kiasi cha kukabidhiwa ikulu yetu!.

Kichama, wanachadema mkubali msikubali, chama chenu kwa sasa japo kipo juu, lakini bado hamjakomaa kufikia kiwango cha kukabidhiwa nchi, bado mko kiuana harakati zaidi kuliko ki chama tawala, na hamjajipanga kwa sura ya kitaifa na utayari wa kutawala nchi.

Kwa vile CCM imechokwa na imekaa mkao wa kifo, hii ndio opportunity yenu Chadema kuongeza offensive ili kuisindikiza CCM kaburini, kwa kujipanga kimkakati ili muwe na sura ya kitaifa, kwa kuonyesha Watanzania kuwa mmekomaa na mko tayari kutawala, hivyo Watanzania watawamini watawakabidhi nchi mwaka 2015.

Sehemu muhimu kabisa kwa Chadema to keep watch kuhakikisha hamuiachii ni hiyo Kanda ya Ziwa ambayo imeipokonya CCM na kuishika, hii ndio Kanda determinant ya nani anakuwa rais wa nchi hii. Aliyeishika Kanda ya Ziwa ndio rais wa Tanzania. Hivyo CCM imeumia sana kupoteza Kanda ya Ziwa na wataelekeza all it might powers to reclaim what it has lost, hivyo Chadema itumie uwezo wake wote kulinda what it has!.

Kwa upande wa Chadema, lazima kibadilike, first and foremost, anzeni na Mwenyekiti wenu Freeman Mbowe, he should go!. Ajiuzulu uenyekiti, ampishe more able person kama Dr. Slaa kwenye usukani wa chama, Katibu Mkuu mpeni Zitto strategically, hii itaifuta ile dhana ya udini na nepotisim kwenye chama chenu, na kulivua lile koti la udini, ukanda na ukabila ili walioichoka CCM wawafungulie mikono kwa kujitokeza kwa wingi kuwapigia kura 2015 kwa kujionyesha Chadema ni chama cha wote, dini zote na kanda zote.

Kupumzishwa kwa Freeman Mbowe sio kuwa hafai no, anafaa sana lakini kwa background yake na nature ya kazi zake, as a businessman, hapo alipoifikisha Chadema amaishafanya kazi kubwa na kufikia mwisho wa uwezo wake. Kwa background yake ya a former DJ na sasa ni mfanyabiashara, focus ya wafanyabiashara kote dunia nzima ni maximisation of profits, hivyo Mbowe atahitaji ruzuku ya Chadema itumike kuivest kwenye assets, kwenye vitu vya kuonekanika yaani assets kama magari, mavazi, etc

Ili Chadema kiweze kushika nchi 2015, it has to invest on people na sio ku invest kwenye vitu. Chadema must invest kwenye mass mobilisation na sio kutegemea mikutano ya hadhara na maandamano. Chadema needs to have able people kuiwezesha kushika dola five years to come kwa kutumia reaching out mechanism kuwafikia the mases kwa kumiliki media yake yenyewe. Chadema lazima ifanye recruitment ya loyal able people, watakaokuja kuendesha serikali ya Chadema. Mbowe hawezi kukubali ruzuku ya Chadema itumike to invest on people, kwasabu it's a loss making venture kwa mfanyabiashara na kuivest kwenye mass media sio profitable investment kwa business man ambaye ni in for profits making!. Dr.Slaa na Zitto sio wafanyabiashara hawa ni ma technocrats. Chama kishikwe na wanasiasa watendaji ma technocrats na sio wanasiasa wafanyabiashara!. Chadema iwekeze kwenye watu na kupanua mtandao wake hadi vijijini, ili kwenda kuiongoa CCM kuanzia kule chini kabisa kwenye mizizi yake ambako ni kule kwenye mashina. Chadema imiliki media yake yenyeshe for mass mobilization na sio kutegemea mikutano na maandamano, huko ni kuendeleza uanaharakati, Chadema inatakiwa kukaa mkao wa kutawala, ikitangaza kitu, kinafika Tanzania nzima!

Chadema ina tatizo la umimi. Kitendo cha Chadema kuihodhi kambi rasmi ya upinzani Bungeni, huu ni udhaifu mkubwa ambao hautawafikisha mbali. Pamoja na kanuni za Bunge kuruhusu Chadema kuunda kambi rasmi ya upinzani peke yake, Chadema peke yenu hamuwezi!. Lazima muwashirikishe wapinzani wengine wote hata kama hawastahili. You have to unite and work as one against a common enemy. Umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu.

Kama CCM ndio hii iko ICU na Chadema haijajipanga, spika ndio huyo mama ma over confidence na over reaction, 2015 tutegemee nini?. Kama Chadema haitabadilika, then 2015, japo imechokwa, japo chovu, ni CCM tena!.

Angalizo: Paskali wa Jamii Forums ni political commentator ambaye yuko objective, bila kuegemea chama chochote, upande wowote na hufanya kazi kwa wote, ila ni muumini wa demokrasia ya kweli ndani ya bunge for the balance of power, hivyo nashangilia sana kambi ya upinzani kuingiza vichwa 100 bungeni, ni matumaini yangu, 2015 kazi itakamilishwa!.

