Ccm imebuni mkakati wa kujisafisha kwa kutumia fedha za walala hoi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ccm imebuni mkakati wa kujisafisha kwa kutumia fedha za walala hoi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Byendangwero, Jan 1, 2011.

 1. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #1
  Jan 1, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru wa Tanzania bara yaliyo tangazwa na rais Kikwete kuwa yatasherekewa nchi nzima kwa nderemo na vifijo, yana lengo la kuwapumbaza watanzania ili waamini kuwa CCM ya sasa ndiyo ile ile iliyo hasisiwa na Baba wa taifa mwaka 1977. Rai yangu kwa watanzania wote, bila ya kujali itikadi ya chama, ni kwamba tusikubali kuyumbishwa; nchi yetu hivi iko kwenye wakati mgumu,kila kukicha tunashuhudia nchi yetu inageuzwa shamba la bibi, rasilimali zetu zinaporwa huku tulio wakabidhi jukumu la kuzilinda na kuhakikisha zinatumika kwa faida ya sote wakichekelea. Katika hali hiyo hakuna sababu yoyote ya kuteketeza mabilioni ya fedha ya walala hoi kwa ajili ya sherehe.
   
 2. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #2
  Jan 1, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Uhuru kwenye swamp la umaskini? I doubt it!
   
 3. N

  Nonda JF-Expert Member

  #3
  Jan 1, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,960
  Trophy Points: 280
  Mkuu,

  Unafanya jambo zuri kuwakumbusha wanaJF hasa wale wanaofurahi, wanaojifurahisha kuwa CCM hawana hela na kwa hiyo inakufa taratibu.
  CCM wanaonekana ni wabunifu katika kukihuisha chama chao, japo kwa njia za matata matata, mashaka mashaka.

  Wao wapo kimaslahi zaidi ya kichama kuliko Taifa.
  Sherehe hizo ni njia moja wapo wa kuteketeza hela ya kodi ya mlalahoi, hela ambayo ingetumika kujenga japo zahanati mbili, tatu huko vijijini.

  kwa maoni yao, sherehe hizi zitatusaidia kukuza uchumi!!!
   
 4. tzjamani

  tzjamani JF-Expert Member

  #4
  Jan 1, 2011
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 997
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Viongozi wetu wanafikiria sherehe tu kila wakati. Hivi hawaguswi na kina mama na watoto kufa kwa kukosa huduma za afya? watoto wanakaa chini hata dawati 1 shida kupata.
  Sijui wana mioyo ya mawe????????????!!!!!!!!!:embarrassed:
   
 5. The Hunter

  The Hunter JF-Expert Member

  #5
  Jan 1, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 1,049
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Maadhimisho huku umaskini unazidi kushika chati, wajinga wanaongeza kwa serikali kushindwa kuajiri walimu, maadhimisho huku Maradhi kama malaria, kipindupindu,pepo punda, bado ni tatizo!
  Maonyesho huku hata spoons tunaagiza nje? power tiller ambazo vijana wetu wa Veta na Magereza wangewezeshwa wangeweza kuzitengeneza lakini bado kwa umbumbumbu wetu tuna agiza China ili kukuza uchumi wa wenzetu? Maadhimisho huku magari yaliyobuniwa na vijana wetu wa jeshi, magari aina ya Nyumbu, hatujataka kuweka nguvu pale,sijui nikwakuogopa yakiendelezwa Mashangingi hayatanunuliwa tena!! Tuna adhimisha nini!! Vichwa vya Wendawazimu
   
Loading...