CCM: ILIZALIWA, IKAKUA na SASA INAKUFA

hapana jamani anakili kuwa ccm sasa siyo tena chama imara na chenye uchungu ndo maana anaumia kuona chama chake kinaondoka madarakani ana hitaji msaada wa hali ya juu kukikomboa chama chake cha msimgi ni kumsaidia afanye nn ili chama chake kikapate kuwa na misingi mizuri tena iliyoachwa na baba wa taifa ili wakitoka madarakani wakajipange upya jinsi ya kukianda tena kuja kuchukua nchi kwa badaye sana hata baada ya miaka mia moja,
 
Nakapanya: Unahitaji USHAURI nasaha ili ufahamu kwamba Tanzania yenye matumaini bila CCM inawezekana.

Nenda leo Jangwani ukapate USHAURI nasaha. Why kuendelea kung'ang'ania CCM yenye maovu hayo yote uliyoyataja?! Haiwezi kujirekebisha imefikia mwisho, historia inatufunza hivyo.
 
Karibu cdm uvae gwanda ccm sasa ni km mzoga ndani ya nyumba, unatoa hewa chafu hata uweke manukato gani utendelea kutoa harufu,.
 
Hakika napenda sikuniione CCM mpya,CCM iliyojikita katika misingi yake ya kutetea wanyonge,CCM ya wakulima na wafanyakazi,CCM yenye sera za kweli za kumkomboa Mtanzania kutoka katika lindi la umaskini uliokithiri.Njia moja wapo ya kufikia haponi kurudia miiko na misingi iliyounda chama chetu,kuwatosa makupe (mafisadie),kuwawajibisha wavivu,na kuweka viongozi wenye nia thabiti na uwezo na kuonyesha njia kule tunakotaka kwenda.Tukifanya hivyo hakikia Tanzania yenye maendeleo,amani na utulivu tutaiona.Kamwe sitavaa gwanda na kamwe sitatetea mafisadi.MUNGU IBARIKI TANZANIA.

...ndg yangu labda mafisadi wote wanyongwe.ila kama kwa nape na wenzake bora ufe mapema.,
 
Hakika napenda sikuniione CCM mpya,CCM iliyojikita katika misingi yake ya kutetea wanyonge,CCM ya wakulima na wafanyakazi,CCM yenye sera za kweli za kumkomboa Mtanzania kutoka katika lindi la umaskini uliokithiri.Njia moja wapo ya kufikia haponi kurudia miiko na misingi iliyounda chama chetu,kuwatosa makupe (mafisadie),kuwawajibisha wavivu,na kuweka viongozi wenye nia thabiti na uwezo na kuonyesha njia kule tunakotaka kwenda.Tukifanya hivyo hakikia Tanzania yenye maendeleo,amani na utulivu tutaiona.Kamwe sitavaa gwanda na kamwe sitatetea mafisadi.MUNGU IBARIKI TANZANIA.

KARIBU SANA JF. naona umeingia na mapovu mdomoni.
 
CCM IMARA NA MADHUBUTI IPO NA ITAENDELEA KUWEPO.
CHANGAMOTO ILIYOPO NI KUJIKOSOA NA KUJIPANGA , BADO WANANCHI WANA IMANI NA CHAMA CHA MAPINDUZI.

"chadema kitakufa kabla ya 2015"-Wasira.
 
Mwezi huu wa Mei nimejitahidi kuhudhuria vikao vyote vya Chama changu CCM. Kitu kimoja nilichokutana nacho katika kila kikao ni ajenda ya " KWANINI CCM IMEPOTEZA MVUTO KWA WANANCHI" jambo hili limemitia hofu kama mwana-CCM lakini limenipa faraja kama mpenda mageuzi ya haki.
Siyo siri kabisa CCM inaweweseka kwa hali isiyo ya kawaida, nasema hivyo kwa sababu majibu yaliyokuwa yanatolewa na wajumbe hayakuhashiria kupata ufumbuzi wa kurudisha mvuto kwa chama zaidi kulaumiana na malumbano ya wao kwa wao.
Katika yote kila mzungumzaji alikuwa anabainisha wazi kuwa CHADEMA imekuja kwa Kasi kiasi cha kuhofu kufanyika kwa chaguzi za kuziba nafasi zilizo wazi za wenyeviti wa vijiji na vitongoji kwa hofu ya kushindwa.