Paskali
 
Hili la kambi ya upinzani bungeni ata nami naona kuna haja ya kuwashilikisha vyama vingine otherwise divided as they are winning a common enemy will be an issue
 
PASCO,

Mwanajamvi nimefurahi sana kujitambulisha kama Political analyst. Ningelifurahi sana kusaidia Taifa lako kama analist kama ungelitusaidia yafuatayo:

i) Utafuti unaonyesha nini duniani kuhusu Leader of the Opposition katika mifumo ya mabunge yaliyoko Duniani. Kwa mtu yeyote anayefanya analysis angelitegemea kuona American Model na WestMinster Model zinaeleza nini. Analysis yako ime base kwa personalities badala ya Model na analysis ya aina hii kwa maoni yangu ni ya hatari sana kwa kuwa inakosa misingi ya kisayansi. Politics is science and should never be reduced to anything less than empirical analysis to be scientific.

ii) Analysis yako imetoa Conclusions kabla ya kujenga plausible major and minor. Scientific and logical conclusion can only be based on a well founded "major and minor". Ili tunaofuatilia tuweze kunufaika na analysis yako ningelitegemea a properly constitued logical arugement inayofuata clasical logical construction ambayo ndio msingi wa analysis yoyote ambayo ni credible.

iii) Analysis yako inaonekana kukosa basic and simple facts. Kwa mfano unapoeleza muundo wa Kambi ya Upinzani tungelitegemea misingi ya hoja yako, analysis ya kwanini tuko hapa tulipo ambapo Chadema wameunda Kambi bila kuwashirikisha CUF and reasons leading to the same, kama kulikuwa na majadiliano yeyote yalikuwapo kwanini yalishindikana, Political Statusquo ya CUF ndani ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inayoongozwa na CCM kama ambavyo Serikali ya Jamhuri ya Muungano inaongozwa pia na CCM hiyo hiyo na Thesis na Antithesis inayotokana na hali hiyo na matokeo yake au conclusions zinazotokana na situation hiyo kutokana na empirical analysis. Vinginevyo analysis unayojenga inaweza kuwa flawed na ikawa msingi mkubwa sana wa political fallacy ambayo ni ya hatari sana katika analysis ya kisayansi, na athari yake ni mbaya kwa kuwa wako wengi ambao watatumia analysis hiyo bila kuifanyia uchambuzi independent wakiamini umetolewa kwa msingi wa kisayansi. Athari za Fallacies katika historia inajulikana sana kwa historical philosophers pamoja na political philosophers.

iv) Maneno "Kuhodhi", "ubinafsi", "umimi", bila kuwa qualified ni manifestation ya "emotion", na kwa kiwango kikubwa ya "ego". Bila vigezo sahihi ya kisayansi maneno hayo ni manifestation kuwa ya kuwa subjective ambayo kimsingi ni kinyume na dhana ya "objective Political analyist unayoijenga. Hivyo ili tunufaike na matumizi ya maneno haya ningelitamani sana kuona qualification ya maneno hayo ili yaweze kulisaidia Taifa letu, kuliko kuyatumbukiza kwa mfumo unaoweza kutafsiriwa kwa sura mbalimbali. Na kwa bahati mbaya hoja hizi zimekwisha kujitokeza mara nyingi kwenye jamvi letu. Kwa vile nia na lengo la jamvi ni kusaida Taifa letu, na Taifa linajengwa na watu wenye uchungu wenye sifa na ujuzi mbalimbali, na hasa kwa kuwa umejitokeza hadharani kama Political Analist ambaye ni "objective" basi nilikuwa nimefurahi sana kupata analysis ambayo inatumia objective criteteria katika hoja zote ulizokuwa unajenga.

Natanguliza shukrani za dhati, na ninategemea kupata objective political analysis ya mapendekezo yako.

Mungu Ibariki Tanzania.
 
Dr.W.Slaa

Unajua wakati mwingine usim-judge mtu kwa ukimya wake wakati mwingine ukimya wa Mbowe ndo unaiweka CHADEMA pale ilipo! japo unaafiki ya kuwa CHADEMA imeongezeka viti unasahau kuwa imeongeza viti hivyo chini ya uenyekiti wa Mbowe na viongozi wengine kuanzia Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu (mikakati na mipango ilifanyika chini ya uongozi wake kwa kushirikiana na wengine)!

Jamani tuache kunyanyapaa.. Zitto itafika wakati atapata huo Uenyekiti au Ukatibu Mkuu anaoutaka! uchaguzi wa vyama utakuja tena! na si kwa jinsi anayotumia sasa kwa ku-discredit the current leaders (naomba ajifunze hili)! Meanwhile siwezi afiki mtu mwingine yeyote kupewa uongozi wa kambi ya Upinzani Bungeni zaidi ya Mbowe maana hiyo itakuwa ni kum-discredit kiongozi wa chama ilhali yupo Bungeni na nathani wenzetu walioanza demokrasia mapema waliliona hili ndo maana kama chairman wa chama ni Mbunge anakuwa kiongozi pia wa chama hata Bungeni!

Tuache ku-pin point individuals unfit for our personal weaknessses like judging someone on identities! na kuwa-discredit for misjudging their merits, uongozi si kupayuka tu! na busara ya kuwaweka wenzako woote pamoja na kusikiliza mawazo ya wengine jamani! Hebu imagine kama Mh Zitto angekuwa Chairman wa chama katika lile suala la Dowans halafu akatofautiana na wenzie juu ya Msimamo; what would have happened? si chama kingalifia mbali kama NCCR-Mageuzi (Mchawi angetafutwa!) lakini impact yake ilikuwa ndogo kwa vile position yake si nzito kama ya chairman...!

Jamani tuwe na subira, Zitto anapaswa kukomaa zaidi haswa kwenye maswala ya ndani ya chama na overall party stands vs public affairs! Kuna mambo hayapaswi kuenda nje na personal stands without reservation of other opinions ni sumu kwa chama haswa kama ukiwa kiongozi wake! nasema hivi kwa sababu so far sijaona issue zozote ambazo zingeweza kuleta mtafaruku kama uliotokea hapo kabla ukimhusisha huyu ndugu yetu..! Ajifunze na uchaguzi unakuja ajipange vizuri na ajaribu kuepuka media katika baadhi ya maswala!
 
Last edited by a moderator:
"Dr.W.Slaa

Dr. Slaa, asante sana kwa kunijibu, kitendo tuu cha kuonyesha umenisoma, hiyo ni faraja tosha kwangu kuwa hata kama hamtayarekebisha mapungufu, my only defence ni kuwa tuliwaambia, mesej sent.

Kwa kuanzia, nakupongeza sana wewe binafsi kugombea, umeleta changamoto ambayo haijawahi kutokea.Ushindi wa hayo majimbo mliyoyatwaa ni uthibitisho wa the powers within you. For the first time in my life, nimehamasika na naweza kutupa karata yangu mahali 2015.

Pole kwa kutopata ushindi uliotarajiwa, ila amini usiamini, wewe bado ni mshindi kwenye roho za watu, na JK ni mshindi kwenye makatasi ya kura. Tunatakiwa kuwa wa shukrani kwa kidogo chochote tunachopata, wewe mwenye majimbo 5 hadi 22 na la 23 ni kesho, ulitakiwa kuonyesha appreciation kwa Watanzania waliokuamini, kitendo cha kususia kutangazwa matokeo for whataver reasons, ni political immaturity, na binafsi nilifadhaishwa sana, umepoteza the golden opportunity ya kuspeak out you mind, hata kama hatimaye utakuja kuita waandishi na kuyasema ya moyoni, never will they have the impact kama ungejitokeza pale na kusema nimekuja siyakubali matokeo kwa sababu yamechakachuliwa.

Nakubaliana na wewe kuhusu weakneses kwenye analysis yangu, infact kitu nilichokisema hapa, its only my observation. True analysis inapatikana baada ya kufanya research, nakiri sijafanya research yoyote serious zaidi ya observation tuu, ila hili jicho langu ndilo la mwananchi wa kawaida kule kijijini na sio jicho la reseacher as a member of academia.

La kambi ya upinzani, nimelisemea, if you go by the books, it is ok kwa vile nyinyi peke yenu mnaconstitute ile quoram kwa mujibu wa kanuni, don't play by the book, just play by reality, logic and moderation. Umimi wenu Chadema, haujaanza leo, msipokubali weaknesses zenu, you can not turn them ito streghths. Naomba nisiende tena kwenye personalities zaidi, tunakuomba kaa siti ya mbele, shika usukani, pangeni safu yenu vizuri, futeni dhana zote zilizojengeka dhidi yenu ziwe za kweli au za kizushi, 2015 ikulu ni yenu, maana wale milioni 12 waliojiandikisha halafu hawakupiga kura, ndio mtaji wenu wa 2015 haswa ukizingatia vijana wa shule za kata ndio watakuwa vyuoni!.

Asante tena.
 
I support 100% Dr. Slaa Peoples President.

Pasco in several occasion binafsi nimekuwa nikifuatilia post zako, mara nyingi tunapofuatilia kukuuliza maswali ya kimsing kama "source" au "basis" ya unachoandika huwa hutoi majibu.

Hata hivyo huwa unakuwa mwepesi sana kukimbilia katika hoja nyepesi. I think to my opinion that is wrong. Wakati mwingine binafsi huwa nafikiria kuwa una "ego" ambazo unapenda sana kujinyanyua. Mara nyingi huwa unakimbilia kuanzisha baadhi ya threads hata kama unajua fika threads zinazofanana na hizo zipo, that is wrong.

Leo umekutana na Dr. wa ukweli, mzoefu wa kisiasa na President of the People, sijui utajibu nini.

Binafsi nilibahatika last year kuongea kwa simu na Dr. Slaa, kubwa lilikuwa kutaka kumpa changamoto kwa nini wasiunganishe nguvu na CUF, NCCR, UDP n.k. Facts nilizopewa nillishiwa nguvu na kujua hakika ni vyama vipi vinakwamisha upinzani. In short CHADEMA walionyesha kwa vitendo huko nyuma kwa kuamua kutosimamisha mgombea wa Urais ili kumuunga yule wa CUF. Iliniuma sana kwa nini vyama vingi mamluki wa kweli. Niliongea na viongozi wa vyama vingine viwili na sikuona seriousness yoyote.

Dr. Slaa tunashukuru sana kwa kupata muda kuja kujibu hoja zetu. Tunakuthamini sana kuliko unavyodhani. A quick scan ya post mbalimbali hapa ni kipimo tosha ya kiasi gani wewe binafsi na CHADEMA mnakubalika. Afterall there should be a start. Rome was not built in a single day. Thank you for getting us here. We will support you!

Amandla!
 
Unajua wakati mwingine usim-judge mtu kwa ukimya wake wakati mwingine ukimya wa Mbowe ndo unaiweka CHADEMA pale ilipo! japo unaafiki ya kuwa CHADEMA imeongezeka viti unasahau kuwa imeongeza viti hivyo chini ya uenyekiti wa Mbowe na viongozi wengine kuanzia Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu (mikakati na mipango ilifanyika chini ya uongozi wake kwa kushirikiana na wengine)!

