CCM ilivyoitia nuksi Bongo Movie

My Son drink water

JF-Expert Member
Nov 30, 2016
4,932
13,283
Kilichowakuta wasanii wa Bongo movie ni fundisho kubwa kwa wenzao wote wanaopenda hiyo sanaa ili kufanikiwa kimaisha.

Wasanii wa Bongo movie walisahau kuwa watanzania wapo matabaka tofauti. Wapo wasio na vyama, wapo walio CCM na wapo Wapinzani pia. Badala ya kufanya biashara, Bongo movie walianza siasa tena kwa kulalia CCM utadhani CCM ndo huwa inanunua kazi zao pekee...

Na hasa ikizingatiwa kwamba Watanzania 85% hawaipendi kabisa CCM kwa kuwaletea umaskini mkubwa, na CCM wanalijua hilo ndo maana inawapasa kuishi kwa kupumulia Police Kama Oksijen yao na TISS Kama dripu zao.

Watanzania kwa hasira waliamua kususa kununua kazi za Bongo movie baada ya baadhi ya wasanii wa Bongo movie kuanza kutoa kashfa kwa watanzania wasio CCM.

Njaa iliwapiga wasanii wakakosa mwelekeo na kuanza kuweweseka,ndipo wakamlilia mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Mh Makonda, naye kwa kukosa Hekima akajaribu kuzindua Kampeni ya kuzuia watanzania wasinunue filamu za nje, bali wanunue filamu za Tanzania tu, ili kuwanusuru Bongo movie wasife njaa.

Kampeni ya Makonda haikufanikiwa, njaa ikaendelea kuwatesa Bongo movie kwa filamu zao kukosa mvuto kwa jamii kwa sababu ya U CCM wao.

Mwisho wa siku Bongo movie ikafa kifo cha mende, Viongozi wa Bongo movie kina Steve Nyerere ndo waliponza wenzao.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu,kwa hishma na taadhima nakupa siri;Unabishia kiuno!Kama CCM inajiamini isingetafuta "wrong-cuts" kukwapua uongozi.Refer:Uchafuzi Local Government!
Unanitus bila sababu , Okey thibitisha kuwa 85% ya watz hawaipend CCM, ukishadhibitisha ndo tutajua Nani anabishia kiuno
 
Unanitus bila sababu , Okey thibitisha kuwa 85% ya watz hawaipend CCM, ukishadhibitisha ndo tutajua Nani anabishia kiuno
Sorry mkuu!Uwe mfuatiliaji wa hali halisi ya maisha ya Watanzania kwa nyakati hizi.Utaelewa tu.Tena muandishi ameremba.Hawampendi Magufuli! Swallow it ninja!😂😂😂😂
 
Sorry mkuu!Uwe mfuatiliaji wa hali halisi ya maisha ya Watanzania kwa nyakati hizi.Utaelewa tu.Tena muandishi ameremba.Hawampendi Magufuli! Swallow it ninja!😂😂😂😂
Siwez kumeza makapi, hzo ni story za vijiweni, leta official documents zinazoonyesha now umaarufu wa JPM ni 15%
 
Siwez kumeza makapi, hzo ni story za vijiweni, leta official documents zinazoonyesha now umaarufu wa JPM ni 15%
Unataka nyaraka za kiserikali hizohizo ambazo huwa zinakaangwa na kuchakachuliwa?Ooh...Lord!Unatakiwa kuombewa uwe huru.
 
Mkuu inaonekana umeishia la saba
Mkuu kwa nini unanikweza hivyo?Mimi ni la tatu "Chee"!niliyeamua kuuza mayai yaliyochemshwa stendi kuu!Huwa mnapenda mdanganywe kwa "mitakwimu" na orodha nyingi za uongo.Kwani hali halisi hauioni?Umefumbwa kwa kulazimishwa kuomba data kimaandishi ili uwekewe ukomo wa fikra.Funguka,toka kwenye kibuyu!🤣🤣🤣🤣
 
Hawa jamaa walikuwa wanatana kweli kipndi kile bt siku hzi wamesharudisha mpira kwa kipa wamebakisha show off za kule fb na insta
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom