CCM ikiwatimua ‘mapacha watatu’ tutawapokea-AFP | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM ikiwatimua ‘mapacha watatu’ tutawapokea-AFP

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by issenye, Jun 16, 2011.

 1. i

  issenye JF-Expert Member

  #1
  Jun 16, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 1,151
  Likes Received: 992
  Trophy Points: 280
  [h=1]CCM ikiwatimua ‘mapacha watatu’ tutawapokea-AFP[/h] Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
  [​IMG]CHAMA cha Wakulima Tanzania (AFP), kimeweka bayana msimamo wake kuwa ikiwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kitaamua kuwafukuza mapacha wake watatu, chenyewe kitawapokea na kumteua Edward Lowassa kuwa mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
  Mwenyekiti wa Taifa wa AFP, Said Soud Said ameiambia RAI wiki hii katika mahojiano maalumu yaliyofanyika katika eneo la Forodhani kwenye Ukumbi wa Ngome Kongwe mjini hapa.
  Said amesema kimsingi CCM inajaribu kutaka kukamata kaa la moto kiganjani na hilo ni jambo la hatari kwao ikiwa itaamua na kuazimia kuwatimua mapacha hao watatu bila ya kupima upepo ulivyo.
  Alisema mapacha hao wana haiba, mvuto na nguvu ya ushawishi wa kisiasa kwa jinsi wanavyokubalika ndani ya umma hivyo chama chake hakitasita kuwapokea na kuwakaribisha kina Andrew Chenge, Rostam Aziz na Lowassa ili kuwa wanachama wake wapya.
  “Tutawapokea kwa nderemo, shangwe, vifijo na hoihoi, hawa ni raia wenzetu, si wahamiaji wa nchi hii, tunaamini ni wasafi, waadilifu na wachapakazi hodari ila mbinu chafu za kisiasa zinawapaka matope wasitamanike kwa utashi wa maadui wao,” alisema.
  Mwenyekiti huyo wa AFP amesema Lowassa ni tajiri mno katika siasa za Tanzania asiyelingana na mwanasiasa yeyote hasa katika kufikia kwake uamuzi wa kujiuzulu uwaziri mkuu na kukaa pembeni ili kuipisha Kamati ya Bunge la Tisa ifanye kazi yake kwa uwazi na hatimaye kubaini ukweli juu ya sakata hilo ambapo yeye ilibainika hakuhusika.
  “Nakuuliza mwandishi ni mwanasiasa yupi ndani au nje ya Serikali ya CCM aliyethubutu kufikia uamuzi uliofanywa na Lowassa, viongozi wengi wameboranga lakini wamebaki kuwa ving’ang’anizi wa madaraka. CCM kabla ya kufikia hatma ya jambo hilo kwanza itafakari kwa kina athari na faida kabla ya kupitisha uamuzi huo wenye majuto kwao,” alisema Said.
  Anaongeza: “Tuhuma pekee haitoshi kusimama kama ushahidi kamili na kufikia kuwaita au kumwita mtu fulani ni fisadi, makosa ya jinai, madai au mauajia yanahitaji ithbati ya vyombo vya kisheria hasa mhimili wa mahakama. Huu unaotaka kufanywa na CCM ni uonevu na ukatili usiostahili kwa raia yeyote kufanyiwa.”
  Alipoulizwa ikiwa AFP na wanachama wake hawaogopi kuwapokea watu hao wanaoshukiwa kuwa kujihusisha na ufisadi, Said alisema hiyo ni hadithi ya kupika na hekaya ya kutengeneza ili kuwatia madoa ambayo kwayo hayana ukweli na ushahidi kamilifu.
  Alisema ikiwa CCM itaamua kuwafukuza wanachama hao wanotuhumiwa kujihusisha na vitendo vya ufisadi vya kufikirika chama basi hicho chote kitamalizika kwa kuwa idadi kubwa ya wanachama na viongozi wake wana utajiri usioelezeka kwa namna walivyoupata.
  “Namkaribisha sana Lowassa na mapacha wake kwa mikono miwili kuhamia AFP, waje haraka, hatutasita kumtangaza Lowassa kama mgombea wetu wa urais mwaka 2015, naamini atashinda kwa kishindo na ndiye Rais ajaye mwaka 2015 Tanzania,” aliongeza Said.
  Aidha, mwenyekiti huyo aliongeza kusema kuwa watu wanaotuhumu kwamba viongozi hao ni mafisadi hawaelezi kwa yakini kile walichofisidi wametenda kosa lipi ila mbio za urais bila shaka ndizo zinazowagharimu na hasa Lowassa.
  Alisema uwezo wa Lowassa ni mkubwa na umeonekana wakati akiwa Waziri Mkuu na kwamba rekodi yake bado haijafikiwa na kiongozi yeyote kati ya walioteuliwa na Rais Jakaya Kikwete katika awamu ya nne.
  “Huyu anafanana na Jacob Zuma wa ANC nchini Afrika Kusini. Rais Jakaya Kikwete kama anapuuza nguvu za Lowassa kisiasa akubali kufanya mabadiliko ya katiba ya CCM kisha Lowassa, Fredrick Sumaye, John Malecela na Rais Kikwete wagombee nafasi ya uenyekiti kama Lowassa hakuibuka kidedea,” alisema.
  Rais Zuma aliwahi kumbwaga Thabo Mbeki wakati akiwa madarakani na yeye kuwa Rais wa ANC huku baada ya kumshinda katika uchaguzi mkuu uliokuwa na mbinde huko Polukwane Afrika Kusini huku akiandamwa na kashfa za uuzaji wa silaha, rushwa na ubakaji.
  Habari zidi zinaeleza kuwa tayari Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Pius Msekwa amekutana kwa nyakati tofauti na wajumbe hao watatu wa NEC ya CCM katika Ofisi Ndogo ya CCM Lumumba huku Lowassa akisisitiza msimamo wake kuwa hajatenda kosa na hastahili kusulubiwa.
  Tarifa zaidi zinasema kuwa Msekwa alimweleza Lowassa na kumtaka aachane na mbio za urais lakini hata hivyo akashindwa kueleza sababu za kumkataza ambapo Lowassa alisema si dhambi ikiwa anataka kufanya hivyo ashinikizwe kuacha kutimiza haki yake ya kikatiba na kidemokrasia.
  Hata hivyo, Mwenyekiti huyo wa AFP Said alisisitiza kuwa yeye na chama chake wanauelewa uthubutu, ubunifu na uhodari wa kupanga mikakati alionao Lowassa na wenzake katika kuhamasisha dhana ya maendeleo hivyo wakiamua kuhamia AFP itakuwa ni kama kuramba raha ya ushindi.
   
 2. Borakufa

  Borakufa JF-Expert Member

  #2
  Jun 16, 2011
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 1,503
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Ni ngumu sana mapacha watatu kutoka ccm
   
 3. NgumiJiwe

  NgumiJiwe JF-Expert Member

  #3
  Jun 16, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 867
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Haya sasa kazi imeanza.Lowasa ashaahidiwa nafasi tayari ya kugombea urais 2015.CCM mko tayari kum release?au porojo tu
  Nimependa aliposema Kikwete abadili katiba ya CCM halafu agombee uenyekiti na Lowasa na Malecela na Sumaye.Naona jamaa anamkubali sana Lowasa huyu!
   
Loading...