Paul Alex
JF-Expert Member
- Jul 14, 2012
- 4,342
- 9,824
Kikwete anaweza kupumzika sasa, kumbe sio yeye tu!
Muda mfupi tu wa uongozi wa Magufuli umeonyesha hili.Magufuli anajaribu kufanya tofauti na anaumiza kichwa kupata kuungwa mkono na watanzania walio wengi ila katika mazingira ya upepo mkali na mawimbi ya kisiasa ambayo kwa bahati mbaya hakujiandaa nayo na huku akiwa na mchanganyiko wa wanasiasa ambao kwakweli kama wangekuwa ni vinywaji basi cocktail yake ingekufanya uumwe na tumbo.
Angalia ; huku Makonda kule Muhongo, huku Nape kule Makamba na Mwakyembe katikati yao : cocktail ya ajabu zaidi kuwahi kutokea katika historia ya dunia hii~ muendelezo wa mvua ya makosa!
Marais wengi hupotea katika ramani za siasa kwasababu ya timu zao za siasa kufanya kazi chini ya kiwango.
CCM kwa hakika walikuwa na imani kuwa Serikali yao chini ya Magufuli itafanya kazi vizuri zaidi ya ile ya Vasco da gama (Mkwere original).Ukiangalia mvua ya makosa inayoendelea baada ya serikali ya Magufuli kuanza kazi lazima CCM iwaze mara mbili.
Kama serikali ya kikwete ilikuwa chini ya kiwango basi haikuwa mbali sana na ya Magufuli.Hata kwa rais mwenye shauku na nia kama ya Magufuli atapata ugumu kugeuza hii cocktail ya wanasiasa wa CCM ikaribie kufanana na timu ya utekelezaji.
CCM inaweza kuwa sahihi kuwa na sura kama ya Magufuli kwenye nafasi ya uraisi.Magufuli ana baadhi ya vigezo ambavyo chama kilichochoka kama CCM kinavihitaji. Ila atafeli kama sura zilezile za watu walioshindwa na kushindikana zitaendelea kujionyesha katika timu yake ya kisiasa.
Kinana alizunguka nchi nzima na akaja na ripoti ya hali halisi ya chama, CCM ikaona jinsi ilivyooza. Kitengo kikakaa, kikasema lazima tuje na njia mbadala, na wakapata njia; Magufuli ~ mchapa kazi, mtiifu na mwanasiasa wa bei nafuu anayeweza kuiba hoja zote za upinzani > angalau kwenye akili zao walifikiri hivyo.
Ulikuwa mkakati kabambe wa kubaka demokrasia na kupulizia chama pumzi mpya ya uhai. Mkakati huu ungefanikiwa kwa asilimia mia ungekuwa mkakati kabambe zaidi kuwahi kutokea Tanzania.
Ila kitengo walisahau kitu; kwa bahati mbaya kwa CCM, mabadiliko ambayo Ukawa ilikuwa ikiyahubiri yalishaanza kwenye mioyo ya watanzania.
CCM ilishaonekana chama cha kizamani na mwanamke mzee hata umpake wanja vipi lazima makunyanzi yatamuumbua!
Kwa vijana CCM ilishaonekana kama kiatu cha chakacha ambacho mwisho wake wa kukivaa ni saa sita ya mchana kabla jua halijaanza kutoka.
Kuweka tu kwa njia rahisi, kitengo hawakujua tu kama CCM ilikuwa inatumia muda wa kuazima na kizazi cha sasa, ukiacha wale ambao CCM kuwa madarakani inamaanisha chakula mezani, hakina muda tena na CCM.
Sahau Magufuli, sahau kitengo; haya ni majira ya upinzani kushamiri.
Kama serikali ikifanya vibaya ni kawaida kwa Magufuli kulaumiwa.
Japo Magufuli bado mgeni sana kuchukua lawama hizi nyingi pamoja na kuwa anaonekana kupata wakati mgumu na Ombwe la wanasiasa aliorithi. Kumudu serikali Magufuli anahitaji muda, uzoefu na uwezo vyote ambavyo hana.
Magufuli ataangushwa na wanasiasa aliorithi ambao si tu kwamba wana chapa na nembo ya kikwete, bali wana chapa na nembo ya CCM.
Ni ngumu katika hesabu kuona Magufuli akifanikiwa na ndio maana nadhani CCM ilihitaji mapumziko zaidi kuliko Magufuli.