CCM Imara, hongereni mliochaguliwa kupitia jumuia za CCM ngazi ya wilaya

Mfua suleiman

Member
Feb 27, 2014
60
62
HONGERA MLIOCHAGULIWA KUPITIA JUMUIA ZA CCM NGAZI YA WILAYA

Kwa heshima na taadhima napenda kuchukua nafasi hii kuwapongeza wote waliochaguliwa kupitia Jumuia za chama cha Mapinduzi ngazi ya wilaya, Kuanzia WAZAZI, U.W.T na Moyo wa Chama UVCCM.

Viongozi waliochaguliwa na hasa wenyeviti wanapaswa kutambua kua wana jukumu kubwa la kusimamia vyema utekelezaji wa Ilani yetu ya Uchaguzi ya mwaka 2015-2020 katika maeneo wanayoyaongoza.

Viongozi mliochaguliwa mnapaswa kujua kua mmepewa dhamana kubwa ndani ya Chama katika maeneo yenu, hivyo mnatakiwa kuhakikisha Ilani inatekelezwa kama ilivyokusudiwa.

Mbali na hilo, pia mnapaswa kutambua kua kuna changamoto kubwa ya baadhi ya watumishi wa Umma katika maeneo yenu mliochaguliwa ambao wanakwenda kinyume na Ilani yetu,hill msilifumbie macho badala yake ninyi ndio mnaopaswa kua mwarobaini pekee wa kadhia hiyo.

Binafsi Nina matumaini makubwa na wote mliochaguliwa kua mtatekeleza vyema majukumu yenu kwa haki na kwa kufuata katiba na miongozo mbalimbali ya chama chetu.

[HASHTAG]#CcmMpya[/HASHTAG] inayoijenga
[HASHTAG]#TanzaniaMpya[/HASHTAG]

Mfua Suleiman Lwahupa
(Mshamba wa Rufiji)
 
Kumbe Ccm bado wapogo wengi. Nikajua watakuwa wameisha.... Anywahi wengi sasa hivi ni wachumia tumbo.
 
Back
Top Bottom