Jamani tuache kunyanyapaa.. Zitto itafika wakati atapata huo Uenyekiti au Ukatibu Mkuu anaoutaka! uchaguzi wa vyama utakuja tena! na si kwa jinsi anayotumia sasa kwa ku-discredit the current leaders (naomba ajifunze hili)! Meanwhile siwezi afiki mtu mwingine yeyote kupewa uongozi wa kambi ya Upinzani Bungeni zaidi ya Mbowe maana hiyo itakuwa ni kum-discredit kiongozi wa chama ilhali yupo Bungeni na nathani wenzetu walioanza demokrasia mapema waliliona hili ndo mana kama chairman wa chama ni Mbunge anakuwa kiongozi pia wa chama hata Bungeni!

Tuache ku-pin point individuals unfit for our personal weaknessses like judging someone on identities! na kuwa-discredit for misjudging their merits, uongozi si kupayuka tu! na busara ya kuwaweka wenzako woote pamoja na kusikiliza mawazo ya wengine jamani! Hebu imagine kama Mh Zitto angekuwa Chairman wa chama katika lile suala la Dowans halafu akatofautiana na wenzie juu ya Msimamo; what would have happened? si chama kingalifia mbali kama NCCR-Mageuzi (Mchawi angetafutwa!) lakini impact yake ilikuwa ndogo kwa vile position yake si nzito kama ya chairman...!

Jamani tuwe na subira, Zitto anapaswa kukomaa zaidi haswa kwenye maswala ya ndani ya chama na overall party stands vs public affairs! Kuna mambo hayapaswi kuenda nje na personal stands without reservation of other opinions ni sumu kwa chama haswa kama ukiwa kiongozi wake! nasema hivi kwa sababu so far sijaona issue zozote ambazo zingeweza kuleta mtafaruku kama uliotokea hapo kabla ukimhusisha huyu ndugu yetu..! Ajifunze na uchaguzi unakuja ajipange vizuri na ajaribu kuepuka media katika baadhi ya maswala!
Geza Ulole, amini usiamini, sina tatizo na Mbowe kuwa ndiye kiongozi wa upinzani bungeni tatizo langu ni si lazima awe yeye simply kwa sababu ni Mwenyekiti. Nimezungumzia point muhimu sana inaypotwa powers from within, Dr.Slaa anayo na Zitto anayo, sorry to say, Mhe. Mbowe hana!.

Victory yoyote hupatikana kwa consolidation of powers na kuzipangia strategies, ndio maana hata vitani, majemedari sio wakaao mstari wa mbele kwenye the line of fire, wanaokaa mbale ni wapiganaji, Mbowe ni Jemedari wenu, Zitto ni mpiganaji wetu. Nafasi ya kioungozi wa upinzani bungeni, haimuhitaji jemedari, inamhitaji mpiganaji kushusha vipigo tuu.

Bunge lililopita, Hamad Rashid ndio alikuwa kiongozi naye ni too diplomatic ila waelewa wanajua it was powers za Dr. Slaa ndizo zilizokuwa major factor of which I doubt kama Mbowe ataruhusu powers za Zitto zimbypass.

Dhana ikijengeka, hata kama ni ya uwongo, hugeuka sumu, maadamu chama Chenu Chadema, tayari kimegubikwa na dhana fulani fulani, msisubiri uchaguzi sijua miaka mingapi ijayo, you have to act fast, kama niliwashauri CCM, Makamba ni liability kwa chama chao, ameshawacost dearly, wakisubiri mpaka 2012 wakati wa uchaguzi wao mkuu, demage inazidi kuongezeka itafikia wakati itakuwa too little too late!.

Naomba nisieleweke kama nampigia chapuo Zitto, nimemtaja tuu kwa sababu nina uhakika na uwezo wake, kumfukuza kafulila was a mistake, lili lilikuwa jimbo lenu, kumuengua Mwera was a mistake, jimba mmelitoa sadaka, sasa vitu kama hivi ni vi cancer vidogo vidogo vinavyoitafuna Chadema from within, cancer ikigundulika, inakatwa kabla haijasaambaa, ama nayo isubiri uchaguzi?.
 
"Dr.W.Slaa

Sijui kama JK anaweza akasoma na kuelewa analysis yako. Labda azungukwe na watu watano wa kumwelewesha. Kwa upande wa Pasco Naamini amekuelewa.

Baada ya hayo machache, nikupongeze kwa campaign nzuri na ya mafanikio. Hakika Tanzania si ile ya zamani. Hata kama officially wewe si Rais wa JMT, watu wote tunakukubali na kukuombea heri na fanaka. Moto uliowasha cheche zake zitabaki mioyoni mwetu and God willing, Tanzania itarudi kwa watanzania. Mungu Ibariki Tanzania.
 
Geza Ulole

You said it all. Binafsi Zitto namkubali sana na najua is a very potential future Leader, lakini pia anachangamoto nyingi zingine umeshaziongea.

Uchaguzi 2010 Zitto kafanya kazi kubwa hadi kusaidia kampeni za wagombea wengine wa CHADEMA, that is a track record. Ingawa pia kwa kiwango hich wengine pia walifanya kama Ndesamburo, Mbowe nk.

Katika uchaguzi huu, Zitto alipenda aonyeshe "Ushindi wa Nyumbani" - I think yeye aliita Homebase kwa maana ya kupata asilimia kubwa sana ya ushindi isiyo na mashaka. bila ya shaka kajitahidi. Hata hivyo Kigoma ainashikiriwa zaidi na NCCR.

Zitto amekuwa ni muumini wa Kuunganisha vyama. namkubali sana kwa hilo. Na amelisema kwa uwazi sana. I support the move lakini kwa vyama visivyo mamluki au vitakavyobadilika.

Tuko pamoja jamani. Tutafika.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Pasco,

Ni kweli kwamba CCM imechokwa na kuna ukweli kwamba CHADEMA inahitaji kujipanga mapema kwa ajili ya 2015. Lakini naomba kutofautiana kwa kiasi fulani na hoja zako kuhusu kambi ya upinzani na pia ku-revamp CCM.

Kumuondoa Makamba na kuwaweka damu changa akina Nape, Kippi, Makamba Jr na wengineo, haiwezi kuwasaidia CCM. Tatizo ni mfumo mzima wa CCM. Hao vijana unaowasema wanaweza kuishia kwenye secretariat ya Chama lakini hawana maamuzi ya mwisho. Wenye maamuzi ya mwisho ni CC na NEC, na wenye nguvu zaidi ni CC. Ukiangalia CC imejaa hao hao wenye mawazo ya akina Makamba. Mfano mzuri ni Mama Makinda aliposema anavyoelewa yeye ni kwamba fisadi ni mwizi wa wake za watu, lakini akawa amesahau kwamba Bunge la Jamhuri ya Muungano lilishatumia neno hilo hilo kwa maana tofauti na aliyoisema yeye, na pia yeye mwenyewe alishatumia neno hilo hilo kwa maana ile ile tunayoifahamu sisi. Kwanini leo hii ageuke ghafla na kuanza kutupatia tafsiri ya kwenye Kamusi? Makinda anaingia kwenye CC sasa anaenda kuwa mmoja wao. Utakuwa umemtoa Makamba umemuingiza Makinda wenye mawazo yale yale ambayo yanaficha ukweli.

Ushindi wa JK haukuwa wa 60%, alipata pungufu ya hizo, na yeye anajua hilo. Hilo pekee ni jibu tosha kwa JK ambaye alisema 70% ya wapiga kura wa Tanzania ni bendera fuata upepo, na ndio maana alikuwa anatarajia kupata more than 80%, kwamba 70% ya akina bendera fuata upepo + 15 ambao wanampenda na wanamuelewa. So zile 15% ndio wangegawana Dr. Slaa, Prof Lipumba na wagombea wengine. Aibu aliyo nayo ni kubwa kuliko unayoisema wewe hasa akikumbuka hilo tusi alilotutukana watanzania.

Nije kwenye swala la Kambi ya Upinzani: Binafsi nilitamani sana vyama vya upinzani vyote vyenye wabunge ndani ya Mjengo waungane pamoja ili wawe na sauti kubwa na umoja, lakini pia nilikuwa ninasita kwa kiasi fulani hasa nikizingatia mseto wa Zanzibar. Kumbuka kwamba wabunge wa kuchaguliwa wa CUF kutoka Bara wako 2 tu, na viti Maalum nadhani kama 4 hivi, the rest wanatoka Zanzibar. Kule Zanzibar CCM na CUF wana mseto, ni rahisi sana kutumia huo mseto kuwa-influence wabunge wa CCM huku bara ili waweze kuiunga mkono CCM kwenye jambo lolote. Yaliandikwa mengi kuhusu makubaliano binafsi ya Januari Makamba na Jussa, na wao walisema yalikuwa personal, hata kama ni personal, Jussa ana influence kubwa ndani ya chama chake na ni mtu wa karibu sana Maalim Seif.

Mrema tulimsikia akimpigia debe JK wakati wa kampeni na ilihali chama chake [TLP] kilikuwa na mgombea wa nafasi hiyo. Mpaka sasa ameishaonyesha wazi kwamba yeye atakuwa pro-CCM, kwa hiyo ukimuweka kwenye kambi ya upinzani ni sawa na kuweka nyoka chumbani ambaye ana sumu maana siku yoyote anaweza kukudhuru.

Mwaka jana, Mzee Cheyo alitimliwa kwenye nafasi yake ya uwaziri baada ya kwenda kinyume na msimamo wa kambi ya upinzani. Mtu kama huyo huwezi kumtegemea, na ameishasikika mara kibao akisema JK ni safi.

NCCR Mageuzi siwezi kuwasemea, maana hao vijana wote siwafahamu, zaidi ya kujua kasheshe za uongozi wao tu.

Ili kambi ya upinzani iwe na nguvu lazima wapinzani wote wawe na agenda moja na msimamo ulio na lengo moja. Lakini ukiangalia maelezo yangu hapo juu kila chama kinaonekana kina agenda yake na hivyo it is much easy kambi hiyo kusambaratika au kwenda kuumbuana ndani ya vikao vya bunge.

Binafsi ninaweza kusema kwamba muafaka wa CCM na CUF kule Zanzibar ni chanzo kikubwa cha kutokuwa na kambi moja ya upinzani yenye nguvu. Ili kuimarisha zaidi huo muafaka, usije ukashangaa ukisikia JK ameteua mwaka CUF mmoja kwenye zile nafasi 10 ili kupunguza makali ya CUF kwenye Bunge.
 
Mbowe ni Jemedari wenu, Zitto ni mpiganaji wetu. Nafasi ya kioungozi wa upinzani bungeni, haimuhitaji jemedari, inamhitaji mpiganaji kushusha vipigo tuu.

maadamu chama Chenu Chadema...

Naomba nisieleweke kama nampigia chapuo Zitto, nimemtaja tuu kwa sababu nina uhakika na uwezo wake, kumfukuza kafulila was a mistake, lili lilikuwa jimbo lenu, kumuengua Mwera was a mistake

Unaandika kama mtu mwenye bifu na Mbowe. Connect dots kwenye reds and then blues! You will get to know whether you are biased or not!
 
Pole kwa kutopata ushindi uliotarajiwa, ila amini usiamini, wewe bado ni mshindi kwenye roho za watu, na JK ni mshindi kwenye makatasi ya kura. Tunatakiwa kuwa wa shukrani kwa kidogo chochote tunachopata, wewe mwenye majimbo 5 hadi 22 na la 23 ni kesho, ulitakiwa kuonyesha appreciation kwa Watanzania waliokuamini, kitendo cha kususia kutangazwa matokeo for whataver reasons, ni political immaturity, na binafsi nilifadhaishwa sana, umepoteza the golden opportunity ya kuspeak out you mind, hata kama hatimaye utakuja kuita waandishi na kuyasema ya moyoni, never will they have the impact kama ungejitokeza pale na kusema nimekuja siyakubali matokeo kwa sababu yamechakachuliwa.

La kambi ya upinzani, nimelisemea, if you go by the books, it is ok kwa vile nyinyi peke yenu mnaconstitute ile quoram kwa mujibu wa kanuni, don't play by the book, just play by reality, logic and moderation. Umimi wenu Chadema, haujaanza leo, msipokubali weaknesses zenu, you can not turn them ito streghths. Naomba nisiende tena kwenye personalities zaidi, tunakuomba kaa siti ya mbele, shika usukani, pangeni safu yenu vizuri, futeni dhana zote zilizojengeka dhidi yenu ziwe za kweli au za kizushi, 2015 ikulu ni yenu, maana wale milioni 12 waliojiandikisha halafu hawakupiga kura, ndio mtaji wenu wa 2015 haswa ukizingatia vijana wa shule za kata ndio watakuwa vyuoni!.

Pasco, binafsi nadhani bado haumtendei haki Dr. Slaa, kama ungekuwa na subira ya kutaka kujua kwa nini Dr. Slaa hakuja kwa kupata first hand information toka kwake, bila ya shaka ungekuwa na maoni tofauti. Sisi tuko mezani tunasubiri chakula, Dr. Slaa yuko jikoni, kuchelewa kufika kwa chakula haina maana kuwa ametunyima nafasi ya kula. Alishaongea kuwa kuna data anakusanya. Several times mwenyewe amesema si mtu wa kukurupuka bali huja na facts mkononi. Hebu tuwe wavumilivu tumpe nafasi.

Hoja yako ya pili sijui kwa nini bado unadhani Dr Slaa anakwenda by the Books. amekupa mifano hai ya Mabunge ya US na UK na bado unasefikiri hayuko really. Kumbuka nchi alizotaja ni wakongwe wa siasa kuliko TZ. Siasa za Tanzania ni bado Changa sana. Kwa kuanzia tu, jiulize kwa nini 42% ya Watanzania wamepiga kura. Is this something to do with CHADEMA au Dr. Slaa au Mbowe nk?
 
I support 100% Dr. Slaa Peoples President.

Pasco in several occasion binafsi nimekuwa nikifuatilia post zako, mara nyingi tunapofuatilia kukuuliza maswali ya kimsing kama "source" au "basis" ya unachoandika huwa hutoi majibu.
Superman, ni kweli sometimes huwa sisemi source ya baadhi ya thread zangu, hii inakubalika kwa kutumia msingi unaitwa 'the confidentiality of the source', unamhifadhi ili kumlinda. Moja wa hawa ma souce ni yule aliyeniambia hata kura zipigwe vipi, CCM imeshinda kwa 80%, nilishambuliwa sana, ila ilimaanisha walijipanga wajitangazie 80% walipoona imeleak, ndipo wakatangaza walichotangaza.

Hata hivyo huwa unakuwa mwepesi sana kukimbilia katika hoja nyepesi. I think to my opinion that is wrong. Wakati mwingine binafsi huwa nafikiria kuwa una "ego" ambazo unapenda sana kujinyanyua. Mara nyingi huwa unakimbilia kuanzisha baadhi ya threads hata kama unajua fika threads zinazofanana na hizo zipo, that is wrong.
Hili la hoja nyepesi nalikubali,na linatokana na kiwango cha kichwa changu ni chepesi tuu, ziwezi kuja na hoja mzoto za lever ya kina Mzee Mwanakijiji, ni mpaka ni kicha cha level hiyo. Uzito wa hoja ni lever ya kichwa husika, kwa hili nakubali mimi mwepesi.

