CCM imara inategemea upinzani wenye nguvu.

kiroba

JF-Expert Member
Sep 10, 2011
324
114
Habari wakuu wana wa JF

Ni matumaini yangu mu wazima wa afya njema na wale wenye matatizo ya kiaafya basi tunawaombea kwa mungu waweze pata ahueni na hatimaye kupona kabisa.

Leo nataka nizungumzie kuimarika kwa chama chetu cha CCM na pia nitatoa tahadhari zitakazokizorotesha chama chetu na hatimaye kukiua kabisa. Nikiwa kama mwanachama wa chama changu cha CCM, binafsi naamini kuwa uimara wa chama chetu utaletwa na ubora na uimara wa vyama vya uponzani. Kwangu mimi nawachukulia hawa wapinzani kama marafiki na ndugu zangu hivyo wao kama wapinzani watafanya kazi yao ya watch dog. Hawa wapinzani wanapokuwa wanafanya kazi yao kwa isahihi wa kuikosoa serikali basi ni kama wanazidi kuipa afya taasisi yetu ya chama tawala yaani CCM. Kwa mantiki hii sioni haja ya sisi kama chama tawala kujikita zaidi kwenye kutaka kiviua ama kuvizorotesha vyama vya upinzani kwani kufanya hivyo ni kuminya na hatimaye kuua kabisa demokrasia.

Kwa mitazamo yangu sisi kama chama tawala hatupaswi kuendesha siasa za kijasusi na hata zile zenye harufu ya kigaidi. CCM yenyewe yapaswa kujikita kwenye kuisimamia serikali ya chama chake ili iweze kukidhi matakwa ya watanzania. Siasa za kijasusi na zile zenye harufu ya kigaidi hazina matokeo mazuri kwa chama chetu ambacho ndio muasisi wa amani ya nchi yetu. Hatupaswi kuwa ndio chanzo cha kutoweka amani katika nchi yetu kwa kuendesha siasa za kijasusi na zenye harufu ya kigaidi.

Kupandikiza migogoro katika vyama vya upinzani hakutatusaidia ili sisi kama chama tawala basi tupendwe na wananchi. Kitakachotufanya tuonekane bora katika macho ya wananchi ni zile sera zetu nzuri na zinazotekelezeka. Tuisimamie kwa umakini ilani yetu ya uchaguzi na kutekeleza ahadi zetu tulizotoa kipindi cha kampeni. Na pia kuisimamia uwajibikaji wa viongozi wa chama na serikali. Tukemee rushwa na pia tuwakemee wale wote wenye mayendo ya kifisadi yanayokichafua chama machoni mwa wanachama wetu na raia kwa ujumla.

Nashangazwa sana na utumiaji wa rasilimali kubwa za chama na serikali katika eti kudhoodisha upinzani. Kwangu mimi sioni kama upinzani ni tatizo kwa chama chetu, ila tatizo kuu kwa chama chetu ni hali ya viongozi wetu wa chama kusemwa vibaya mbele ya jamii. Cha msingi hapa ni kulifanyia kazi suala hili ili kukipa chama muonekano mzuri mbele ya jamii. Ifike wakati chama kisiwaonee haya viongozi wenye kashfa. Tukiwatosa hao viongozi wenye kashfa basi chama kitanawiri sana.

Mwisho namaliza kwa kumshukuru mungu kwa kulinda amani ya nchi yetu ambayo ni tunu tulojaaliwa na mwenyezi mungu. Tuiombee amani nchi yetu na pia tuviombee vyama vyetu vyote vya siasa ili viendeshe siasa za kistaarabu na zenye tija kwa taifa. Hatuna haja ya kugombana na kuwekeana visasi hadi tukaelekea kufanya siasa za kijasusi na zenye harufu ya kigaidi. Sisi sote ni ndugu na afrika ni moja hivyo tupendane kama ndugu. Tusieuhusu tofauti zetu za kisiasa hasa itikadi zetu kuzifanya kutuongoza katika chuki na kupeleka nchi katika machafuko.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom