CCM ilizaliwa tar 3/2/1977

Nakumbuka ule wimbo
"tarehe tano februari thamanini na nane, wananchi wa tabora njoni tushangilie.
twakumbuka, miaka kumi na moja leo ya chama chetu"

Duh, ya mwaka huu kali sijui waliimbaje???!!!!!! wajameni maCCM mmetupa jongoo na mti wake?????!!!!!
 
nshapata picha wasingeadhimisha leo wakaadhmisha j4 wasingepata watu
mkutano ungedoda na wale wabebwa kwa malori na mabasi wasingepatikana
isitoshe wamejaribu kufanya leo ili watu kwa vile ni mapunziko watazame tv zao
uzuri ni kuwa bado chama kimepoteza dira na uelekeo,
Horance Kolimba alikuwa sahihi licha ya mauaji aliyofanyiwa.
sijui kama huwa wanamkumbuka katika maadhimisho haya kama mtu aliekijenga chama
na kusema ukweli alipoona kimepoteza dira na uelekeo wake.
 
wameamua kubadilika mwaka huu kwa sababu ccm wengi ni waajiriwa wameona ni bora wafanye sherehe weekend ili siku ya tarehe 5 ambayo itaangukia siku jumanne watu waende kazini kama kawaida. nawasifu kwa hili kwa kuamua kuijenga nchi kwa vitendo.
Ebu fafanua vizuri unaposema CCM wengi ni waajiriwa ni akina nani hao? usitake kupindisha mada chama kinapokuwa kinaendeshwa kwa kufuata matunguri na utabiri ni matatizo sana hakuna sababu iliyosababisha mabadiriko haya zaidi ya lamri na matunguri.
 
Ebu fafanua vizuri unaposema CCM wengi ni waajiriwa ni akina nani hao? usitake kupindisha mada chama kinapokuwa kinaendeshwa kwa kufuata matunguri na utabiri ni matatizo sana hakuna sababu iliyosababisha mabadiriko haya zaidi ya lamri na matunguri.
mkuu umejuaje kwenye red highlight?
viongozi wengi wingi ni makada wa ccm. hebu fikiria kama ingekuwa tar5 mwakyembe asingekuwepo kazini wala wakuu wa mikua, wilaya na kadhalika.
 
CCM imekufa kabisa! iweje ifanyiwe sherehe ya kuzaliwa wakati iko tumboni mwa TANU NA ASP! Hii inatudhihirishia mwisho wao upo tayari. :nimekataa
 
CCM leo inatimiza miaka 36 baada ya kuzaliwa tar 5.2.2013.
Ninajiuliza ni hofu gani iliyokishika chama kilichokwisha kuvunja ungo kuogopa kufikisha siku ya kuzaliwa.
Wadau na wanaCCM naombeni mnisaidie hapa.

Usihofu Mkuu Ringo ilikuwa kisherehekee tarehe 5.2.2013 Jumanne. Kuna sababu mbili inawezekana zimefanya ifanyike tarehe 3.2.2013 badala yake. Sababu hizo inawezekana ni:-
1. Huenda wale walinzi wa Sheikh Yahaya wamemwambia asisherehekee siku ya Jumanne maana wengi wa watu wa namna hiyo Jumanne kwao siyo siku nzuri eti siku ya majini.
2. Sababu ya pili inawezekana kuwa Mh. atasafiri kwenda majuu, si unajua??
 
Ama kweli chama cha zamani kinakufa vibaya kwa kufata kanuni za waganga wa jadi,kumbe kwao hiyo ni siku ya majini ndo maana hawasemi kwanini wamesherekea jana badala ya kesho,kweli mfa maji haishi kujitapatapa.
 
wadau tuliozaliwa miaka ya nyuma tunakumbuka kipindi ccm ikongozwa na baba wataifa,mwinyi na mkapa kila ikifika tar 5.2 tunasherehekea kuzaliwa kwa chama cha mapinduzi.
kila ikifika tar hiyo tuliimba na kucheza na pia bendi nyingi zilipiga nyimbo na kuitaja hiyo siku na tuliifurahia kwa kweli.
swali lililopo kichwani kwangu ni kuwa kesho siku itakuwa je baada ya miaka 36 pale lumumba,ccm makao makuu dodoma na ofisi za ccm nchi nzima?
je ni nani kabariki uhuni huu wa kuikimbia siku iliyoasisiwa na wazee wetu?
je ni baraka za mwenyekiti?
je ni sekretariet mpya?

maswali ni mengi kuliko majibu.
je ikiangukia tar 5.2 siku ya alhamisi tutaisogea ta 7.2 jumamosi au tutairudishatar 31.1 jumapili?
huu ubabaishaji utaendelea hadi lini?

NAPE,KINANA NA MANGULA NAOMBENI UFAFANUZI.
au ndio kila alichokiasisis nyerere mnakiua kifo cha kimyakimya?
au ni azimio jipya la kigoma.