Hili la "ego" na kujinyanyua ni relative, mimi najiona niko chini usawa wa mavumbini, sijawahi kusema shughuli zangu nini, naishi wapi, maisha yangu yakoje ili tuu nisionekana najinyanyua, ukweli mimi ni mtu wa chini sana, na ni kawaida watu wa chini, kutaka kujinyanyua ili angalau waonekane wako juu, pont noted nitabaki uvunguni.
Ila la kuanzisha thread zinazofanana,hili sikubaliani nawe, kwa vile mimi huanzisha thread za aina mbili tuu, ya kwanza ni kuhusu event fulani, na wakati huo mimi huwepo hapo kwenye event phisically, hutokea nimeshapost kumbe kuna mwingine naye alianzisha kabla yangu, mfano mzuri ni juzi wakati wa matokeo ya uchaguzi, nikiwa chumba cha kutangaza matokeo nikaanzisha kumbe kuna member kaona life kwenye tv akanitangulia, thread yangu ilifungwa na niliupdate thread iliyotangulia.
Aina ya pili ya thread zangu, ni my opinion, hii huusu mawazo na mitazamo yangu binasi kama thread hii. Ila pia nitafuatilia kwa karibu to make right the wrong ones.

Leo umekutana na Dr. wa ukweli, mzoefu wa kisiasa na President of the People, sijui utajibu nini.

Binafsi nilibahatika last year kuongea kwa simu na Dr. Slaa, kubwa lilikuwa kutaka kumpa changamoto kwa nini wasiunganishe nguvu na CUF, NCCR, UDP n.k. Facts nilizopewa nillishiwa nguvu na kujua hakika ni vyama vipi vinakwamisha upinzani. In short CHADEMA walionyesha kwa vitendo huko nyuma kwa kuamua kutosimamisha mgombea wa Urais ili kumuunga yule wa CUF. Iliniuma sana kwa nini vyama vingi mamluki wa kweli. Niliongea na viongozi wa vyama vingine viwili na sikuona seriousness yoyote.

Dr. Slaa tunashukuru sana kwa kupata muda kuja kujibu hoja zetu. Tunakuthamini sana kuliko unavyodhani. A quick scan ya post mbalimbali hapa ni kipimo tosha ya kiasi gani wewe binafsi na CHADEMA mnakubalika. Afterall there should be a start. Rome was not built in a single day. Thank you for getting us here. We will support you!

Amandla!
Superman,
Asante tena,
Amandla!
Pasco.
 
Geza Ulole, amini usiamini, sina tatizo na Mbowe kuwa ndiye kiongozi wa upinzani bungeni tatizo langu ni si lazima awe yeye simply kwa sababu ni Mwenyekiti. Nimezungumzia point muhimu sana inaypotwa powers from within, Dr.Slaa anayo na Zitto anayo, sorry to say, Mhe. Mbowe hana!.

Victory yoyote hupatikana kwa consolidation of powers na kuzipangia strategies, ndio maana hata vitani, majemedari sio wakaao mstari wa mbele kwenye the line of fire, wanaokaa mbale ni wapiganaji, Mbowe ni Jemedari wenu, Zitto ni mpiganaji wetu. Nafasi ya kioungozi wa upinzani bungeni, haimuhitaji jemedari, inamhitaji mpiganaji kushusha vipigo tuu.

Bunge lililopita, Hamad Rashid ndio alikuwa kiongozi naye ni too diplomatic ila waelewa wanajua it was powers za Dr. Slaa ndizo zilizokuwa major factor of which I doubt kama Mbowe ataruhusu powers za Zitto zimbypass.

Dhana ikijengeka, hata kama ni ya uwongo, hugeuka sumu, maadamu chama Chenu Chadema, tayari kimegubikwa na dhana fulani fulani, msisubiri uchaguzi sijua miaka mingapi ijayo, you have to act fast, kama niliwashauri CCM, Makamba ni liability kwa chama chao, ameshawacost dearly, wakisubiri mpaka 2012 wakati wa uchaguzi wao mkuu, demage inazidi kuongezeka itafikia wakati itakuwa too little too late!.

Naomba nisieleweke kama nampigia chapuo Zitto, nimemtaja tuu kwa sababu nina uhakika na uwezo wake, kumfukuza kafulila was a mistake, lili lilikuwa jimbo lenu, kumuengua Mwera was a mistake, jimba mmelitoa sadaka, sasa vitu kama hivi ni vi cancer vidogo vidogo vinavyoitafuna Chadema from within, cancer ikigundulika, inakatwa kabla haijasaambaa, ama nayo isubiri uchaguzi?.

Kuasha mwanangu... Kafulila ni sisimizi.. Kule Kigoma NCCR inakubalika zaidi ya CHADEMA toka 2000 na 2005 sio tatizio.. Kuhusu Mhe. Zitto sio kweli kwa kuwa hata CHADEMA kiliwasaidia vijana wengi kugombea Zitto akiwa mmojawapo tena chini ya Mhe. Mbowe...

Ni juzi tuu Zitto kaomba msamaha kuhusu msimamo wake kuhusu mashine za Dowans.. He called it a flawed thought lakini chama chini ya Slaa na Mbowe waliweka msimamo tofauti na Zitto na ikagundulika na Zitto Mwenyewe kuwa alikosea na akaomba msamaha watanzania...

Acha kulala na umimi ulionao kuwa shujaa mwenzio anakiri kukosea na anakuwa shujaa zaidi lakini wewe huzingatii haya kuwa Zitto ni mtoto kisiasa na bado anakuwa chini ya Slaa na Mbowe... Bless him cause He can bend the way but he can simply apologise!!!
 
Pasco ana point anatakiwa point zake zichukuliwe kama anagalizo zuri kwa Chadema,

Kuhusu Analysis yake amekiri hakwenda deep ila still naona kitu ktk maneno yake.