CHADEMA wananchi wajenga imani kubwa kwenu, lililosubiriwa ni kuwakabidhi nchi 2015, ombi kwenu jenga mkakati wa mshikamano kama chama na pia hakikisha mnashuka hadi ngazi ya chini. Kuiga siyo vibaya kama inafaa, anzisha mashina kila sehemu na pia jiandae kuweka wagombea kila nafasi kila eneo. Msiruhusu watu wa kupita bila kupingwa.
Kwa kuanzia mwaka huu hakikisha kila kata kuna uongozi wa Chama waliopikwa na kuiva ndio hao wawe makamanda wapiganaji kuelekea vijijini.
Sijui kama CHADEMA mnajitambua mlivyo kwisha ikamata nchi! Wewe fikiria CCM na ukongwe wake mwaka huu karibia ikose watu wa Kugombea nafasi mbalimbali za chama kuanzia hao mabarozi, na viongozi wa matawi na kata. Walikuwa wameweka vigezo vya mtu kugombea lazima awe amelipa ada ya uanachama walipokosa wakaondoa hicho kigezo mambo yawe kanyaga twende, hata baada ya kuondoa hiyo hali haikubadilika sana ndipo walijitokeza watu wasio na mshiko kuanaza kugombea. Ukiona baadhi ya watu waliokamata nafasi za uongozi katika mashina utashangaa sana, hasa ukizingatia kuwa CCM ni chama tawala. Watu wenye akili zao wanakwepa bila kutoa sababu za kukataa kwao wazi wazi.
Ngazi za kata nako vile vile, uchaguzi huu haujafanyika kisa wagombea hawajapatikana katika baadhi ya nafasi! inashangaza kwa CCM kubembeleza wagombea. Hivi katika kili unadhani itapata viongozi wenye uwezo wa kukitetea chama katika siasa za ushindani? La hasha. CHADEMA jiandae kuongoza nchi.
Wakati mnajiandaa naomba nilete maombi yaha kwenu

1. Msilipize kisasa kwa viongozi wa CCM kwa madhambi yao bali jiweke kuwa mfano ili watanzania wajifunze na kubaini
jinsi ambavyo viongozi wao walikuwa chanzo cha matatizo yao kwa kuona mabadiliko kutoka kwenu.
2. Mtusaidie kuziba pengo la walionacho na wasionacho ili kuleta mshikamano wa kitaifa.
3. Amsha ari ya watanzania katika kuipenda nchi yao ili watu wajivunie kuitwa watanzania.
4. Msijenge tabaka la kifalme kama walivyojijengea viongozi wa CCM maana sasa kinachochukua nafasi si uwezo wa
mtu bali ni mtoto wa nani.
5.Naomba mtakapo ingia madarakani jaribu kila liwezekanavyo kupunuza garama za serikali, kwa kuanzia punguza
wizara ikiwezekana kwa kuanzia zisizidi 10 na baada ya hapo kufikia mwaka 2020 iwe wilaya moja jimbo la uchaguzi
moja.
6. Viwanja vyote vya michezo vyote viwe mali ya Serikali maana CCM ilifanya kujimilikisha lakini vilijengwa kwa fedha
za watanzania wote.

Naomba wana JF muongezee mengine ambayo mnataka CDM itufanyie pale itakaposhika uongozi wa nchi ili waanze kuona nini wanachi wanataka kungali mapema.:spit::spit:
 
kwa hiyo umetupa manyanga chini sisiem ukaamua kutoa ushauri wako hapa au undumilakuwili unaendelea.
 
1. Msilipize kisasa kwa viongozi wa ccm kwa madhambi yao bali jiweke kuwa mfano ili watanzania wajifunze na kubaini
jinsi ambavyo viongozi wao walikuwa chanzo cha matatizo yao kwa kuona mabadiliko kutoka kwenu.
[/b]2. Mtusaidie kuziba pengo la walionacho na wasionacho ili kuleta mshikamano wa kitaifa.
3. Amsha ari ya watanzania katika kuipenda nchi yao ili watu wajivunie kuitwa watanzania.
4. Msijenge tabaka la kifalme kama walivyojijengea viongozi wa ccm maana sasa kinachochukua nafasi si uwezo wa
mtu bali ni mtoto wa nani.
5.naomba mtakapo ingia madarakani jaribu kila liwezekanavyo kupunuza garama za serikali, kwa kuanzia punguza
wizara ikiwezekana kwa kuanzia zisizidi 10 na baada ya hapo kufikia mwaka 2020 iwe wilaya moja jimbo la uchaguzi
moja.
6. Viwanja vyote vya michezo vyote viwe mali ya serikali maana ccm ilifanya kujimilikisha lakini vilijengwa kwa fedha
za watanzania wote.

