MAHANJU
JF-Expert Member
- Aug 26, 2014
- 5,244
- 7,970
Tangu jana nililisema hili na leo nalisema tena, inapotea CCM ilivyokua na mbinu za kila aina,inapotea CCM iliyokua imesheheni wazee wa propaganda! Eti inazaliwa CCM mya ya kina Pole pole khaaa!
Vijana kama kina Mwigulu,Nape na Makamba,Jerry Slaa na wengine ndio waliokua na amsha amsha ila kwa sasa inaonaonekana ni kama wamepigwa ganzi sijui ni ya nini!na sio hii ya kina pole pole na Bashite wanaowekwa msitari wa mbele kupambana na kina Lissu na Lema ati ndio CCM mpya.
Jana niliwaponda vijana wa CCM kuwekeza nguvu nyingi kwa propaganda za kutukana watu, kubeza wapinzani,kujidai ati ninyi mna dola,kuandaa makundi kwenye mitandao ya kijamii na kijifanya wao ni vijana wa CHADEMA, hizi ni mbinu zilizokufa! Kama hamtaki kukubaliana na hilo subuirini muda unakwenda na mwisho jibu litapatikana.
UVCCM mmekaa kimya kutetea asiyekua na vyeti vya shule mnajifanya kuzipuuza kelele za wapinzani na kauli yenu ya "hapa kazi tu# huku kazi hamfanyi mnachekelea bila kujua kua wapinzani wako strategical zaidi kwa kila yanayotokea, mnawaita wapinzani manyumbu watu wa matukio! Maskini hamjui kua pia siasa ni matukio.
Mnachekele kufukuzwa maelfu ya wanachama kwa madai ya kukisafisha chama mkasahau kua kuna mtu moja anayewachafulia chama na mizaha yenu matunda yake mtayapata muda si mrefu. Kama mnafikiri kutimua watu kwa visasi mnajenga basi subirini.
UVCCM mlishindwaje kupeleka pendekezo kwa mwenyekiti wenu kua hamtaki mtu flani anawachafulia Chama ili kuilinda taasisi ya chama chenu,mmemwacha hebu sasa angalieni aibu anayoifanya kwa kuvamia ofisi za watu kwa sababu ya upeo wa akili yake iliyoshindwa shule ni.
Nawaambieni endeleeni kuamini kua mtu wenu anaandamwa kwa sababu ni mpiganaji mzuri juu ya watumiaji na wasafirishaji wa Madawa ya kulevya. Ndio mawazo yenu yalivyo! Mlishindwaje kujiuliza inakuwaje yeye peke yake alivalie njuga suala la Madawa ya kulevya bila kutaka ushirikiano kwa wenzake wote ispokua kwa mzee Madabida tu ambaye naye kumbe hamkua na imani naye.