Naumngana mkono na Slaa kuhusu hali ya upinzani sasa CUF wako na serikali Znz ni ngumu sana kuwaita wapinzani n.k
 
Dr. Slaa, asante sana kwa kunijibu, kitendo tuu cha kuonyesha umenisoma, hiyo ni faraja tosha kwangu kuwa hata kama hamtayarekebisha mapungufu, my only defence ni kuwa tuliwaambia, mesej sent.

Kwa kuanzia, nakupongeza sana wewe binafsi kugombea, umeleta changamoto ambayo haijawahi kutokea.Ushindi wa hayo majimbo mliyoyatwaa ni uthibitisho wa the powers within you. For the first time in my life, nimehamasika na naweza kutupa karata yangu mahali 2015.

Pole kwa kutopata ushindi uliotarajiwa, ila amini usiamini, wewe bado ni mshindi kwenye roho za watu, na JK ni mshindi kwenye makatasi ya kura. Tunatakiwa kuwa wa shukrani kwa kidogo chochote tunachopata, wewe mwenye majimbo 5 hadi 22 na la 23 ni kesho, ulitakiwa kuonyesha appreciation kwa Watanzania waliokuamini, kitendo cha kususia kutangazwa matokeo for whataver reasons, ni political immaturity, na binafsi nilifadhaishwa sana, umepoteza the golden opportunity ya kuspeak out you mind, hata kama hatimaye utakuja kuita waandishi na kuyasema ya moyoni, never will they have the impact kama ungejitokeza pale na kusema nimekuja siyakubali matokeo kwa sababu yamechakachuliwa.

Nakubaliana na wewe kuhusu weakneses kwenye analysis yangu, infact kitu nilichokisema hapa, its only my observation. True analysis inapatikana baada ya kufanya research, nakiri sijafanya research yoyote serious zaidi ya observation tuu, ila hili jicho langu ndilo la mwananchi wa kawaida kule kijijini na sio jicho la reseacher as a member of academia.

La kambi ya upinzani, nimelisemea, if you go by the books, it is ok kwa vile nyinyi peke yenu mnaconstitute ile quoram kwa mujibu wa kanuni, don't play by the book, just play by reality, logic and moderation. Umimi wenu Chadema, haujaanza leo, msipokubali weaknesses zenu, you can not turn them ito streghths. Naomba nisiende tena kwenye personalities zaidi, tunakuomba kaa siti ya mbele, shika usukani, pangeni safu yenu vizuri, futeni dhana zote zilizojengeka dhidi yenu ziwe za kweli au za kizushi, 2015 ikulu ni yenu, maana wale milioni 12 waliojiandikisha halafu hawakupiga kura, ndio mtaji wenu wa 2015 haswa ukizingatia vijana wa shule za kata ndio watakuwa vyuoni!.

Asante tena.

Pasco,

Naona bado tatizo lako liko pale pale: unataka kulazimisha kitu ambacho hakiwezekani ile mradi tu message yako iwe sent!, Hata sisi wananchi wa vijijini unaotusemea kuwa hatuelewi haya mambo tayari tumeshatambua kuwa CUF imeshajiunga rasmi na CCM!. Hivi kuna tija gani kutaka CHADEMA lazima ishirikishe CUF kwenye uongozi wa vyama vya upinzani bungeni wakati CUF tayari wako serikalini???:bowl:

Suala la kwanini mhe. Zitto asiwe kiongozi wa upinzani bungeni nalo halina mantiki kwa sababu mhe. Zitto tayari ni makamu wa kiongozi wa upinzani bungeni. Kwanza hivi bunge lililopita wakati mhe. Zitto akishirikiana na Dr.(Ph.D) Slaa kutoa hoja nzito nzito bungeni mbona hakuwa kiongozi wa upinzani bungeni?. Mhe. Mbowe ni kiongozi wa chama na kwa bahati nzuri naye amefanikiwa kuwamo bungeni, ndio maana emeendelea kuwa kiongozi wa wabunge wake kule mjengoni. Lakini hili halimzuii Mhe Zitto ama kamanda SUGU kutoa hoja zao na kuzizimamia kisawasawa kule mjengoni.

Dr.(Ph.D) Slaa alishasema kwamba tusubiri CAHDEMA kama chama watakuja na maelezo ya kina kwa wananchi juu ya nini kilitokea wakati wa uchaguzi na nini cha kufanya huko mbeleni lakini wewe unaita ni political immaturity! . Bila shaka siku ile angeenda pale, wewe ungekuwa ni mtu wa kwanza humu jamvini kumtuhumu kwanini alihudhuria!!!

Kwakuwa umekiri mwenyewe hukufanya research ni vema ufanye research kabla ya kutoa maoni ambayo yanaweza kuleta mgawanyiko usio na msingi haswa kipindi hiki ambacho tunatakiwa kushikamana zaidi.

Unaandika kama mtu mwenye bifu na Mbowe. Connect dots kwenye reds and then blues! You will get to know whether you are biased or not!
The Dreamer, asante kwa angalizo hilo, naadmit mistake pale niliposema wenu na wetu, hivyo nami kujionyesha ni kama Chadema flan, sorry nikosa, sina bifu yoyote na Mhe. Mbowe, who am I?. I'm nothing ila nakiri udhaifu kuwa Zitto namkubali sana mpaka kupoteza objectivity, nitajirekebisha thanks again.
Pasco
 
Back
Top Bottom