CCM Imeanza kutumia Magazeti Mahiri Kuijeruhi CHADEMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM Imeanza kutumia Magazeti Mahiri Kuijeruhi CHADEMA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Joblube, Apr 20, 2011.

 1. J

  Joblube JF-Expert Member

  #1
  Apr 20, 2011
  Joined: Mar 4, 2011
  Messages: 367
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Nimesoma makala ya Mwandishi Lula Wandali wa Raia Mwema na niegundua kuwa CCM inakakati wa kutumia majarida yanayoaminiwa sana na Wananchi kumaliza CHADEMA. Kwenye makala yake yenye kichwa 'Itashangaza kama Chadema kikipoteza nafasi hii adimu". Binafsi nilitarajia mwandishi achambue nafasi Chadema ilizonazo za kujiimarisha zaidi kuelekea uchaguzi ujao kinyume chake habari inaeleza jinsi CCM inavyoipiga bao CHADEMA kwa kutekeleza hoja zake eti mwisho wake CHADEMA watakosa cha kuwaeleza wananchi kwenye uchaguzi ujao. Labda mwandishi anashindwa kuelewa kuwa mgunduzi wa hoja na anayekopi hoja ni tofautikabisa katika kuielezea hoja usika. Tazama CCM wanavyobabaika kwenye hili la Katiba mpaka wanachomoa hoja bungeni nani amejipatia sifa kwa sasa. Kilichonishangaza zaiidi ni pale mwandishi anapomalizia hoja yake kwa kusema " Chadema hawana nafasi ya kufanya vizuri uchaguzi ujao 2015 kama huu wa 2010 bila ya kutoa hoja za msingi.

  Pia ukitazama kichwa kikuu cha Gazeti hili cha 'Chadema yakana kubeba mafisadi' ujanja umetumika kufikisha ujumbe wa jinsi CCM inavyajiimarisha. Hii inaashiria huko tuendako usishangae Raia mwema likaanza kushambualia CHADEMA.
  Angalizo kwa CHADEMA ni kusoma alama za nyakati na kujiandaa na chanagamoto hii na siku simbali mtaamini haya nisemayo. Hata hivyo wanapaswa kujua Jenerali Ulimwengu pamoja na uzalendo wake kwa Tanzania bado ni kada ndani ya CCM.
   
 2. itnojec

  itnojec JF-Expert Member

  #2
  Apr 20, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 2,191
  Likes Received: 223
  Trophy Points: 160
  point taken
   
 3. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #3
  Apr 20, 2011
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,641
  Likes Received: 1,429
  Trophy Points: 280
  sijakuelewa...narrate vizuri point zako tukuelewe
   
 4. Shinto

  Shinto JF-Expert Member

  #4
  Apr 20, 2011
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 1,781
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Unataka magazeti yote yawe pro-CDM?
  Mbona vyama vingine havipewi hata hiyo nafasi ya kutajwa tu na havilalamiki?
   
 5. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #5
  Apr 20, 2011
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Nakubaliana kabisa na angalizo lako kuwa CHADEMA iwe makini na magazeti kama hilo la RAIA MWEMA kwani historia yake inaonyesha ukaribu wa wamililki wake na mafisadi wa nchi hii. Ikumbukwe tu kuwa mtaji wa kuanzisha gazeti la RAIA MWEMA ulichangiwa partly na mapato ya kuuza magzeti ya habari corp. kwa Rostam Aziz; si hivyo tu baada ya Ulimwengu kupata dhoruba juu ya uTanzania wake enzi za Mkapa ,alikuja kombolewa baada ya Lowassa kuukwaa uwaziri mkuu ndipo swala lake likapata ufumbuzi wa kudumu. Ni dhahili basi kuwa historia hii bado inamuweka Ulimwengu kuwa sympathetic na hawa mafisadi ingawa eye na mmoja kati ya hao thee musketeers hawaivi hata kufikia kutaka kutwangana wakati wakila ulabu kwenye kilabu yao ya Legion!!
   
 6. Mwanahakij

  Mwanahakij Senior Member

  #6
  Apr 20, 2011
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 129
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hata wafanyeje, chama cha magamba, wamejimaliza wenyewe! hata usanii wao wa kutumia kibwagizo cha kujivua gamba, ni kujimaliza> Nyoka akijivua gamba anabakia kuwa nyoka tu, hawi mjusi. Sumu ya ufisadi ilishamea na kushamirishwa kwenye mfumo wa ccm. suluhisho si kuvua gamba au kuvaa kanzu mpya wakati sheikh ni yuleyule!
   
Loading...