Naomba wana jf muongezee mengine ambayo mnataka cdm itufanyie pale itakaposhika uongozi wa nchi ili waanze kuona nini wanachi wanataka kungali mapema.:spit::spit:

hakuna kulipiza kisasi kama unavyofikiri na kuomba, ila inabidi kujenga utamaduni wa kuwa honesty ambao wtz wengi tumeupoteza, hivyo wale wenye makosa kama mafisadi, kutumia vibaya madaraka nk ni lazima wafikishwe kwenye vyombo vya dola i.e mahakamani hivyo ukweli upatikane huko kama hawana makosa warudi uraiani, kama wana makosa basiw aende kunyea ndooni kama kawaida ilivyo kwa wakosefu. hii itarudisha nidhamu
 
Uchunguzi wa karibuni kabisa unaonyesha dalili zifuatazo:-

1/Zaidi ya 50% ya mtandao wake nchi nzima umekufa (eg. kufa kwa miradi,mwitikio mdogo kwenye chaguzi za ndani na kukosekana kwa pesa za kutosha kujiendesha kwenye jumuiya, mashina na matawi)

2/Kushindwa kwa secretarieti ya chama mara mbili mfululizo ndani ya miaka sita tu (Ilianza ya Makamba Senior sasa ya Mukama).

3/Kasi ya kukimbiwa na wanachama wake nchi nzima inayoendelea sasa.

4/Kuongezeka kwa idadi kubwa ya makada mamluki ndani ya chama (wako kusaka vyeo na ulaji na hawana mapenzi ya dhati kwa CCM)

5/Kuzidi kupoteza mvuto kwa wananchi wa kawaida (eg. matokeo ya chaguzi ndogo,idadi na hamasa ndogo kwenye mikutano)

6/Vita sugu za makundi ndani ya chama kuwania vyeo (eg. Urais,ubunge,ujumbe wa vikao vikuu vya chama,uongozi wa chama)

7/Kukua kwa kasi kwa chama pinzani hususani Chadema.

8/Kuongezeka kwa uolewa wa wananchi kunakochangiwa na vyombo vya habari na mitandao.

9/Hatua za CCM kujiandaa kuwa chama cha upinzani siku zijazo (eg.mapendekezo ya NEC ya CCM kwenye mchakato wa sasa wa katiba mpya kuhusu mgombea binafsi,kupingwa kwa matokeo ya urais mahakamani)

10/Kutokuaminiana tena baina ya viongozi waandamizi wa chama (eg. Kuvujisha siri za vikao,fununu za kulishana sumu na ushirikina, siasa za kupakana matope, tishio la mauaji ya kutengeneza, kitisho cha kuvuana magamba, fununu za kuhamia upinzani)

*SOURCE: Ripoti ya kikao cha NEC ya CCM (May 2012) ,Maoni ya baadhi ya wahadhiri wa vyuo vikuu, wadadisi na wachambuzi kadhaa wa kisiasa Tanzania.
 
kumtumia mtu asiye na mvuto kama Dr. Bana kukipamba.
 
Suluhisho la tatizo si kulikimbia bali ni kulikubali na kutafuta njia na mbinu sahihi ya kulitatua,naamini kwa CCM itaweza kufanya hivyo na kuingia madarakani tena mwaka 2015 kwa kishindo zaidi,CDM tunomba muendelee kuvaa magwanda ili muimarishe ulinzi wa nchi yetu na tunashukuru kwa hilo.
 
Chama kipya cha upinzani kijacho ni sisiem tena kisipoangalia kitakuwa chama lege lege cha upinzani.
 
Nakapanya kumbe na wwe nimwa sisiem?wwe nimtoto wakigogo yupi?sisiem niya matariji,vigogo,watoto wao,wake zao.ssa wwe upo kundi lipi?wakati mnaendelea namchakato wakukijenga upya chama chenu,inabdi mbadirishe nembo yachama.toa jembe na nyundo weka kisu na kijiko mpaka mkimaliza ujenzi.
Mimi si mtoto wa kigogo,si mtoto wa fisadi bali ni mtoto wa mfanyakazi mstaafu,CCM haina mwenyewe,ngoja nikuulize; hv ulishawahi kuangalia muundo wa kiuongozi wa cdm?je umewahi kuangalia viongozi waliopo ndani yake?na kama ulifanya hvyo unajua uhusiano mwingi uluiopo kati ya viongozi hao?naomba majibu
 
Back
Top Bottom