El Roi
Senior Member
- May 29, 2020
- 183
- 321
Binafsi, kwa dhati ya moyo wangu, napendezwa na approach ya mheshimiwa Rais wetu namna anavyoyaona mambo na anavyoongoza kwa ujumla. Nafurahia utulivu wake na alivyo juu ya mambo ( over board).
Mtu anapokuwa over board maana yake ni kwamba kayamudu mambo, anafuata mifumo na anakuwa na picha kubwa juu ya anayoyafanya. Anaona mbele kabla hali yenyewe haijatokea ( pro active) na hana mihemuko ( reactive).
Kuna wakati hapo nyuma, baadhi yetu hatukufurahia namna mambo yalivyokuwa yamekaa. Ubabe, vitisho , kukosa mifumo iligeuka kuwa order of the day. Kwa muda huu huoni hiyo. Tunamshukuru sana Mungu. Sasa tunategemea tu kuyaona maendeleo maana sifa kuu za msababisha maendeleo ( Rais) huyu wa sasa anazo.
Baada ya hayo na nia njema ya Rais wetu juu ya kuleta maendeleo mapana( inclusive developments), shida yangu Sasa inabaki kuona kama chama chake kina uwezo wa kujigeuza na ku accomodate falsafa na maono ya Rais. Katika kuongoza nchi.
Kwangu Mimi CCM ni chama kigumu sana kubadilika kwa maana pana . Ni rahisi kubadilika wao kwa wao kama wanataka kufanya jambo lao, lakini mabadiliko mapana yanayoingiza jamii pana au sema nchi, ni wagumu sana kubadilika
Labda kiasi utaona mabadiliko kwenye sughuli za kiuchumi. Wanajitahidi na kiasi kikubwa wanafanya vizuri. Mahali ambapo hawa jamaa nawaona vigumu kubadilika ni katika siasa na uongozi wa nchi.
Namkumbuka Rais msitaafu Jakaya, alivyokuwa na Nia ya dhati ya kutafuta katiba mpya. Ni ukweli uliowazi kwamba Jk alikuwa kiongozi wa wakati, aliyeona mahitaji ya wakati na alipenda demokrasia. Niambieni kama alifaulu katika dhima yake ya kupata katiba mpya. La hasha!
Tunajua jinsi alivyogeuka na akawa self contradictory Kwa mambo ambayo alitaka yawepo.
Angalia jinsi alivyopiga nyundo m apendezo yaliyoratibiwa na timu ya watu nguli na aliowateua m wenyewe.
Unadhani alikuwa yeye? CCM walikuwa nyuma. Hawakutaka mabadiliko yale kwa sababu yalikuwa yanatoa nafasi ya wao kuwa mashakani kuchukua madaraka na uongozi, ambavyo tayari CCM wanaona wao ndo tu wanafaa kuwa hivyo.
Rais wetu ana maono ya Sasa ya namna nchi zinavyotakiwa kuongozwa. Na nadhani mnaona anavyo behave. Swali tata ni kwamba atafanikiwa?
Tangu ameingia madarakani, tumeona jitihada zake mbalimbali za kuunda timu kadhaa za Siri na za wazi ili kufanya nchi itulie na iongozwe kistaarabu( professionally). Kubwa nitakalolisemea ni kamati aliyoiunda ya kuangalia mabadiliko ya katiba. Je atafanikiwa ?
Hivi kweli hii kamati itakapopendekeza mabadiliko yanayopaswa ( Tangible) kama ilivyokuwa tume ya Warioba, CCM watakubaliana na Rais ambaye ndo Mwenyekiti wao?
Mifumo ya nchi na mazoea yanaibeba CCM katika mambo Mengi. CCM hawa ninaowajua watakubali kweli mabadiliko makubwa hasa yanayoleta usawa wa yeyote na chama kingine kushika madaraka??
Nionavyo mie mabadiliko anayoyatafuta Rais yako likely kutopatikana kwa sababu Chama chake hakijajigeuza kabisa kujua wakati huu na kuacha ubinafsi.
Hivi CCM wataridhia usawa katika kufanya siasa, kukubali kushindwa kwenye sanduku la kura, tume huru ya uchaguzi inayowaweka nje wakurugenzi ambao ni turufu yao kwenye uchaguzi?
Kuna maandiko katika msaafu wa wakristo yanayosema" huwezi kuweka divai mpya katika kiriba ( chupa) ya zamani.
Naiona CCM kama kiriba Cha kale ambacho hakiwezi kukubali kabisa, usasa katika kuongoza nchi. Je dhamira njema ninayoiona kwa Rais wetu itafanikiwa? Anaweza kisimamia mambo mwenyewe wakati CCM wanapinga?
Tujipe muda, ingawa maombi yangu ni kwamba CCM ibadilike ili ku accomodate mabadiliko chanya katika uongozi wa nchi na kuifanya nchi kuchanua.
Wasalaam.