CCM ilivuna mbegu za walalahoi zilizopandwa shamba la DECI

Mwakitobile

JF-Expert Member
Oct 4, 2012
452
120
CCM wanapora kila kitu alichonacho mwananchi wa kawaida.Yapata miaka miwili au mitatu sasa,toka serikali ya chama tawala ikamate mabilioni ya pesa za walalahoi waliyopanda katika taasisi isiyo ya kiserikali DECI kama upatu,kesi ipo mahakamani kwa muda mrefu sasa,lakini maendeleo yake hayaridhishi,kwani ushahidi upo wazi kabisa.Je ni kweli serikali ya chama tawala ilikuwa na nia ya dhati ya kuokoa pesa za walalahoi kutoka mikononi mwa waliowatuhumu kama matapeli,? au walichukua pesa hizo kwa ajili ya matumizi ya kampeni mwaka 2010?..Tutaongea ukweli tu hata kama kesi bado ipo mahakamani,kwani mahakama zetu ni sehemu za kupoka,kuchelewesha na kukandamiza haki za walalaho kupitia maagizo ya serikali ya wanamagamba.
 
Afadhali mbegu zingeendelea kuwa deci kwani huenda wapandaji wangevuna kuliko sasa miaka mitatu kimyaaaa!!!!
 
Afadhali mbegu zingeendelea kuwa deci kwani huenda wapandaji wangevuna kuliko sasa miaka mitatu kimyaaaa!!!!

Kama walikuwa wanavuna kila baada ya miezi 3, sasa miaka 3 hao ni matajiri sio wenzetu.....Mie niliogopa kupanda pesa
 
Hawakomi hawa watu wee angalia Sizonje hadi za rambirambi kalamba. Juzi tu katia fora kalamba zaidi ya 1.5T. utadhani mchwa wenye meno ya chuma
 
Nilipanda mbegu aseee... nakumbuka Mizengo Pinda.. sio mtu mzuri bilion 13
 
Back
Top Bottom