MWENYEZI MUNGU AILAZE MAHALI PEMA ROHO YA BBA WA TAIFA MAHALI PEMA PEPONI.
AAMINA.
 
wadau tuliozaliwa miaka ya nyuma tunakumbuka kipindi ccm ikongozwa na baba wataifa,mwinyi na mkapa kila ikifika tar 5.2 tunasherehekea kuzaliwa kwa chama cha mapinduzi.
kila ikifika tar hiyo tuliimba na kucheza na pia bendi nyingi zilipiga nyimbo na kuitaja hiyo siku na tuliifurahia kwa kweli.
swali lililopo kichwani kwangu ni kuwa kesho siku itakuwa je baada ya miaka 36 pale lumumba,ccm makao makuu dodoma na ofisi za ccm nchi nzima?
je ni nani kabariki uhuni huu wa kuikimbia siku iliyoasisiwa na wazee wetu?
je ni baraka za mwenyekiti?
je ni sekretariet mpya?

maswali ni mengi kuliko majibu.
je ikiangukia tar 5.2 siku ya alhamisi tutaisogea ta 7.2 jumamosi au tutairudishatar 31.1 jumapili?
huu ubabaishaji utaendelea hadi lini?

NAPE,KINANA NA MANGULA NAOMBENI UFAFANUZI.
au ndio kila alichokiasisis nyerere mnakiua kifo cha kimyakimya?
au ni azimio jipya la kigoma.

MWENYEZI MUNGU AILAZE MAHALI PEMA ROHO YA BBA WA TAIFA MAHALI PEMA PEPONI.
AAMINA.
Timiza wajibu wako siyo kuwaza sikukuu ambazo hazina masirahi kwa taifa wakati watu wanalia na njaa hizo hela za maandalizi bora zipelekwe mikoa amayo ina njaa au zitumike kuboresha miundombinu ya taifa fikiri sana acha kuwaza sikukuu ambazo hazina msingi wowote
 
Uchawi huo, kwani mmesahau kuhusiana na jambo hilo? Pili, hawana uhakika na nini kitatokea Bungeni jumatatu na jumanne hasa kutokana na hoja mbili moto za Maji dar ya Mnyika na kuhusu Baraza la mitihani ya Nassari , so wameamua kuiwahisha ,

Ila kama ni mganga aliwaambia , watapaswa kumfukuza kazi ya uganga kwani jana imekuwa ni balaa kwao zaidi maana picha za magazeti ya leo ni mbaya kwao na inaonyesha walivyo watu wa vurugu.........
 
Msinipige mawe kama akina Aden Rage, Jafo, Mutanda, Chatanda, Nyangwini walivyomukumu yule MCHADAEMA kwa mawe jana kule Dodoma.

Nitawanong'oneza masikioni polepole, wamesherehekea 3/02 ambayo ni JUMAPILI kwasababu ya MFUMO KIRISTO :smiling:
 
Waliona kwa Kigoma kupata watu siku ya kazi, kwa vile tarehe 5/2 siyo siku ya mapumziko,si rahisi. Wasingeweza kupata watu wa kuacha kazi zao na kusombwa na mafuso kwenda kwenye mkutano. Hivyo wakaamua wafanye hivyo siku ya Jumapili ambayo ni siku ya mapumziko. Si unajua tena Kigoma ni Mkoa wa Wapinzani!! Anayekufa hutapatapa. CCM bye.
 
Hayawi hayawi sasa yamekuwa,ukificha maradhi siku zote kifo hukuumbua.Nimeanza na misemo hii ya kiswahili kuonyesha kuwa ngoma ikipigwa sana mwisho wake hupasuka.CCM wamefikisha miaka 36 toka kuzaliwa kwake,tarehe ya kuzaliwa kwake kila Mtanzania anaijua kwani tulifundishwa siasa mashuleni wakati ule wa chama kushka hatamu,lakini kwa kukosa umakini wamesherehekea siku mbili kabla ya kuzaliwa..

CCM imezaliwa tarehe 05/02/1977,lakini ajabu na kweli umakini wake umekosekana katika maazimisho ya siku ya kuzaliwa kwa chama hicho na kupoteza ile mantiki ya kufikisha miaka 36.Nasema hivyo kutokana na maazimisho yao kufanyika tarehe 03/02/2013 kabla ya siku mbili ili kuweza kutimiza miaka 36,kimantiki sherehe hiyo ya kuzaliwa haikuwa sahihi kuitangaza kuwa ni miaka 36 bali ni miaka 35 na siku 363.

Hali hii inaonyesha jinsi gani chama hiki kikizidi kupoteza hata zile identity za chama ikiwa ni pamoja na kupotosha historia ya chama hiki kwa kizazi kilichopo.Hali hii ilipelekea mh.Vicent Nyerere kuibeza CCM ndani ya bunge kwa kufikisha miaka 36 hali yakuwa hawajui tarehe yao ya kuzaliwa.
Uko wapi umakini wa kushughulikia matatizo sugu ya wananchi ikiwa hata historia ya kuzaliwa kwa chama hiki imeanza kupotoshwa.
 
Kuzaliwa siku mbili kabla=njiti.
Kuwa na alama ya jembe na nyundo badala ya pochi na bastola.
 
Nahisi Mwaka huu imezaliwa Njiti, yaani Pre mature, hapo utabiri wa namba aliowaachia sheikh HAYAHAYA lazima ume apply...!!!
 
Mwaka kesho 2014 CCM itaadhimisha kuzaliwa kwake tarehe 2.2.2014 ambayo itakuwa ni Jumapili kwani tarehe 5 itakuwa Jumatano. Tehe heeeeee!
 
hivi vyama vingine historia yake ipo wapi??? ........tutendeeni haki watanzania.......mie binafsi najua vingi vimeandikishwa 28 Mei 1992...lakini sijui lini vimezaliwa?......kina nani walihusika katika kuzaliwa kwake?? Itusaidie katika kutunza kumbukumbu....... isije huko baadaye tukawa na historia ya kubabaisha tu
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom